Mapya yaibuka uchaguzi wa marudio majimbo matatu

Kitaturu,
Hakuna haja ya kuumiza kichwa kwa maswali kama hayo...!!
Ukweli ni kwamba FEDHA HII YOTE ILIKUWA NI PAMOJA NA GHARAMA ZA KUWANUNUA HAO WABUNGE WALIOKUWA WAKO UPINZANI ILI WAHAMIE CCM, RUSHWA KWA MAPOLISI NA TISS KUHAKIKISHA KURA ZOTE ZINACHAKACHULIWA NA KUPEWA WAGOMBEA WA CCM.....!!!Unakumbuka siku ile baada ya Kutangazwa mshindi Jimbo la UKONGA MAPOLISI WALIONEKANA WAKISHANGILIA NA KUSHEREKEA WAKIWA NA BASHITE.......HAWA NDO WALIOKULA HIYO PESA YA UCHAGUZI...!!

Kuna jimbo kama la Korogwe Vijijini HAKUKUWA NA UCHAGUZI ULIOFANYIKA LAKINI FIGURE IKO PALEPALE...!!
Wote waliotaka kuingia kwenye kinyanganyiro walipewa MPUNGA WA UHAKIKA na wakabwaga manyaga....ili CCM ipite kwa ULAINI.
Kwa lugha rahisi na nyepesi na bila kutafuna maneno... HII NI AINA MOJAWAPO YA UFISADI WA SERIKALI YA AWAMU HII YA 5.
CCM na rushwa ni kama pichu na kotama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi ku-display kitu kama hicho...Hela nyingi imepigwa kwenye RUSHWA NA HONGO KUWARUBUNI WABUNGE TOKA UPINZANI......!!!Kama kuna watu jasiri wafuatilie Account za WAITARA, MOLLEL na KALANGA kama hutakuta mamilioni kadhaa yako huko....kwa ujumnla ni wapinzani wote waliohamia CCM....!!DEMOKRASIA YA TANZANIA INABAKWA MCHANA KWEUPEEEE!!

Hili ni zaidi ya ufsadi. Hii ishara kuwa nchi yetu sasa kweli ni "banana republic",
 
Tena nawashangaa sana, badala ya kujibu maswali mnanivaa mimi? Si kichwani tu, mweupe sehemu nyingi.

Punguani wahed.
Sifa kubwa ya kuwa mwanaccm ni kujitoa ufahamu.

tapatalk_1541697603951.jpeg
ccm.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona shutuma yoyote ya ufisadi hapo au kuwa hizo pesa hazikutumika kama ilivyo paswa. Sijaona mtu yoyote kulengwa kuwa kafanya ufisadi. Naona matumizi tu yamepanda. Jipya lipi?

Matumizi yamepanda kwa zaidi ya 300% ndani ya miaka miwili. Fair enough katika zama za kubana matumizi!
 
Ccm hawajawahi kuwa wasafi
Dar es Salaam. Serikali iliidhinisha takriban asilimia tano ya bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, kurudia uchaguzi katika majimbo matatu mwaka jana.

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/19, inaonyesha kuwa Hazina ilibadili matumizi ya zaidi ya Sh12.4 bilioni kufanikisha uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga, Monduli na Korogwe Vijijini uliofanyika Septemba mwaka jana. Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja alithibitisha kuhamishwa kwa fedha hizo, “Ni kweli fedha hizo zimehamishwa kama inavyoonekana lakini hilo ni jambo moja kujua kama zimetumika zote au sehemu tu. Ni suala ambalo (NEC) Tume ya Taifa Uchaguzi wanayo maelezo sahihi.”

Mwaipaja alifafanua kuwa Serikali hutoa fedha kulingana na mahitaji ya mhusika ambaye baadaye hutakiwa kuthibitisha matumizi yake kwa kuzingatia mchanganuo alioutoa.

Alipoulizwa jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage alishauri atafutwe Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa maelezo kuwa ndiye mwenye taarifa husika.

Alipotafutwa, mkurugenzi huyo Dk Athumani Kihamia alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.

“Nipo kwenye mkutano, nitumie meseji,” alisema Dk Kihamia. Lakini alipotumiwa ujumbe, hakujibu.

Baadaye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James alisema NEC hutengewa bajeti mahsusi kila inapotokea sababu ya msingi.

“Ni waziri wa fedha pekee mwenye mamlaka ya kuhamisha fedha kutoka fungu moja kwenda jingine. Anachokifanya ni kutoa fedha kulingana na maombi yaliyowasilishwa. Tume ya Uchaguzi walifanya hivyo, wakamshawishi waziri kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kwa wastani, bajeti hiyo ni zaidi ya Sh4.1 bilioni kwa kila jimbo, ikilinganishwa na Sh991 milioni zilizotumika kwa kila jimbo mwaka 2015 katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dotto alisema mahitaji ya majimbo hayalingani kwa kuwa hutofautiana ukubwa wa eneo, idadi ya kata pamoja na wapigakura.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni kufanikisha uchaguzi kwenye majimbo 264 ambazo NEC ilitumia Sh261.6 bilioni.

Hata hivyo, katika uchaguzi mdogo, baadhi ya vifaa vilivyotumika ni vile vya uchaguzi mkuu hivyo kuacha maswali kuhusu gharama zake na Jimbo la Korogwe Vijijini halikufanya uchaguzi baada ya mgombea wa CCM, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa.

Bajeti majimbo matatu

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha za Serikali inaonyesha kati ya zaidi ya Sh12.44 bilioni zilizotolewa, Sh3.7 bilioni zilikuwa kwa ajili ya posho maalumu na Sh2.08 bilioni zilikuwa za kujikimu (perdiem) kwa siku 30 za watumishi wa NEC kusimamia uchaguzi huo.

Kwa kuwa uchaguzi huo uliwapa majukumu ya ziada, Sh1.24 bilioni zilitengwa kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa Tume pamoja na Sh917.16 milioni za kufanikisha usafiri wao wakiwa kwenye majimbo na Sh626.21 milioni kwa ajili ya chakula na viburudisho.

Tume ilipaswa kutumia Sh1.22 bilioni kuchapisha na kudurufu nyaraka muhimu kwa ajili ya uchaguzi huo huku Sh105.91 milioni zikitengwa kuwalipa vibarua wakati wajumbe wakitakiwa kulipwa Sh228.41 milioni kwa kuhudhuria vikao.

Sh306.35 milioni zilitumika kwa ajili ya malazi na Sh291.7 milioni kwa ajili ya kukodi magari binafsi. Dizeli Sh548.866 milioni ilinunuliwa na Sh32.4 milioni zikinunua vocha kwa ajili ya mawasiliano ya simu.

Kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, tume ilikodi maturubai na vifaa vya kupigia kambi kwa Sh258.27 milioni huku ikitumia Sh24.19 milioni kuwasafirisha watendaji wake kwa ndege.

Fedha nyingine zilitumika kwa ukarimu (Sh16.45 milioni), vifaa vya ofisi (Sh117.05 milioni), kompyuta na vifaa vyake (Sh72.84 milioni), matangazo (Sh145 milioni), huduma za mzabuni (Sh311.31 milioni) na mikutano ikigharimu Sh177.8 milioni.

Maoni

Ingawa demokrasia ni gharama, Mbunge wa Momba, David Silinde alisema kutenga kiasi kikubwa hivyo ni ufujaji wa fedha za umma.

Alipendekeza kufutwa kwa uchaguzi wa marudio endapo mbunge atahama chama au kufariki basi chama kilichoshinda kijaze nafasi iliyo wazi.

Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi ambaye alihama Chadema na kujiunga CCM alisema “ndiyo gharama za demokrasia. Ndiyo namna pekee iliyopo kwamba mbunge akijiuzulu uchaguzi unaitishwa, hakuna jinsi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Paul Luisulie alisema, “cha msingi vyombo vilivyopewa jukumu la kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma vifuatilie.”

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Bubelwa Kaiza alisema katika utekelezaji wa demokrasia, siyo fedha peke yake zinazoangaliwa bali masilahi ya wananchi.

In God we Trust
 
Mkuu ili ulipate gazeti la mwananchi inakubidi uwe na buku sasa huyo chumia tumbo na mramba viatu wa chakubanga atapata wapi hiyo buku?
Mkuu unabishana na huyo mwehu ambaye hata tofauti ya herufi kubwa na ndogo hajui? Yaani yeye anacomment tu kile kilichomjia kichwani. Hajui hata hiyo taarifa iko gazeti la leo la Mwananchi. Yaani ni shida sana.

In God we Trust
 
Kwa stahili hii kuwachia madaraka kirahisi ni ngumu sana!
Jiwe atavunja rekodi ya ukwapuaji katika shamba la bibi.

Nisikiavyo wakati ule wa uchaguzi alikuwa anasema ni lazima tu shinde, wanaomzunguka walikuwa wanamjibu mzee hii ngoma bila milioni... ni ngumu.

Mzee anainuwa simu na kuamrisha wapewe.

In God we Trust
 
Back
Top Bottom