Wimbo huu wa Taifa letu unanikwaza sana pale ninapokuwa naimba au kuusikia watu wakiiamba hasa kwenye ubeti wa kwanza pale kwenye mstari wa Pili unaosema Wabariki viongozi wake Daima huwa nawaza mengi ni hawa viongozi mafisadi wa nchi hii ndio huwa nawaombea au maana yake nikiimba ndio wabadilike huwa nafikiri naendelea kuwaombea maisha mema waendelee kutubuluza...Sijui kwanini huwa nawaza viibaya kwani nikifika kwenye sehemu hiyo huwa nakaa kimya kabisa, ebu nisaidieni maana yake kuwaombea akina nani hawa hawa wanaojiongezea Posho wapendavyo?
WIMBO WA TAIFA – (TANZANIA NATIONAL ANTHEM)
1. Mungu Ibariki Afrika, (God Bless Africa)
Wabariki Viongozi Wake, (bless her leaders)
Hekima, Umoja na Amani (wisdom, unity and peace)
Hizi ni Ngao Zetu,(these are our shields)
Afrika na Watu Wake. (Africa and her people)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Tubariki, Watoto wa Afrika,(Bless, Children of Africa)