Mapya yaibuka uchaguzi wa marudio majimbo matatu

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
18,481
Points
2,000

radika

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
18,481 2,000
Dar es Salaam. Serikali iliidhinisha takriban asilimia tano ya bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, kurudia uchaguzi katika majimbo matatu mwaka jana.

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/19, inaonyesha kuwa Hazina ilibadili matumizi ya zaidi ya Sh12.4 bilioni kufanikisha uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga, Monduli na Korogwe Vijijini uliofanyika Septemba mwaka jana. Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja alithibitisha kuhamishwa kwa fedha hizo, “Ni kweli fedha hizo zimehamishwa kama inavyoonekana lakini hilo ni jambo moja kujua kama zimetumika zote au sehemu tu. Ni suala ambalo (NEC) Tume ya Taifa Uchaguzi wanayo maelezo sahihi.”

Mwaipaja alifafanua kuwa Serikali hutoa fedha kulingana na mahitaji ya mhusika ambaye baadaye hutakiwa kuthibitisha matumizi yake kwa kuzingatia mchanganuo alioutoa.

Alipoulizwa jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage alishauri atafutwe Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa maelezo kuwa ndiye mwenye taarifa husika.

Alipotafutwa, mkurugenzi huyo Dk Athumani Kihamia alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.

“Nipo kwenye mkutano, nitumie meseji,” alisema Dk Kihamia. Lakini alipotumiwa ujumbe, hakujibu.

Baadaye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James alisema NEC hutengewa bajeti mahsusi kila inapotokea sababu ya msingi.

“Ni waziri wa fedha pekee mwenye mamlaka ya kuhamisha fedha kutoka fungu moja kwenda jingine. Anachokifanya ni kutoa fedha kulingana na maombi yaliyowasilishwa. Tume ya Uchaguzi walifanya hivyo, wakamshawishi waziri kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kwa wastani, bajeti hiyo ni zaidi ya Sh4.1 bilioni kwa kila jimbo, ikilinganishwa na Sh991 milioni zilizotumika kwa kila jimbo mwaka 2015 katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dotto alisema mahitaji ya majimbo hayalingani kwa kuwa hutofautiana ukubwa wa eneo, idadi ya kata pamoja na wapigakura.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni kufanikisha uchaguzi kwenye majimbo 264 ambazo NEC ilitumia Sh261.6 bilioni.

Hata hivyo, katika uchaguzi mdogo, baadhi ya vifaa vilivyotumika ni vile vya uchaguzi mkuu hivyo kuacha maswali kuhusu gharama zake na Jimbo la Korogwe Vijijini halikufanya uchaguzi baada ya mgombea wa CCM, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa.

Bajeti majimbo matatu

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha za Serikali inaonyesha kati ya zaidi ya Sh12.44 bilioni zilizotolewa, Sh3.7 bilioni zilikuwa kwa ajili ya posho maalumu na Sh2.08 bilioni zilikuwa za kujikimu (perdiem) kwa siku 30 za watumishi wa NEC kusimamia uchaguzi huo.

Kwa kuwa uchaguzi huo uliwapa majukumu ya ziada, Sh1.24 bilioni zilitengwa kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa Tume pamoja na Sh917.16 milioni za kufanikisha usafiri wao wakiwa kwenye majimbo na Sh626.21 milioni kwa ajili ya chakula na viburudisho.

Tume ilipaswa kutumia Sh1.22 bilioni kuchapisha na kudurufu nyaraka muhimu kwa ajili ya uchaguzi huo huku Sh105.91 milioni zikitengwa kuwalipa vibarua wakati wajumbe wakitakiwa kulipwa Sh228.41 milioni kwa kuhudhuria vikao.

Sh306.35 milioni zilitumika kwa ajili ya malazi na Sh291.7 milioni kwa ajili ya kukodi magari binafsi. Dizeli Sh548.866 milioni ilinunuliwa na Sh32.4 milioni zikinunua vocha kwa ajili ya mawasiliano ya simu.

Kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, tume ilikodi maturubai na vifaa vya kupigia kambi kwa Sh258.27 milioni huku ikitumia Sh24.19 milioni kuwasafirisha watendaji wake kwa ndege.

Fedha nyingine zilitumika kwa ukarimu (Sh16.45 milioni), vifaa vya ofisi (Sh117.05 milioni), kompyuta na vifaa vyake (Sh72.84 milioni), matangazo (Sh145 milioni), huduma za mzabuni (Sh311.31 milioni) na mikutano ikigharimu Sh177.8 milioni.

Maoni

Ingawa demokrasia ni gharama, Mbunge wa Momba, David Silinde alisema kutenga kiasi kikubwa hivyo ni ufujaji wa fedha za umma.

Alipendekeza kufutwa kwa uchaguzi wa marudio endapo mbunge atahama chama au kufariki basi chama kilichoshinda kijaze nafasi iliyo wazi.

Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi ambaye alihama Chadema na kujiunga CCM alisema “ndiyo gharama za demokrasia. Ndiyo namna pekee iliyopo kwamba mbunge akijiuzulu uchaguzi unaitishwa, hakuna jinsi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Paul Luisulie alisema, “cha msingi vyombo vilivyopewa jukumu la kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma vifuatilie.”

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Bubelwa Kaiza alisema katika utekelezaji wa demokrasia, siyo fedha peke yake zinazoangaliwa bali masilahi ya wananchi.
 
much know

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Messages
2,644
Points
2,000

much know

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2017
2,644 2,000
Wafadhili kateni misaada na mikopo na hizo fedha hudimieni masikini walioko katika nchi zenu au nchi zingine zinazohitaji misaada na sio kusaidia watu wasiojitambua na waliojaa ubinafsi.

Tukiumia ndio tutapata akili ya kukataa watawala wabovu.
Tukiwa na njaa hatutaweza kuwakabiri watawara wabovu zaidi ndo watatutawala vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
69,506
Points
2,000

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
69,506 2,000
Dar es Salaam. Serikali iliidhinisha takriban asilimia tano ya bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, kurudia uchaguzi katika majimbo matatu mwaka jana.

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/19, inaonyesha kuwa Hazina ilibadili matumizi ya zaidi ya Sh12.4 bilioni kufanikisha uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga, Monduli na Korogwe Vijijini uliofanyika Septemba mwaka jana. Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja alithibitisha kuhamishwa kwa fedha hizo, “Ni kweli fedha hizo zimehamishwa kama inavyoonekana lakini hilo ni jambo moja kujua kama zimetumika zote au sehemu tu. Ni suala ambalo (NEC) Tume ya Taifa Uchaguzi wanayo maelezo sahihi.”

Mwaipaja alifafanua kuwa Serikali hutoa fedha kulingana na mahitaji ya mhusika ambaye baadaye hutakiwa kuthibitisha matumizi yake kwa kuzingatia mchanganuo alioutoa.

Alipoulizwa jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage alishauri atafutwe Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa maelezo kuwa ndiye mwenye taarifa husika.

Alipotafutwa, mkurugenzi huyo Dk Athumani Kihamia alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.

“Nipo kwenye mkutano, nitumie meseji,” alisema Dk Kihamia. Lakini alipotumiwa ujumbe, hakujibu.

Baadaye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James alisema NEC hutengewa bajeti mahsusi kila inapotokea sababu ya msingi.

“Ni waziri wa fedha pekee mwenye mamlaka ya kuhamisha fedha kutoka fungu moja kwenda jingine. Anachokifanya ni kutoa fedha kulingana na maombi yaliyowasilishwa. Tume ya Uchaguzi walifanya hivyo, wakamshawishi waziri kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kwa wastani, bajeti hiyo ni zaidi ya Sh4.1 bilioni kwa kila jimbo, ikilinganishwa na Sh991 milioni zilizotumika kwa kila jimbo mwaka 2015 katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dotto alisema mahitaji ya majimbo hayalingani kwa kuwa hutofautiana ukubwa wa eneo, idadi ya kata pamoja na wapigakura.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Serikali ilitoa zaidi ya Sh270 bilioni kufanikisha uchaguzi kwenye majimbo 264 ambazo NEC ilitumia Sh261.6 bilioni.

Hata hivyo, katika uchaguzi mdogo, baadhi ya vifaa vilivyotumika ni vile vya uchaguzi mkuu hivyo kuacha maswali kuhusu gharama zake na Jimbo la Korogwe Vijijini halikufanya uchaguzi baada ya mgombea wa CCM, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa.

Bajeti majimbo matatu

Taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya fedha za Serikali inaonyesha kati ya zaidi ya Sh12.44 bilioni zilizotolewa, Sh3.7 bilioni zilikuwa kwa ajili ya posho maalumu na Sh2.08 bilioni zilikuwa za kujikimu (perdiem) kwa siku 30 za watumishi wa NEC kusimamia uchaguzi huo.

Kwa kuwa uchaguzi huo uliwapa majukumu ya ziada, Sh1.24 bilioni zilitengwa kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa Tume pamoja na Sh917.16 milioni za kufanikisha usafiri wao wakiwa kwenye majimbo na Sh626.21 milioni kwa ajili ya chakula na viburudisho.

Tume ilipaswa kutumia Sh1.22 bilioni kuchapisha na kudurufu nyaraka muhimu kwa ajili ya uchaguzi huo huku Sh105.91 milioni zikitengwa kuwalipa vibarua wakati wajumbe wakitakiwa kulipwa Sh228.41 milioni kwa kuhudhuria vikao.

Sh306.35 milioni zilitumika kwa ajili ya malazi na Sh291.7 milioni kwa ajili ya kukodi magari binafsi. Dizeli Sh548.866 milioni ilinunuliwa na Sh32.4 milioni zikinunua vocha kwa ajili ya mawasiliano ya simu.

Kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, tume ilikodi maturubai na vifaa vya kupigia kambi kwa Sh258.27 milioni huku ikitumia Sh24.19 milioni kuwasafirisha watendaji wake kwa ndege.

Fedha nyingine zilitumika kwa ukarimu (Sh16.45 milioni), vifaa vya ofisi (Sh117.05 milioni), kompyuta na vifaa vyake (Sh72.84 milioni), matangazo (Sh145 milioni), huduma za mzabuni (Sh311.31 milioni) na mikutano ikigharimu Sh177.8 milioni.

Maoni

Ingawa demokrasia ni gharama, Mbunge wa Momba, David Silinde alisema kutenga kiasi kikubwa hivyo ni ufujaji wa fedha za umma.

Alipendekeza kufutwa kwa uchaguzi wa marudio endapo mbunge atahama chama au kufariki basi chama kilichoshinda kijaze nafasi iliyo wazi.

Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi ambaye alihama Chadema na kujiunga CCM alisema “ndiyo gharama za demokrasia. Ndiyo namna pekee iliyopo kwamba mbunge akijiuzulu uchaguzi unaitishwa, hakuna jinsi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Paul Luisulie alisema, “cha msingi vyombo vilivyopewa jukumu la kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma vifuatilie.”

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Bubelwa Kaiza alisema katika utekelezaji wa demokrasia, siyo fedha peke yake zinazoangaliwa bali masilahi ya wananchi.
Hayo "mapya" yaliyoibuka ni yepi?
 
Mromboo

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
1,746
Points
2,000

Mromboo

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
1,746 2,000
Umeelewa kinachozungumziwa hapo lakini?
Mkuu unabishana na huyo mwehu ambaye hata tofauti ya herufi kubwa na ndogo hajui? Yaani yeye anacomment tu kile kilichomjia kichwani. Hajui hata hiyo taarifa iko gazeti la leo la Mwananchi. Yaani ni shida sana.
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,860
Points
2,000

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,860 2,000
chadema mzidi kisusia kama kawaida yenu kutia mpira kwapani
Unajiaibisha na kuwaaibisha unaodhani unawatetea kumbe unawachafua! Huwa najiuliza sana umahiri wako wa kuropoka bila kuwaza na kutafakari madhara ya mropoko wako kwa pande zote uanakuchoraje kwa jamii inayokujua? Huisaidii ccm bali wewe ni mnafiki ambaye umejiapiza kuizika mazima kwa kujifanya unaitetea!
Hebu onyesha uhusika wa cdm kwenye hizo tuhuma za ubadhirifu! Mmekwapua na sasa mnaweweseka limevujaje ilihali mlifungia kila kitu! Jiandaeni kuanikwa zaidi!
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,860
Points
2,000

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,860 2,000
sasa ya uchaguzi yanawahusu nn wakati mlikimbia match
Mpuuzi wa kweli na siyo unajitoa ufahamu bali ndivyo ulivyo kiuhalisia! Unajadili kitu tofauti na ni kwasababu umevurugwa kwa kuambiwa acha au hutolipwa tena kwani ujinga wako haununuliki na unakitia chama cha mapinduzi hasara!
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
4,336
Points
2,000

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
4,336 2,000
chadema mzidi kisusia kama kawaida yenu kutia mpira kwapani
Wewe ni ZUZU na SHENX Type...!!Watu wanajadili UFUJAJI WA FEDHA ZA WALIPA KODI wewe unawalaumu CHADEMA...?Kweli nchi hii kuna vichaa na mabazazi wa kutupwa.Ule utafiti ulio baini kwamba katika KILA WATZ 4 kuna 1 ni KICHAA kabisa..ulikuw asahihi!!!
Na hii sehemu ya 1 katika 4 au 25% ya vichaa iko kwa NZI WA KIJANI wanaopatikana mitaa ya Lumumba......ni hatari sana kwa kweri!...
 
Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
5,261
Points
2,000

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
5,261 2,000
I agree, demokrasia ina gharama zake.....

Hata hivyo, haya matumizi yaliyorekodiwa hapa ni ufisadi ulio wazi kabisa kwa jina la "demokrasia ni gharama"....

Hebu cheki hii, eti TShs 629,000,000 zimetumika kwa ajili ya CHAKULA na VIBURUDISHO na VIRUTUBISHO...sijui walikuwa wanarutubisha nini kwenye uchaguzi...

maswali ni haya:

1. Kina nani walikuwa wanakula chakula hiki?

2. Aina gani ya chakula?

3. Kina nani walikuwa "wanaburudishwa" na "kurutubishwa"? Walikuwa wanarutubisha nini? Mbegu za kiume na za kike??

4. Ikumbukwe kuwa kuna posho za kujikimu kwa kila aliyeshiriki zoezi hili. Hivi, unapopewa posho ya kujikimu si ndiyo gharama zako za malazi, chakula, kujiburudisha nk zinakuwa ndani? Iweje kuwe na fungu separate tena la chakula, VIBURUDISHO na virutubisho na wakati huo huo kuna posho???

4. Hivi tukisema, serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli Pombe ndiyo imefungulia bomba la ufisadi tunakuwa tunakosea wapi???

5. Je, huu si ndiyo ushahidi usio hata na chembe ya shaka?

6. Iweje majimbo matatu tu yatafune billion 270 wakati majimbo 265 yalitumia kiasi pungufu ya hicho?

7. Serikali inapata wapi uhalali wa kuwachangisha wananchi elfu 10 ama 20 ama 50 eti kumchangia ujenzi wa madarasa ama zahanati wakati kuna kikundi kidogo cha watu kinafuja fedha na kodi zetu kiasi hiki???

HAPANA, HILI HALIKUBALIKI. tusidanganyane, tukatae hili. TUSEME wote ENOUGH is ENOUGH!!!
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,860
Points
2,000

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,860 2,000
unajiabisha sana kijana.hao unaowatete wanakusaidia nn maelezo mengi hakuna cha maana
Wewe umesaidikaje na upuuzi wako huu wa kuropoka hovyo mithili ya mamluki wa mungiki au intarahamwe?
Yawezekana kweli ukawa upo kukivuruga ccm maanake upo kinafiki zaidi!
 
Forum statistics

Threads 1,390,025
Members 528,081
Posts 34,041,243
Top