radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
- Thread starter
- #21
I agree, demokrasia ina gharama zake.....
Hata hivyo, haya matumizi yaliyorekodiwa hapa ni ufisadi mfupi kwa jina la "demokrasia ni gharama"....
Hebu cheki hii, eti TShs 629,000,000 zimetumika kwa ajili ya CHAKULA na VIBURUDISHO...
maswali ni haya:
1. Kina nani walikuwa wanakula chakula hiki?
2. Aina gani ya chakula?
3. Kina nani walikuwa "wanaburudishwa" na "kurutubishwa"?
4. Ikumbukwe kuwa kuna posho za kujikimu kwa kila aliyeshiriki zoezi hili. Hivi, unapopewa posho ya kujikimu si ndiyo gharama zako za malazi, chakula, kujiburudisha nk zinakuwa ndani? Iweje kuwe na fungu separate tena la chakula, VIBURUDISHO na virutubisho na wakati huo huo kuna posho???
4. Hivi tukisema, serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli Pombe ndiyo imefungulia bomba la ufisadi tunakuwa tunakosea wapi???
5. Je, huu si ndiyo ushahidi usio hata na chembe ya shaka?
6. Iweje majimbo matatu tu yatafune billion 270 wakati majimbo 265 yalitumia kiasi pungufu ya hicho?
7. Serikali inapata wapi uhalali wa kuwachangisha wananchi elfu 10 ama 20 ama 50 eti kumchangia ujenzi wa madarasa ama zahanati wakati kuna kikundi kidogo cha watu kinafuja fedha na kodi zetu kiasi hiki???
HAPANA, HILI HALIKUBALIKI. tusidanganyane, tukatae hili. TUSEME wote ENOUGH is ENOUGH!!!
Watu wamepiga sna hela ni hatar sana mkuu mwenyewe nimesoma hata sijaamini