Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Wanabodi,
Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais dhaifu", weak!, asiyeweza kufanya maamuzi magumu!.

Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

Nawatakia majadiliano mema.

Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

Wasalaam

Pasco wa jf.

NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
 
aliingia kwenye urais bila vission wala mission.
Hili ni pungufu kubwa sana hata katika maisha ya mtu mmoja mmoja.

Katika ngazi ya uraisi ni balaa zaidi.

Cha kumsaidia, walio karibu naye wampe vission japo ya muda huu mchache uliobaki.
Bora achegue hata sekta moja aiendeleze japo akitoka tumkumbuke kwa hilo.

Sasa hivi tutamkumbuka sikui kwa kitu gani labda safari za nje.
 
Hivi kushindwa kuwawajibisha wasaidizi wake ni huruma na upendo??

Huruma na upendo kwa nani?
Kwa maslah ya nani?

Mimi naona kama kutojiamini katika maanuzi na kujaribu kuficha uozo wa uteuzi wake wa wasaidizi wake ambao wengi ni washkaji, wengine vilaza ili wasiweze kumchaleni sana.

Baadhi ya mabosi hasa kama hajiamini hata maofisi anayependa surbodinates waliosmart kuliko yeye.
 
aliingia kwenye urais bila vission wala mission.
Hili ni pungufu kubwa sana hata katika maisha ya mtu mmoja mmoja.

Katika ngazi ya uraisi ni balaa zaidi.
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.
 
Mkuu Pasco, kubali tu kuwa mkulu hakuwa na hivyo vitu, na kama ni ilani ya uchaguzi alikili mwenyewe kuwa alikabidhiwa pale jangwani!
 
ile ilikuwa ya chama
yeye kama individual alitaka kuacha mark gani kwa watanzania?

Hata kama chama kiandae vission nzuri kiasi gani, kama individual unayesimamia utekelezaji wa mission hiyo kama wewe mwenyewe huna motivation hakuna linaloweza fanyika.

Lazima chama kiwe na vission na mtu anayeenda kukalia kiti hicho awe na vission inayosapoti vission ya chama chake.

Inaweza kuwa vission ya chama chake ni nzuri, lakini interest zake as an individual zinzkwamisha zoezi zima.
Kwa hiyo vission ya chama inakuwa haina mantiki kwa wananchi.

'conflict of interest'

halafu hii ya kusema watendaji wamemwangusha, msiwe mnasema kabisa kumtetea. Sababu mnazidi kum-expose zaidi weakness zake.

Kama hawezi kujua na kuchagua watu wa kumsaidia kazi basi hafai hata kidogo.

Hivi ukishindwa kujenga kwako na kusomesha watoto wako utamlaumu nani? Mkeo? Hausi gelo? Watoto?
What an excuse!
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.
 
kama wanataka tumsaidie
wavumilie tumpasue jipu tu bila ganzi

kuanzia mwanzo
hakuwa na inner motivation kama raisi
hata hiyo ilani ya chama sijui hata kama aliielewa
na kujaribu kuifanya ioane na ilani yake binafsi ya kugombea.

Mkuu Pasco, kubali tu kuwa mkulu hakuwa na hivyo vitu, na kama ni ilani ya uchaguzi alikili mwenyewe kuwa alikabidhiwa pale jangwani!
 
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Mbona hiyo Ilani aliyo inadi ameshindwa kuisimamia na kutekeleza yote aliyo ahidi?
 
Serikali imeshindwa kuwabana wawekezaji na kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidika na rasilimali zilizopo hapa nchini, migodi inachimbwa dhahabu statistics kwenye soko la dunia zinaonesha dhahabu toka tanzania imeuzwa kiasi kadhaa lakini sisi tumeambulia karibia na sifuri.
Pia serikali haijaonesha nia ya dhati ya kupunguza matumizi makubwa yasiyo ya lazima mfano, magari ya kifahari, misafara mikubwa wanapokwenda nje ya nchi na kufikia hotel za bei kubwa, kusafiri kwenye business class au first class kwa vigogo wa serikali. Mtoto wa mkulima alikataa gari lakini bado linatumika kwa hiyo hamna tofauti yoyote iliyoonekana katika kupunguza matumizi.
Serikali pia iwe na scale of preference, siyo tunatumia billioni kadhaa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru au kukimbiza mwenge wakati watoto wetu wanakaa chini kwa kukosa madawati na shule kibao za kata hazina vifaa.
 
Hivi kushindwa kuwawajibisha wasaidizi wake ni huruma na upendo??

Huruma na upendo kwa nani?
Kwa maslah ya nani?

Mimi naona kama kutojiamini katika maanuzi na kujaribu kuficha uozo wa uteuzi wake wa wasaidizi wake ambao wengi ni washkaji, wengine vilaza ili wasiweze kumchaleni sana.

Baadhi ya mabosi hasa kama hajiamini hata maofisi anayependa surbodinates waliosmart kuliko yeye.

Anatumia "leiza fea" leadership style and democracy hata kwa mambo ya msingi ambyo kiongozi imara na shupavu, anayejua wajibu wake hawezi kushindwa kufanya. Na pia kiongozi bora lazima ajue wajibu wake (both accountability and resposibility) kwa anaowaongoza na kutenda kwa ujasiri na uimara na pia usahihi na kusimamia maamuzi yake kwa weledi.
Sasa kwa JK hata umpigie ngoma hawezi cheza, filimbi hasikii, hata sijui yupo kwa maslahi ya nani!
 
Mr Prezida anatakiwa kuwa mkali na watendaji wazembe serikali, especially wale ambao anaweza kuwawajibisha moja kwa moja. Kama maswala ya Miundo mbinu; Reli, Bandari, , ATC haya anatakiwa ayabebee bango jino kwa jino maana naona kuna uzembe mkubwa sana ulifanyika na unaendelea kufanyika katika miundombinu.

Kwenye kilimo sasa tutoke kwenye makarabrasha na tukaendeleze kilimo kwanza kwa vitendo, aibane wizara husika isaidie kuboresha mazingira kwa wakulima , wajuu, wa kati na wachini ili wote wanufaike.

Ajira, ajitahidi kubana ajira za wageni maana wageni wanaongezeka kila leo wengine wanafanya kazi ambazo kwa kweli wenyewe tunaziweza.

Kodi, Awabane wahusika wahakikishe kila anayestahili kulipa kodi analipa. Kwa sasa ni makampuni makubwa tu ndio yanalipa lakini nayo bado yanaleta janja. Tuwabane hawa wafanya biashara wa kada zote, Ifike wakati mama ntilie, fundi cherehani, Fundi viatu, muuza chips, Fundi baskeli, nk wote wachangie pato.

Kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuiwezesha TIC iwe ni "one stop shop" ili mambo ya kodi, uhamiaji, ardhi , manispaa yafanyike hapo.

Kwenye Chama ningependa rais kama mwenyekiti awe mkali, akemee chama ndani ya chama kwakuwa sasa ndani ya CCM kuna vi chama vidogo vidogo vya kina Sitta. Kama vipi awaoneshe mlango wa kutokea waende wakaendeshe CCJ yao nje ya CCM.
 
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Is it implemented 100% without choosing what to implement and what not? Kwa mfano unapokataa hukusema una vision ya kuona maisha bora kwa kila mtanzania ina maana hukujua unalosema?
 
Amechagua wasaidizi ambao wamekuwa mzigo mkubwa kwake kwa kufikiri kidogo, kufanya kazi chini ya kiwango na kupenda kuheshimiwa kuliko hata wao kutoa heshima.
 
@capito

kwenye madini ndo balaa kabisa.
Jaribu kufuatilia kisa cha kubadili 1998 ming act to 2010 mining act, utashangaa.

Hao wasimamizi wenyewe wa hiyo Sheria ya madini hawaijui/hawaielewi kivile.
Wawekezaji wako ahead of the game, wanaijua kama sala ya asubuhi.

Wanajua mianya yote ya kufanikisha biashara zao iwe kwa uhalali au haramu.

Na sehemu inayoshangaza kabisa ni mamlaka ya waziri kusaini mkataba wa uchimbaji ambao una power ya ku-overrule mining code. It's absurd!

Hili sijui kama nimtupie lawama moja kwa moja mkuu, sababu ni suala la kitaalamu zaidi.
 
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Mkuu Pasco hii ni ile ya Nyani kushindwa kujenga nyumba anasema kwa sababu ya uvivu na kusingizia kesho.

Umeona kabisa viongozi ulio nao hawaendi na mipango yako unayotaka ni wabovu hawaendi na kaksi unayoitaka au vission na mission yako then bado unao tuu.

Ya nini kupanda kwenye meli na mzigo ambao unajua kabisa kuwa utawafanya mzame . Kwanini asiwaondoe hao vionzozi wabovu akatengeneza hata team mpya ya watendaji hata kwa kipindi kilichobaki wa kufanya kazi na kuendana na kasi yake.

Anawalea watu kama hao wa nini iwapo wameshindwa kufanya kazi na kuenda na kile anachotaka yeye
Suala hapa wala sio viongozi wabovu ila vission na mission yake haieleweki lich aya kusaidiwa na ilani ya chama chake ambayo nayo ni mzigo mwingine.

Ahadi mia na kitu wakati uwezo wa kuzitekeleza hata moja haupo.

Mikataba ya ajabu ajabu inasainiwa ya kutorosha rasilimali zetu na usimamizi wa kila kitu uko ovyo, hakuna nidhamu ya matumizi kwemnye serikali yake na kila kiongozi anasema na kufanya kile anachoona kinamtoka au kufaa kwa wakati huo hata kama atakuwa anapingana na wenzake.

Serikali imebaki jina tuu kila mtu na lwake
 
1, hasimamii kile anachokisema (kwa ufupi ni muongo)
2, ni mtu kigeugeu
3, anajifanya msikivu sana kumbe mnafiki.
4, ni mdini mkubwa.
5. hajui ni kwanini yupo ikulu na wala hajui majukumu ya mtu anayefika ikulu ni yapi. (anafikiri ikulu ni dangulo au soko la maharamia)
 
Pasco,

Kama kuna kosa Kikwete alifanya na sasa serikali yake imekua kama nyumba ya Kambale ni kukubari kuchonganishwa na rafiki yake Lowassa! Matokeo toka amejiuzulu hakuna cha maana kinachoendelea, hakuna nidhamu serikalini, kumebakia fitina, majungu na kulalamika!

Kama miaka mitatu iliyobakia anataka kubaki ktk kumbukumbu hana budi kumpa Uwaziri Mkuu mtu aina ya Magufuri na kuwatema mawaziri wake wengi wa sasa! Kufanya mabadiliko chanya kwa watendaji serikalini. Huko kuna baadhi Makatibu wakuu, Makamishina na Wakurugenzi waliovimbiwa, sasa wanacheua kwa dharau!
 
@capito

kwenye madini ndo balaa kabisa.
Jaribu kufuatilia kisa cha kubadili 1998 ming act to 2010 mining act, utashangaa.

Hao wasimamizi wenyewe wa hiyo Sheria ya madini hawaijui/hawaielewi kivile.
Wawekezaji wako ahead of the game, wanaijua kama sala ya asubuhi.

Wanajua mianya yote ya kufanikisha biashara zao iwe kwa uhalali au haramu.

Na sehemu inayoshangaza kabisa ni mamlaka ya waziri kusaini mkataba wa uchimbaji ambao una power ya ku-overrule mining code. It's absurd!

Hili sijui kama nimtupie lawama moja kwa moja mkuu, sababu ni suala la kitaalamu zaidi.
Unarudi pale pale hakuna wa kulaumu maana yeye ndiye aliyewachagua na kuwateuwa kusimamia rasilimali za taifa. Unapokuwa na team ambayo inawez akukaa hotelini na wawekezaji kwa baraka zako na wakasaini mkataba na ukafanya kazi ukiw ana mapungufu na wewe ukakaa kimya bila kuchukua hatua zozote ni balaa sana.

Kwenye madini ni uozo mtupu na wala hakuna hata wasi wasi wa kuongea hilo. Wawekezaji wanafanya kile wanachoamua maana unapompa mtu kipisi cha ardhi labda hekta 100 za kuchimba madini hapa juu wakati huko chini ya ardhi hujui anaweza kwenda umbali gani ni balaa.

Ndo hapo unapokuta mwekezaji aliye maybe Kahama ameshaenda umbali unaozidi ule aliopewa juu ya ardhi chini kwa chini wakati juu yeye juu ya ardhi hana ukubwa huo ni balaa
 
hivi kwa nini nyie mnaojulikana nani humu huwa mnaanzisha threads na kujiwahi humu kujijitetea, mnata vyeo kiaina fulani au?
 
@brialex

ni kweli kabisa
sidhani kama sheria ya madini inaongelea uchimbaji at ana angle. At the same time sidhani kama ni kitu rahisi kihivyo.

Sababu leseni ya madini haiwi in isolation, kila mwenye leseni yake anachunga leseni yake.
Am sure huu utakuwa wizi

Anyway, umenipa homework hapa!
 
Back
Top Bottom