Mapya kifo cha dude

Mshana Nimegundua kumbe pamoja na yote hujawahi kukutana na Madon wenye majina unaowajua wewe hapa Tz,Unajua kwamba Hwa top notch ya matajiri wa Tz wengi wanalindwa na usalama wa taifa na Makomando wa kijeshi kabisa?? Hii ipo nchi nyingi sana
 
Huyo Lulu kuna uwezekano ni linage ya Mganangwa. Ambaye na yeye alikuwa mwanajeshi mpigania uhuru wa Zimbabwe hivyo ana influence kubwa sana jeshini na ndo maana aliweza kumuondoa Mugabe.

Huyo Lulu historia yake imefichwa sana na hakuna habari zake ambazo ziko wazi. Hata kujulikana ni baada ya huyo Chivayo kupiga naye picha. Na baada ya hapo aliyekuja kuweka wazi kuwa ni nani huyo mwanamke(Lulu), ni dada yake bonge Wicknell.

Huyo Lulu mwenyewe alitambulishwa ikulu kwa Mnagangwa na Chivayo, na katika kumtambulisha kuwa ni mchumba wake, alisema kwamba huyo mwanamke ni kizazi cha Mnagangwa, alitumia neno β€œlinage”

Huyo Lulu alikuwa mtu wa low profile na rekodi zake za nyuma zimefichwa sana, naamini huyo wana udugu na rais Mnagangwa. Na kuna uwezekano yeye mwenyewe alikuwa ofisa kipenyo.

Kwahiyo kupewa ulinzi wa aina hiyo unaonyesha connection iliyopo kati ya hao watu. Na ndiyo maana Mnagangwa amemlinda sana Chivayo na kumpa ma deal mengi ya mikataba ya serikali.

Pia jamaa amekuwa na kesi nyingi sana ambazo nazo zimeisha kwasababu ya Mnagangwa. Mwisho wa siku majaji wanamkuta hana hatia. Rufaa inakatwa lakini jamaa bado anakutwa hana hatia.

Chivayo alikuwa mtu wa Mnagangwa, Ila baada ya kumuoa huyo Lulu mwaka 2024, mambo yakawa safi zaidi kwake na kesi yake iliisha mwaka huo huo 2024.

Huyo Lulu ametokea kwenye familia yenye uwezo, na hicho tu ndo kinajulikana. Zaidi ya hapo, background yake haijulikani kwenye taarifa za wazi.
 
Kwa hapa Tz Ulinzi binafsi unaruhusiwa hata wewe ukitaka unaenda Polisi unakua unalindwa , Kumbuka hata Mo Dewji walinzi wake baadhi ni polisi na wanajeshi hata Gwajima pia miongoni mwa walinzi wake ni polisi..

Kwa mujibu wa Kifungu cha 75(1) cha Police Force and Auxiliary Services Act, Cap. 322 kinampa Inspector-General of Police (IGP) mamlaka, chini ya maelekezo ya Waziri, kumuweka idadi fulani ya askari kwenye special duty baada ya mtu kuomba na IGP kuridhika kwamba ulinzi huo ni muhimu.
Hapa ni kuwa askari anayekulinda utamlipa hiyo special duty kama kawaida, na hii ni kama mtu anapata tishio la kiusalama na umuhimu wake.

Huenda Zimbawe pia sheria za nchi zinaruhusu mtu binafsi apewe ulinzi wa serikali kutokana na matishio ya kiusalama.
 
Huyo Lulu alikuwa mtu wa low profile na rekodi zake za nyuma zimefichwa sana, naamini huyo wana udugu na rais Mnagangwa. Na kuna uwezekano yeye mwenyewe alikuwa ofisa kipenyo.

Kwahiyo kupewa ulinzi wa aina hiyo unaonyesha connection iliyopo kati ya hao watu. Na ndiyo maana Mnagangwa amemlinda sana Chivayo na kumpa ma deal mengi ya mikataba ya serikali.πŸ₯ΊπŸ™‡πŸΏβ€β™‚
 
Mshana Nimegundua kumbe pamoja na yote hujawahi kukutana na Madon wenye majina unaowajua wewe hapa Tz,Unajua kwamba Hwa top notch ya matajiri wa Tz wengi wanalindwa na usalama wa taifa na Makomando wa kijeshi kabisa?? Hii ipo nchi nyingi sana
Ndugu yangu sina cycles za high profiles kuyajua tote ha yoπŸ™ŒπŸΏπŸ˜‚.. Asante kwa kunitoa tongotongoπŸ’ͺπŸΏπŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…