Sasa nitoe constructive criticisms.
JK ni Rais anayependa sifa, hilo ni tatizo ambalo litagharimu sana legacy yake. Hotuba yake ya kwanza kwa Bunge lake akiwa kama Rais, aliahidi mambo mengi sana ambayo kama angeyatekeleza yangeweza kumpa umaarufu mkubwa sana, lakini ilipokuja kwenye utekelezaji ilikuwa ni zero. Mfano, aliahidi kurudisha nyumba zilizouzwa na serikali ya Mkapa, hakutimiza. Aliahidi kupitia upya mikataba mipya, hakuna kilichofanyika. Aliahidi kupambana na ufisadi, lakini akawa wa kwanza kuficha uvundo wa ufisadi wa Mkapa, Chenge na wengineo wengi ambao walikuwa wamegubikwa na tuhuma za ufisadi ambazo ushahidi wake ulikuwa wazi kabisa.
Mwaka 2005 hakuuzwa na Ilani ya Chama chake, bali aliuzwa na mtandao, vyombo vya habari na ule unafiki wake kwamba yeye ni mtu wa watu. Ndio maana kila kukicha utamuona yuko kwenye misiba. A day baada ya kuchaguliwa kuwa Rais alidamkia Muhimbili, watu wakasema sasa tumepata Rais atakayejali afya za walalahoi. Sasa kama Rais anajali afya za walalahoi na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya wana tuhuma kibao, kwanini hizo tuhuma zisifuatiliwe? Halafu leo anasema hawezi kufanya mabadiliko kwa shinikizo la madaktari, sasa kama wameona kwamba viongozi wa wizara hawafai, wao wafanye nini?
Nani anafanya assessment ya utendaji kazi wa kiongozi? Ni Appointing Authority au yule anayeongozwa? Mjomba alishasema tutapima size ya kiatu after 5 yrs, so the Drs have all the rights za ku-judge utendaji kazi wa mawaziri wa wizara yao.
Nije swala la Katiba, pia JK kwa kupenda sifa na alipoona kwamba upinzani unapata umaarufu, alikurupuka na kuahidi katiba mpya. Bahati mbaya hakujua kwamba Katiba mpya inamuweka mahali pagumu zaidi maana wana CCM walikuwa hawataki mabadiliko. Matokeo yake mwanzo kwenye hotuba akawasema wapinzani na kudai kwamba atajaribu u-dictator na baadaye akaja kulamba matapishi yake kwa kuwaruhusu wapinzani wapeleke mapendekezo yao na alikubaliana nao. JK alifanya hivyo baada ya kuona wananchi wako against msimamo wa chama chake. Ndio maana nasema kwamba JK anapenda sana sifa na hiyo ni weakness mbaya sana.
Kitendo cha kupata 61% kwenye uchaguzi uliopita, lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa JK, hakutegemea ashuke kutoka 80% mpaka hapo, na hapo NEC (Tume ya Uchaguzi) ilikuwa imemsaidia sana kuchakachua na yeye anajua hilo. Kama wasingemsaidia, hata hizo 61 zisingefika. Ndipo akaunda Kamati ya Mukama kuchunguza kiini cha CCM kufanya vibaya kwenye huo uchaguzi. Ndipo ikaja Falsafa ya Vua Gamba, ambayo nayo imezidi kumuweka pabaya maana ameshindwa kuitekeleza kama wananchi walivyokuwa wakitegemea.
To conclude, ni kwamba kwa kuwa Rais wetu anapenda masifa, mara nyingi huwa ni mkurupukaji wa kuweka ahadi tamu na nzuri kusikika masikioni mwa wananchi bila kuzifanyia tathimini ya kina ili kuona kama ni ahadi ambazo zinatekelezeka au la. Matokeo yake sasa, Pinda ndo amekuwa mbebeshwa lawama halafu JK yuko kimya hasemi kitu kabisa na hasa akishapima upepo kwamba wananchi wako against. Ninamuonea huruma Pinda kwa kuwa wakati mwingine ni ngumu sana kufanya kazi na mtu ambaye anapenda credit iende kwake all the time na mabaya yote wabebeshwe wengine.