Mara ya mwisho lini ulimchekesha mpenzi wako?

BAOSITA

JF-Expert Member
Nov 2, 2011
368
188
Habari zenu wadau wa hii sekta!Swali ndio hilo hapo juu!
Wengi wetu huwa tunajidai tupo seriously busy na pilikapilika za kila kukicha na kusahau kwamba wenzi wetu wanahitaji kufurahishwa nasi,mwishowe mkeo anachekeshwa na muuza vyombo halafu inakuwa balaa..!Teh teh teh!
Kumbuka bila kicheko maisha yanazidi ugumu!
 
Kabisa kabisa nakubaliana na wewe...mapenzi sio kilio, lazima muwe mnafurahi...majokes yawe kwa wingi tu na kicheko ni dawa ya mapenzi.
 
Nimeshaona watu wengi wanaojidai serious,wamekwapuliwa wapenzi wao na watu wacheshi!Kaa chonjo
 
Hivi haya maisha vile ambavyo jk ameyafanya yawe magumu namna hii,bado tu kuna watu wao kutwa nzima wanawaza kuchekeshana?
 
Kwani mie "ze komedi"?akawape tu huko wanaomchekesha hovyo!yan ntafute pesa na pia ntafute na kichekesho cha kuja kumchekesha mwanamke?khaa!
 
Nakumbuka mpenz wangu aliniambia anapenda sana kucheka,kujichek mimi sio mcheshi kiviiiiile! Basi nikawa narudi home na mikanda ya vichekesho!! Ila siku moja nikamletea kinywaji akalewa basi akawa anacheeeeka,nikimuulza jina lako nani daaah atavunja mbavu! Nikawa nimegundua mbinu ya kumchekesha badala ya mikanda nikawarudi na vinywaji!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom