Jamani jamani, Ikiwa JK aliiingia Ikulu kwa pesa za EPA (ufisadi), itakuwaje awe na mapungufu anapofanya Ufisadi.. mapungufu yake yangekuwa kama angefanya kinyume cha Ufisadi..JK anawalinda mafisadi inavyopaswa kulindwa, anawaweka watu wake wanaoweza kumlinda yeye na utawala huu iweje yawe mapungufu ili hali nyie wenyewe mlimchagua kwa sifa za kulinda Ufisadi?..Mapungufu mnayo nyie wenyewe wananchi na ndio maana mlimchagua YEYE..na he is doing what you deserve ikiwa leo hii mfano mbora kwenu kwa kiongozi ni Mkapa na Lowassa...Na ndio maana nasema mapungufu hupimwa kutokana na ujazo mnaoutaka na sifa zake. Kama JK ni robo chupa, Mkapa kafika nusu halafu Lowassa robo tatu ya Ufisadi itakuwaje mseme JK ana mapungufu kwa kutumia kipimo tofauti kabisa wakati sifa zinakwenda kwa kina Mkapa?
Sasa ikiwa yeye ana mapungufu hivi kweli hamkuona mapungufu wakati wa Mwinyi na Mkapa ambao wote wameyafanya sawa au zaidi ya JK ila kwa nyakati tofauti?. IPTL, Loliondo, Rada, City water, Meremeta, Green bank yaani kashifa juu ya kashifa toka enzi za kina Ami mpungwe na Idd Simba.. Ilikuwaje Elimu nchini imepiga mbizi baada ya Mwinyi kuingia madarakani, Mahospital yetu pamoja na kuwa mengi (quantity) lakini quality ya huduma zake zilipungua toka wakati wa Mwinyi tukavaa mitumba na ikawa sifa kubwa za Mh. Mwinyi na Ruksa - kipindupindu, Ukoma na maradhi ambayo yaliisha wekwa ktk koba la karantini yakarudi kwa kasi kubwa. Hamtaki kuzungumzia maswala ya Elimu na Afya, viwanda na miundombinu ilivyokufa kwa sababu mnazo interest zenu japokuwa kuna vitu wazi kabisa.
Makanisa wamerudishiwa mashule na Hospital mbona Aghakhan yule mdosi hakurudishiwa shule zake kama vile Mwanza sekondary, Tambaza na kadhalika. halafu tujiulize hivi kweli kurudisha zile shule ilikuwa maamuzi ya busara. Mtasema NDIO japokuwa ni ktk maamuzi kama hayo JK hana uwezo wa kuwaambia chochote akihofia kiti chake, leo taasisi za dini wanaepa kodi, tax exemption zimetupotezea mabillioni ya fedha na tuna NGOs mia kidogo zote hizi zikiepa kodi. JK aseme jamanin haifai tayari anaitwa mdini..Machinga, Chokoraa, MaChangudoa wamejaa mabarabarani kila kona ya miji yetu wakizuiwa kidogo, Vurugu nchi nzima na wanaungwa mkono na wanasiasa wetu wenyewe.
Magufuli na Mama Tibaijuka wakajaribu mangapi, na mwisho wa siku huonekana wao ndio watu wabaya sana wenye wivu na mtajaribu kila njia kuonyesha wao sii saints. Heee jamani tazameni reli ya kati, bandari, tumeua viwanda na hata kilimo na mazao yote ya biashara tukitegemea kuuza nyumba na viwanja kwa mafisadi ndio ajira kubwa leo ya Mtanzania, bado tu hamuoni tunakoelekea!.Jk anafanya exactly what he is supposed to do! kwa sababu akifanya inavyotakiwa haswa kupambana na ufisadi nchini na katika mazingira ambayo almost 50% ya wananchi wake ni unemployed, hatuzalishi kitu ila kuiba fedha za WB na Bank ya Afrika mtamchukia vibaya na pengine hataweza kumaliza miaka yake ya utawala.
Hee! wameondoka wangapi walijaribu kutetea maslahi ya wananchi na hakuna Mtanzania hata mmoja anayewakumbuka kwa mazuri. Toka Kolimba hadi huyu Mwakyembe mguu nje ndani hawapewi msaada wowote zaidi ya watu kudai atoe ushahidi laa sivyo afe huko huko India. Kuna mpiganaji gani alosifika kwa kupambana na ufisadi zaidi ya Dr.Slaa na vijana kama Zitto ambao leo hawapendwi na wameundiwa chuki kubwa. Wao sii wajinga hata kidogo wanapenda kuishi, maisha matamu jamani watafika mahala watachoka vile vile.
Madaktari wamegoma lakini hamtaki kuzungumzia fedha wanazopewa asasi zinazohusika na huduma za Afya wao wanazitumia vipi, JK anaogopa kugusia swala la CSSC na hatkuna kiongozi hata mmoja wa Upinzani anayethubutu kuzungumzia hili - Hakuna na kama yupo asimame hata mmoja kukemea mfumo wa misamaha ya Tax, Elimu na Afya nchini!.. wote hawa wana waogopa nyie wananchi kutokana na nguvu ya Udini iliyopo nchini, kinyume watapoteza unga wao. Leo mnamtuaka Mponda na Nkya wajiuzuru bila kujua wamekosa nini hasa kupitia sheria..Mapungufu tunayo sisi wananchi na kibaya zaidi sisi ni wanafiki hakuna mfano!