Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Yaani kutowawajibisha wezi wa EPA ni huruma? kama anahuruma kwanini asiwasamehe na wengine pia kama akina babu seya? JK ni msanii, ndani ya usanii huo kuna ufisadi, ushikaji, kutaka kupendwa na kila mtu, kuchukulia kila jambo ni kama mzaha, vyote hivyo naviweka ndani ya usanii.

Hakuna upole wala huruma hapo. Sheria ni sheria haina cha mkubwa wala mdogo, tusijifanye hatujui kwanini aliwasamehe wezi wa EPA, au hakuchukua hatua dhidi ya Ufisadi wa rada, Richmond n.k maana huwezi kumuepusha JK na kashifa hizi.

Labda niseme hayo yote yanasababishwa na udhaifu mmoja mkubwa sana, JK ni mtu wa hila, hulka yake ni kupata jambo fulani kwa njia yeyote hata kama ni kwa hila. sasa watu kama akina RA ambao ni ma king maker huwa wanatumia nafasi hiyo kuifanikisha hiyo hila, ili baadaye waje kuwa na nguvu katika maamuzi, ambapo matokeo yake ndo kiongozi kama JK anakuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe.
 
Baniani mbaya, kiatu chake ni dawa!

JK atakumbukwa kwa hulka yake ya kutoa uhuru wa kila mtu kusema ama kubwabwaja atakavyo kwa kupitia kinywa chake ama vyombo vya habari ilimradi azingatie kuwa 'unapoishia uhuru wake ndio unapoanzia uhuru wa mwingine'. Na kwa sababu hiyo jamii imenufaika kwa kupata mawazo na fikra mbadala, hata km ni mwiba kwa serikali na chama tawala.

Kubuni mradi wa ujenzi wa UDOM ni credit nyingine kwake...na kuruhusu ufisadi uliotendeka wakati wa awamu ya tatu kuwekwa hadhani ni ujasiri mwingine...
 
Jamani msitafute mchawi, mkulu ndo tatizo. haiwezekani umepangwa kupiga penati halafu na ww unatoa pasi!!!. Sina haja ya kutaja mambo ambayo yy kama yy alikuwa anatakiwa kutoa kauli ya mwisho, anamwachia Pinda.

Mbaya zaidi huyo pinda akifanya maamuzi anamshushua.
 
Nchi inasonga mbele.

Watu tunatoka Dar kwa Bajaj hadi Mwanza. Tuna mabenki zaidi ya 50 sasa nchi hii. Tuna mashule mengi tu. Tuna vyuo na vyuo vikuu vingi tu. Tunafufua reli iliyofia mikononi mwa Mkapa. Watanzania wanamiliki majumba, magari ya kisasa kwelikweli. Chaguzi zinazidi kuwa huru zaidi. JMK ataacha KATIBA MPYA kabisa. Tuna vyombo vingi vya habari kuliko wakati mwingine wowote tangu uhuru. Tunaandika na kusema mengi juu ya JMK na wengine wote. Harusi na misiba sasa ni ya mamilioni.

Baadhi ya mapungufu yake ni kujenga watu wenye nguvu ndani ya chama chake kuliko chama chenyewe. Hili kwa sehemu kubwa limechangiwa na namna alivyoupata URAIS. Pungufu jingine ni kuteua watu wa kumsaidia kwa USWAHIBA, UDINI.

Jingine ni usimamizi hafifu wa KATIBA ya JMT. Zanzibar ni NCHI sasa. Pungufu jingine ni kutotumia kikamilifu na kisheria vyombo vya DOLA hasa UwT, PCCB, POLICE,..

Jingine kutoipa umuhimu MAHAKAMA kama afanyavyo kwa BUNGE. Pungufu jingine ni kuigawa mno CCM. Ndani ya CCM watu wanachukiana kwa viwango vya kutisha. Hili nalo lina mizizi yake tangu alipoanza kuusaka URAIS.

Pungufu jingine ni ile nguvu ya URAIS inapotakiwa kutumika, kuonekana, kuhitajika, kusimama kama TAASISI inakuwa tatizo.

Rais wetu pia ameelemewa mno na familia na marafiki zake. Wamekuwa WABIA wake kwenye URAIS.
 

Mkuu Pasco, hapo kwenye nyekundu ndo balaa na usitake kupata uhakika kwa kutumia njia hiyo.Nina hakika utakuwa na tetesi fulanifulani sasa u just want to prove beyond any reasonable doubt.Kwa taarifa yako (isiyokuwa na chembe ya uongo) JK aliingia madarakani kwa pesa za EPA na usijaribu kupata wazo kwamba kuna siku atakuja kuwafunga hao MAJIZI.

Picha yenyewe ilikuwa hivi, baada ya jina la JK kupitishwa kuwa mgombea wa CCM 2005 Mh.B.W.Mkapa alifuatwa na wanamtandao wakiongozwa na Rostam Aziz ili kupanga mkakati wa kupata pesa kwa ajili ya Kampeni.Mkapa akamwita Mzee Apson Mwang'onda na kumweleza afanye anavyojua ili pesa ya Kampeni ipatikane.Sababu kubwa ya kumtumia Apson aliyekuwa DG wa TISS ni kutokana na ukweli kwamba TISS wanakula pesa sana na hakuna maelezo zaidi ya kutoa taarifa tu kwamba ni kwa shughuli za Usalama na Ulinzi wa nchi. Mzee Apson akamvaa Daudi Balali aliyekuwa Governor wa BOT.

Huyo ndiye aliyewashtua kwamba kuna michuzi ya EPA, katika hatua kama hiyo Rostam hafanyi kosa hata siku moja.Hadi kufikia hatua hiyo nataka kukuhakikishia kwamba JK alikuwa anafuatilia sana suala la pesa za Kampeni kwa kuwa jamaa alikuwa na usongo na U-Presidaa kuliko tamaa ya fisi kwenye mkono wa binadamu unaoning'inia.Baada ya wizi huo na JK kuukwaa u-presidaa, Kumbuka kuwa Auditors waliokuwa BOT wakagundua mchezo, Balali akaona ishakuwa noma akawawakia kwamba hiyo haikuwa sehemu ya kazi waliyotakiwa kuifanya.

Balali akawatoa nduki, lakini tayari watu wa World Bank walishapata habari na walishajua Account zote zilizojazwa pesa chafu za EPA wakatuma taarifa ya kumtaka Presidaa apitishe haraka sheria ya biashara chafu ya pesa MONEY LAUNDERING,Presidaa alipotaka ushauri kwa Apson akaambiwa hiyo inaweza kuwa hatari kwa kuwa Presidaa hajui inaweza kuja kumgusa nani, so yawezekana ikajamgusa hata mtoto wake, kwa hiyo jamaa akaitolea nje na World Bank wakajulishwa kwamba transactions walizoona wale Auditors zinahusu masuala ya Usalama.

Rejea Statement ya Zakia Meghji akiwa Finance Minister.Wabia/Washirika wa maendeleo walipokuja juu na Serikali ikaona itapigwa chini kuhusu misaada ndo bomu likaiva.Pasco hadi kufikia hapo hiyo huruma kupita kiasi ya JK iko wapi ? Huyo ni mwizi kama wezi wengine tu Rostam, Lowasa na wengineo wengi.Hawezi kuthubutu kumtupa mwizi yeyote Selo kwa kuwa naye ni sehemu ya wizi huo na ndio wizi uliotumika kumfikisha hapo alipo.

JK alipokuwa akiwania kuteuliwa aliwatumia watu wengi sana kuwapanda migongoni mwao, leo amewapa asante ya kumwezesha kuwa hapo.Nakuhakikishia JK mwenyewe kwa upeo mdogo wa kuchambua mambo alionao hajui kama jamaa hawamsaidii, achilia mbali hao mawaziri wenyewe kutojijua kwamba si msaada wowote kwenye serikali.Hii si huruma ni Serikali ya Ki-ushikaji tu na kisanii.Pendekezo langu nadhani ingefaa kuitwa KAOLE GOVERNMENT na si THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA,kwani tangu 2005 hiyo serikali haipo.
 
Jamani jamani, Ikiwa JK aliiingia Ikulu kwa pesa za EPA (ufisadi), itakuwaje awe na mapungufu anapofanya Ufisadi.. mapungufu yake yangekuwa kama angefanya kinyume cha Ufisadi..JK anawalinda mafisadi inavyopaswa kulindwa, anawaweka watu wake wanaoweza kumlinda yeye na utawala huu iweje yawe mapungufu ili hali nyie wenyewe mlimchagua kwa sifa za kulinda Ufisadi?..Mapungufu mnayo nyie wenyewe wananchi na ndio maana mlimchagua YEYE..na he is doing what you deserve ikiwa leo hii mfano mbora kwenu kwa kiongozi ni Mkapa na Lowassa...Na ndio maana nasema mapungufu hupimwa kutokana na ujazo mnaoutaka na sifa zake. Kama JK ni robo chupa, Mkapa kafika nusu halafu Lowassa robo tatu ya Ufisadi itakuwaje mseme JK ana mapungufu kwa kutumia kipimo tofauti kabisa wakati sifa zinakwenda kwa kina Mkapa?

Sasa ikiwa yeye ana mapungufu hivi kweli hamkuona mapungufu wakati wa Mwinyi na Mkapa ambao wote wameyafanya sawa au zaidi ya JK ila kwa nyakati tofauti?. IPTL, Loliondo, Rada, City water, Meremeta, Green bank yaani kashifa juu ya kashifa toka enzi za kina Ami mpungwe na Idd Simba.. Ilikuwaje Elimu nchini imepiga mbizi baada ya Mwinyi kuingia madarakani, Mahospital yetu pamoja na kuwa mengi (quantity) lakini quality ya huduma zake zilipungua toka wakati wa Mwinyi tukavaa mitumba na ikawa sifa kubwa za Mh. Mwinyi na Ruksa - kipindupindu, Ukoma na maradhi ambayo yaliisha wekwa ktk koba la karantini yakarudi kwa kasi kubwa. Hamtaki kuzungumzia maswala ya Elimu na Afya, viwanda na miundombinu ilivyokufa kwa sababu mnazo interest zenu japokuwa kuna vitu wazi kabisa.

Makanisa wamerudishiwa mashule na Hospital mbona Aghakhan yule mdosi hakurudishiwa shule zake kama vile Mwanza sekondary, Tambaza na kadhalika. halafu tujiulize hivi kweli kurudisha zile shule ilikuwa maamuzi ya busara. Mtasema NDIO japokuwa ni ktk maamuzi kama hayo JK hana uwezo wa kuwaambia chochote akihofia kiti chake, leo taasisi za dini wanaepa kodi, tax exemption zimetupotezea mabillioni ya fedha na tuna NGOs mia kidogo zote hizi zikiepa kodi. JK aseme jamanin haifai tayari anaitwa mdini..Machinga, Chokoraa, MaChangudoa wamejaa mabarabarani kila kona ya miji yetu wakizuiwa kidogo, Vurugu nchi nzima na wanaungwa mkono na wanasiasa wetu wenyewe.

Magufuli na Mama Tibaijuka wakajaribu mangapi, na mwisho wa siku huonekana wao ndio watu wabaya sana wenye wivu na mtajaribu kila njia kuonyesha wao sii saints. Heee jamani tazameni reli ya kati, bandari, tumeua viwanda na hata kilimo na mazao yote ya biashara tukitegemea kuuza nyumba na viwanja kwa mafisadi ndio ajira kubwa leo ya Mtanzania, bado tu hamuoni tunakoelekea!.Jk anafanya exactly what he is supposed to do! kwa sababu akifanya inavyotakiwa haswa kupambana na ufisadi nchini na katika mazingira ambayo almost 50% ya wananchi wake ni unemployed, hatuzalishi kitu ila kuiba fedha za WB na Bank ya Afrika mtamchukia vibaya na pengine hataweza kumaliza miaka yake ya utawala.

Hee! wameondoka wangapi walijaribu kutetea maslahi ya wananchi na hakuna Mtanzania hata mmoja anayewakumbuka kwa mazuri. Toka Kolimba hadi huyu Mwakyembe mguu nje ndani hawapewi msaada wowote zaidi ya watu kudai atoe ushahidi laa sivyo afe huko huko India. Kuna mpiganaji gani alosifika kwa kupambana na ufisadi zaidi ya Dr.Slaa na vijana kama Zitto ambao leo hawapendwi na wameundiwa chuki kubwa. Wao sii wajinga hata kidogo wanapenda kuishi, maisha matamu jamani watafika mahala watachoka vile vile.

Madaktari wamegoma lakini hamtaki kuzungumzia fedha wanazopewa asasi zinazohusika na huduma za Afya wao wanazitumia vipi, JK anaogopa kugusia swala la CSSC na hatkuna kiongozi hata mmoja wa Upinzani anayethubutu kuzungumzia hili - Hakuna na kama yupo asimame hata mmoja kukemea mfumo wa misamaha ya Tax, Elimu na Afya nchini!.. wote hawa wana waogopa nyie wananchi kutokana na nguvu ya Udini iliyopo nchini, kinyume watapoteza unga wao. Leo mnamtuaka Mponda na Nkya wajiuzuru bila kujua wamekosa nini hasa kupitia sheria..Mapungufu tunayo sisi wananchi na kibaya zaidi sisi ni wanafiki hakuna mfano!
 

Appreciated mkuu....deep insights and thoughts

Say now you are in the committee to advice on how to get out of this mess. It is like we are in the enmeshed pile of contradictions. What are we supposed to do on our way forward stepwise???
 
Pasco hujafahamu kuwa dunia imebadilika sana! Enzi za mwalimu kutoa amri ilikuwa kawaida na raisi akisema haulizwi swali....pengine hivyo silka/hulka ndiyo imetufikisha hapa, ila napenda kusema enzi za kutoa amri katika maslahi na haki za binadamu hazina nafasi tena. Serikali za siku hizi zinaendeshwa kwa hoja, majadiliano na maridhiano. Japokuwa siungi mkono mgomo wa madaktari, sioni wapi raisi anaweza kuwalazimisha hao kuingia kazini. Maana linalohitajika hapa sio presence but ufanyaji kazi. Watu wamesema waweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni....lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Bahati mbaya wenye kuumia ni sisi ambao hosptali za umma ndo kimbilio. Kama huo ndo ushauri wako kwa mh raisi wa kuwafungulia mashtaka madaktari nadhani wewe hapo sio mshauri mzuri hata kidogo....that proposal will never work
 
Nchi inasonga mbele.

Watu tunatoka Dar kwa Bajaj hadi Mwanza. Tuna mabenki zaidi ya 50 sasa nchi hii.
Idadi ya mabenki kuwa kubwa haina maana kwamba nchi inasonga mbele. cha msingi ni kwamba mabenki hayo yanamsaidia mtanzania? ama ni mirija tu ya ku-siphon mali za mtanzania? kuna uwekezaji wa akili na wa faida na kuna ule wa hasara. wetu ni wa hasara zaidi.

Tuna mashule mengi tu. Tuna vyuo na vyuo vikuu vingi tu.

Mashule mengi? sema tuna "vituo" vingi wanapokusanyika wanafunzi. kama wamekaa chini, kama wana maabara au hawana, kama hawana waalimu au hawana, hiyo ni ishu nyingine. "shule" ni ukamilifu wa mahitaji ya shule, kitu ambacho kitaifa hakipo. tunatengeneza taifa lenye matabaka kielimu. na hata huko mashuleni na vyuoni, kuna quality education? kutoka wapi? ni usanii juu ya usanii.

Watanzania wanamiliki majumba, magari ya kisasa kwelikweli.
Hii ni maendeleo kwa wale wanaotengeneza magari hayo na kutuuzia, siyo sisi tunaoyanunua kama mazuzu, magari ya gharama kubwa ambayo hayatumiki kuinua uchumi, bali kutambiana kwa ufahari wa kijinga. yanaongeza foleni na kuchelewesha hata wale ambao wako serious na nchi hii, washindwe kutoa mchango wao vizuri. wenye akili wala hawahangaiki nayo, ila sisi tu hapa. nenda Rwanda ukaone.

Hayo uliyoita maendeleo na kupiga hatua, kwa kweli yanaingia kwenye matatizo tu ya nchi hii
 
Mode, nakuomba na hii thread ifanye sticky ili tunapoendelea kusoma yale mazuri ya JK, na mabaya pia tuyaone!.
 

Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.

Katika kumzungumzia JK, nilitoa angalizo lifuatalo "Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!." Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!
 


Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.

Kaka Pasco bado nataka kuendelea kukuheshimu, personally na michango yako hapa jukwaani, convince me please.


Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!

Aisee!
 

Fafanua pleasa, kuanzia hapo juu kwenye warning hadi hapo chini..je wewe unatofauti gani na JJ na mamlaka ya kuja hapa na kumhukumu JJ unayatoa wapi huku na wewe umefanya vilevile.
 


vision
 

right?, May be he had a good reason to but how he handled the issue... mmmhh....alitumia JAZBA.
busara haijatumika katu.
 

Mijadala ya namna hii na wabunge wa CCM tofauti iko wapi? Huu ndio upuuzi aliousema Mnyika. Eti watendaji wamemwangusha, kwani nani alimchagulia watendaji?

Wewe nafahamu kuwa una akili zote, mashaka yangu umetumwa kubadili mada hapa jamvini. Mtu unaweza kuacha wezi wachukue billions halafu unawaambia warudishe halafu mtu mwingine JUHA anasema hiyo ni huruma! Angekuwa na huruma angewahurumia wamama wanaojifungulia sakafuni huko vijijini.

Njoo na mada nyingine ya maana, hii imekaa ki-CCM (according to Ho.Mnyika MP)
 
:msela:
Tabia ya mtoto huwa inarandana na wazazi wake.

Akiwa mtukukutu ujue kuna shida katika malezi aliyopata kutoka kwa walezi au wazazi . Akiwa mvivu si ajabu anajifunza toka kwa wazazi/walezi wake.

Naamini hatuwezi kuzungumzia udhaifu wa viongozi tuliowachagua bila kuzungumzia udhaifu wetu sisi tunaowachagua.

Tunapaswa kujilaumu kwa udhaifu miongoni mwa wale tuliowachagua kuwa viongozi wetu.
 

Huyu Ndugu yangu hajui maana ya Ikulu ni mahala patakatifu. Tangu alipofundishwa kuweka maslahi binafsi mbele na kumtumia Rtzi kuchota, amepoteze dira. Amejaa mgongano wa kimaslahi, na sasa amekuwa ni dhaifu saanaa kwa nafasi hiyo. Good charisma but bad character.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…