Mapungufu katika Wimbo wa Taifa la Tanzania

Kwakweli japokua mimi ni mwanademokrasia sijapata kusikia wimbo huu wa taifa ukiimbwa halafu wanachama hawa wenzetu wakachomekea neno Chadema badala ya Tanzania kwenye ubeti huo! Kama ni kweli basi itakua ni mandumila kuwili wasio kitakia chama hiki mema, ni kweli tunaheshimu sana wimbo huu wa taifa na wala hatuna nia ya kuipotosha jamii kwa kufanya hivyo hii itakua ni sawa na kubadilisha bendera ya taifa na kupandisha bendera yenye nembo nyingine! hata mimi napiga vita kuhusiana na tabia hiyo kama ipo au imeshajitokeza. Alunta Continue!

Kama Tanzania wameichoka basi Wahamie kwenye hiyo nchi inayoitwa Chadema.
 
Acheni imani potofu,hivi cdm wakianza kuimba wanatangaza rasmi kuwa huo ndo wimbo halisi wa taifa? Au maneno ya wimbo yaka kopilaiti?mbona wasanii wanaimba na hamuonei kijicho? Watu wanalilia Tz iwe na patent na copyright ya Tanzanite,kilimanjaro,serengeti n.k wewe mnalilia kuimba,imbeni sasa ndo mpate shibe. Ningekuwa mimi ningeufuta wimbo huu haramu wa kinafiki. Mwanzoni mkapa alipata ugumu kuona watu wanavaa nguo za rangi ya jeshi na hata bendera ya taifa,baada ya kueleweshwa sasa tunaona kawaida,ni ufupi wa kufikiri tu watu wanadhani uzalendo wa kinafiki unalazimishwa! Mi siupendi wimbo huu hata kidogo,unamhusisha Mungu ktk maneno yake alaf watawala wanatupa hardlife,ni ujinga! Hata zamani ikipigwa filimbi ya kushusha bendera watu walisimama wima,nenda Tanzania au hata city center uone,uyu anashusha bendera,uyu anapiga honi,uyu anapiga milio ya pikipiki(watoto wa kiarabu na kipemba),uyu anabishana uccm vs.chadema,full vurugu. Badala ya kutuamasisha tujenge nchi,tuwatoe baru wakoloni weusi,tulete kilimo na ufugaji bora,mnakimbilia kuweka kopilaiti kwenye nyimbo,usanii na maneno ya wanyonyaji ktk wimbo wenu wa taifa! Sipendi!
 
Taifa lenyewe liko wapi?..Nchi yenyewe iko wapi?...:shock:
Mnasemea nchi hii ya Al-Adawi na Rostam?..:shock:
Mnapenda nyimbo, wakati nchi inauzwa?...you are not serious..not at all!:shock:
Mnalilia beti za nyimbo, wakati mikataba ya hovyo inasainiwa MAHOTELINI!:shock:
Mnaongelea beti, wakati Mama Salma anaondoka kutalii na ndege ya Serikali!:shock:
Mnataka mapambio, wakati wake zenu hamjawaachia sukari nyumbani!:shock:
Mnatamani rap, wakati viwanda vinakufa kwa kukosa umeme!:shock:
My godness!!:shock:
Hivi tunawaza kweli?...tunaitakia mema nchi hii?..are we serious?...my hairs!
:shock:

Najua mkimaliza wimbo mtakuja na hoja ya MWENGE!...
Hoja dhaifu tupu...viroja!

Na kuna vijana wenzenu wanaanza maandamano ya nchi nzima leo kuunga mkono HOTUBA YA KIKWETE! , na bado mnaongelea wimbo!
I better quit earlier!

Kuna mwanajamvi mmoja amenena vyema kwamba huu ni utoto, na hujui maana ua utaifa na uzalendo. Hata viongozi wa CDM hawawezi kukubaliana na wewe kamwe,, make no mistake on that! Sasa kwa kubadilisha na kuudhalilisha wimbo wa Taifa ndiyo mikataba mibovu itakwisha?n Unapoudhalilisha wimbo wa Taifa na Tanzania kwa ujumla ndiyo unapata sukari? Yaani matatizo yetu ndiyo yatufanye tuisaliti Tanzania? Huu ni usaliti na ni kosa la jinai, ni sawa na kudharau Bendera ya Taifa. Tofautisha ndugu,, huu siyo wimbo wa CCM ni wimbo wa Taifa Tanzania, na watanzania wenye uzalendo hawawezi kukubaliana na watu kama wewe. Nashauri itungwe sheria kali (kama haipo) dhidi ya watu wanaodhalilisha alama za Taifa. Najua kuna mzungu mmoja zilimkuta mbaya alipochana noti yetu (YA TANZANIA) ya shilingi 5000 hadharani. Sasa wewe hujiulizi ni kwanini?? Hujui dola wewe.
 
Acheni imani potofu,hivi cdm wakianza kuimba wanatangaza rasmi kuwa huo ndo wimbo halisi wa taifa? Au maneno ya wimbo yaka kopilaiti?mbona wasanii wanaimba na hamuonei kijicho? Watu wanalilia Tz iwe na patent na copyright ya Tanzanite,kilimanjaro,serengeti n.k wewe mnalilia kuimba,imbeni sasa ndo mpate shibe. Ningekuwa mimi ningeufuta wimbo huu haramu wa kinafiki. Mwanzoni mkapa alipata ugumu kuona watu wanavaa nguo za rangi ya jeshi na hata bendera ya taifa,baada ya kueleweshwa sasa tunaona kawaida,ni ufupi wa kufikiri tu watu wanadhani uzalendo wa kinafiki unalazimishwa! Mi siupendi wimbo huu hata kidogo,unamhusisha Mungu ktk maneno yake alaf watawala wanatupa hardlife,ni ujinga! Hata zamani ikipigwa filimbi ya kushusha bendera watu walisimama wima,nenda Tanzania au hata city center uone,uyu anashusha bendera,uyu anapiga honi,uyu anapiga milio ya pikipiki(watoto wa kiarabu na kipemba),uyu anabishana uccm vs.chadema,full vurugu. Badala ya kutuamasisha tujenge nchi,tuwatoe baru wakoloni weusi,tulete kilimo na ufugaji bora,mnakimbilia kuweka kopilaiti kwenye nyimbo,usanii na maneno ya wanyonyaji ktk wimbo wenu wa taifa! Sipendi!

Hapo penye wekundu, mkuu,, wewe Taifa lako ni lipi? Huu siyo wimbo kama ambavyo wewe unafikiria,, hii ni alama ya Taifa Tanzania. Popote duniani unatambulika hivyo kama kitambulisho cha nchi Tanzania. Kama huzijui alama za Taifa, hata kwenye google utazipata, si lazima uende shule. Kama unadharau kiasi hicho,, hebu na wewe siku moja chana noti hadharani, au bendera ya Taifa (siyo ya CCM), Chana, hapo ndipo utajua kama maharage ni mboga au kiungo cha makande. Na hapo ndipo serikali hii hii unayodhani ni dhaifu,, utajua muziki wake. Wewe unaonekana hukusoma,, la sivyo usingesema eti "kopilaiti" ukimaanisha copy right. Ya nini hata kubishana na wewe.
 
Kubadilisha maneno ya wimbo huo na kuimbwa rasmi na chama si sahihi. Sasa je ni chama kimeamua kuutumia rasmi ktk shughuli zake au ni washiriki wa maandamano ya chama wameutumia?! Halafu kumbe tuna wazalendo wa kweli ktk nchi hii? Vizuri sana wameona matumizi mabaya ya wimbo wa Taifa, kingine cha hatari walichoona ni nini???
 
Kweli Kubadili Wimbo wa taifa sio kitu cha busara, naamini wanachadema walipoimba vile waliimba kwa hisia kali sana, na ni vema kukumbushana katika swala muhimu kama hili, ili huko tuelekeapo tujenge uzalendo kwa taifa letu, na ndipo umuhimu wa Taifa kwanza Chama baadae unapokuja. Ila hili sio tatizo kubwa sana, nilikiongelewa watu watafahamu na kurudi kwenye mstari cha msingi ni kuondoa uozo wa Chama tawala, kuondoa ufisadi, Mikataba mibovu, mfumuko wa bei, matumizi mabaya ya mali za uma na mambo mengine mengi.
 
Hivi kweli bado kuna Tanzania?

Mbona akina Mwiba ndiyo wanamalizia kujitenga na Muungano?

Kikwete akija kuamka, atajikuta amekuwa Gorbachev mwingine, Rais asiye na nchi.....

Na nyie mtabaki kulilia Tanzania wakati Zanzibar haipo tena....

.......Mungu ibariki, Chadema na watu wake.........
 
Nimehudhuria mara nyingi uwanja wa taifa wakati Yanga ikicheza mechi za kimataifa. Na mara zote tena hata kupitia runinga na redia mashabiki wa Yanga Africa wamekuwa wakiweka kibwagizo hiki cha ibariki Yanga Africa waziwazi.
Ajabu ninayoiona wengi hatukushtuka hadi pale CDM walipoamua nao kukienzi (?)chama chao kupitia wimbo wa taifa. Kwa nini Yanga wanaachwa kutumia kibwagizo hicho tena mbele ya viongozi wa kiserikali na Chadema wasakamwe hapa JF? Au hii ni sawa na wale wanaopiga sana kelele wakati nabii mmoja anapoitwa Mungu na wanakaa kimya wakati mnyama fulani anapoitwa Mungu na baadhi ya wafuasi wa dini zingine.
Please Stop this double standard.
Samahani nilikuwa ninapita tu!!
 
jamani ndugu zangu wote kwa pamoja chadema na ccm na vyama vingine,nchi yetu Tanzania itabaki milele lakini h vyama vyetu hivi vitapita tuu huu ndo ukweli ila taifa liko na litaendelea kuwepo,ishu ya wimbo ya taifa kama ni kweli basi inawezekana walikengeuka kidogo na sidhani kama walifanya makusudi,msomi kama dk slaa sidhani kama anaweza akaliacha hili bila kulikemea! wimbo wa taifa ni kama SALA na ni UTAMBULISHO wetu kwahiyo sio kitu cha kuchezea zea,mahali popote hapa ulimwenguni watu watakuwa na itikadi tofauti lakini inapokuja swala la wimbo wa taifa wote husimama kwa utulivu kuonyesha heshima yao kwa wimbo wa taifa! watanzania wenzangu wa cdm nadhani mtalifanyia kazi hili swala tusije tukachekwa na mataifa mengine! mungu ibariki Tanzania
 
Nimehudhuria mara nyingi uwanja wa taifa wakati Yanga ikicheza mechi za kimataifa. Na mara zote tena hata kupitia runinga na redia mashabiki wa Yanga Africa wamekuwa wakiweka kibwagizo hiki cha ibariki Yanga Africa waziwazi.
Ajabu ninayoiona wengi hatukushtuka hadi pale CDM walipoamua nao kukienzi (?)chama chao kupitia wimbo wa taifa. Kwa nini Yanga wanaachwa kutumia kibwagizo hicho tena mbele ya viongozi wa kiserikali na Chadema wasakamwe hapa JF? Au hii ni sawa na wale wanaopiga sana kelele wakati nabii mmoja anapoitwa Mungu na wanakaa kimya wakati mnyama fulani anapoitwa Mungu na baadhi ya wafuasi wa dini zingine.
Please Stop this double standard.
Samahani nilikuwa ninapita tu!!

Wewe mwenyewe umetuambia hapa kwamba umewasikia Yanga mara nyingi wakifanya hivyo,, je uliona ni sahihi tu?Kukaa kwako kimya ina maana hukuona shida la siyo ungekemea. Mimi mwenziyo nimeliona jambo hili juzi kwenye Blog ya michuzi na sikulipenda ndiyo maana nasimama kulipinga kwa dhati. Sijawasikia hao Yanga, la sivyo ningesema. Hii inaashiria nini? Yaani uone kosa unyamaze,, halafu mwanao akifanya kosa akakemewa, uanze kusema ooh mbona yule jana alifanya,, wewe ndiye uliyemwona,, ulikuwa na nafasi ya kulikemea hilo,, wenzio hawakuona. Sasa kukaa kwako kimya hakumaanishi na wengine wakae kimya waonapo makosa kama haya.
Cha msingi, ni kujua kwamba CUF,TLP,CCM,CDM, NNCR na vingine vyote, kuna mambo yanayotufanya tuweke tofauti za kiitikadi kando,, wimbo wa Taifa ni moja ya mambo hayo na haupaswi kuchezewachezewa. Watanzani wote tunapaswa kuuheshimu na kuuenzi wimbo wa Taifa na lama zingine zitambulishazo Taifa.
 
Hapo penye wekundu, mkuu,, wewe Taifa lako ni lipi? Huu siyo wimbo kama ambavyo wewe unafikiria,, hii ni alama ya Taifa Tanzania. Popote duniani unatambulika hivyo kama kitambulisho cha nchi Tanzania. Kama huzijui alama za Taifa, hata kwenye google utazipata, si lazima uende shule. Kama unadharau kiasi hicho,, hebu na wewe siku moja chana noti hadharani, au bendera ya Taifa (siyo ya CCM), Chana, hapo ndipo utajua kama maharage ni mboga au kiungo cha makande. Na hapo ndipo serikali hii hii unayodhani ni dhaifu,, utajua muziki wake. Wewe unaonekana hukusoma,, la sivyo usingesema eti "kopilaiti" ukimaanisha copy right. Ya nini hata kubishana na wewe.

mkuu naanza na msamiati wa kwanza ktk sentensi ya 'last but one' hapo inaonekana umeiponda lugha niliyotumia alafu ukatumia lugha sanifu kwa lugha yako,ok. Ila mkuu kuchangia mada sikuhitaji PhD. After all mi natafuta PhD yenye Thesis maalumu si zile za akina dr.j.m.kikwete ,hosea,kamara,na dr.mrema!sihitaji elimu iyo. Pia mbona uwakemei akina mohamed Shosi wenye elimu ya kawaida?tena Pass kama shahada ya rais wako? Tusiende mbali mkuu elimu haielezi physical ability ni compliment ya internal human traits less biological ones. Sitaki upate tuisheni ya bure maana serikali inatulipa kwa kuwaeleza mambo kama aya wadogo zenu ktk sekta ya elimu. Turudi kwenye mada yako,ivi ukiimba Ibariki Africa,roho haikusuti kwa umaskini wa kuletewa na watawala wetu? Ivi taifa unalolitetea unalijua kweli au unafuata mkumbo? Nakuuliza maswali madogo ili toka apo tuongee kama watu wazima,kwanza,nchi ya Tanzania ilipata uhuru tarehe ipi,kutoka kwa mkoloni yupi na mwaka upi? Hapa usitoe takwimu ya Tanganyika maana ilishavunjwa zamani,hapa tuna taifa huru la dhahania Tanzania. TANU ilikuja kwa uwepo wa ASP,nieleze ishara ya ASP ya vidole,kisha ya TANU na leo ya ccm,na utoe tofauti kati ya alama ya ccm na ASP. Pia nipe alama ya vidole ya adui wako chadema na utoe tofauti kati alama iyo na ya ASP. Kama hujui ilo na misingi ya taifa ili,basi ukae kimya. Unajua watoto wa siku izi wanamezeshwa ila hawatambui,wakijielewa watahumia sana. Pili, Tanganyika kabla ya kuvunjwa ilihusika vp ktk kuikomboa zbar na kuleta mapinduzi. Tatu,sababu zipi zilifuatwa kuifuta AMNUT party kwa upande wa Zbar?all muslims party! Nne,katiba ipi ni ufunguo au nembo ya taifa,ile inayomtambua waziri kiongozi zbar au makamu marais wawili na rais wa zbar? Au tuikumbatie eti ni nembo ya taifa! Taifa gani duniani lina marais watano,yani makamu 3 na rais2?ili ni taifa au kikundi cha marais?kumbuka makamu ni rais ikitokea vingnevo kikatiba! Ebu twende sawa,weka majibu ndo twende sawa labda unaweza kurudisha imani yangu kwa hawa walio kwenye List of Shame. Ukiona magumu si mpaka ujibu yote,anza na marahisi. You can choose to 'resistance' by collaboration/passive or uprisings/active,I choose the latter to you and Ccm,until later!
 
ndani ya hekima mna kila kitu. Kupitia hekima mfalme suleman alikuwa mtawala pekee duniani mwenye maamuzi sahihi na utajiri wa kutupwa. Suala katika wimbo wetu ni kwa staili gani tunaiomba hii hekima? Pangekuwepo haki usawa na uzalendo, hekima ingefanya kazi yake. Hivyo wimbo hauna tatizo kabisa ila sie wenyewe tukiongozwa na watawala wetu
 
Mungu ibariki Afrika
Wabariki viongozi wake
Hekima, umoja na amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake
Ibariki, Afrika
Ibariki, Afrika
Tubariki, watoto wa Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na umoja
Wake kwa waume na watoto
Mungu, ibariki
Tanzania, na watu wake
Ibariki, Tanzania
Ibariki, Tanzania
Tubariki, watoto wa Tanzania

UMEONA SEHEMU YENYE NYEKUNDU TOA HIYO WEKA NENO LOLOTE ULIPENDALO.

Sikubaliani na wewe. Yawezekana kwa nyakati fulani tumechikuzwa na baadhi ya viongozi ambao pengine hawatendi haki kama ilivyotarajiwa. Lakini kumbuka siku zote hatutapata viongozi wabaya tu; kuna nyakati pia watainuka wazuri. Je, wazuri pia tusiwaombee? Kumbuka wimbo wa taifa hudumu vizazi na vizazi labda uniambie tubadili kila mwaka au kila baada ya uchaguzi. Labda ingesomeka hivi:

WABARIKI VIONGOZI WAITUMIKIAO NCHI YETU KWA MOYO MNYOFU NA UZALENDO

Nawasilisha.
 
wATANZANIANIA NI WAVIVU WA KUFIKIRIA.
HUU WIMBO TULIUKOPI KUTOKA AFRIKA YA KUSINI NA TUKAUTAFSIRI.
HUWA NACHEKA SANA ETI KUNA LIJAMAA LINASEMA ETI LENYEWE NDIO LILIUTUNGA HUO WIMBO WAKATI UNAJULIKANA KABISA ASILI YAKE

Kaka kwani South Africa walipata uhuru lini hadi unasema sisi tuli copy wimbo wao?
 
Ndugu zangu, mkitaka kujua nyimbo za Taifa zenye kuamsha uzalendo, jaribuni kutafuta na msikilize wimbo wa Taifa wa iliyokuwa USSR. Huo wimbo unasifiwa kwa kuamsha hisia za kizalendo. Yasemekana kwamba midundo ya huo wimbo ulikuwa ukiwafanya askari wa Red Army kupigana kwa kujituma dhidi ya majeshi ya Ujerumani wakati wa vita kuu ya pili. Hadi hii leo, kuna wakomunisti wa kimaficho bado wanauimba wimbo huo kwa hisia kali.

Kutokana na umahiri wa wimbo huo katika kuamsha u-patriotism, taifa jipya la Russia liliamua kufanyia mabadiliko kidogo wimbo huo lakini waliendelea kutumia maudhui yaleyale ya midundo na ala ya kimuziki ingawa maneno katiak stanza za wimbo huo zilibadilishwa.

Tanzania(Tanganyika) yatubidi tufanye utafiti wa wimbo mpya kwa Taifa letu ili tunapobadili katiba ya nchi na kukaribisha jamhuri mpya, tukio hilo liendane na uzinduliwaji wa wimbo mpya. ayo ni maoni yangu tu.
 
wATANZANIANIA NI WAVIVU WA KUFIKIRIA.
HUU WIMBO TULIUKOPI KUTOKA AFRIKA YA KUSINI NA TUKAUTAFSIRI.
HUWA NACHEKA SANA ETI KUNA LIJAMAA LINASEMA ETI LENYEWE NDIO LILIUTUNGA HUO WIMBO WAKATI UNAJULIKANA KABISA ASILI YAKE

Kaka kwani South Africa walipata uhuru lini hadi unasema sisi tuli copy wimbo wao?
 
Ubeti wa kwanza lazima uanze na Afrika kwa kuwa Tanzania ipo ndani ya Afrika(ni nchi iliyopo Afrika) .Nchi nyingine za Afrika lazima zibarikiwe kwanza na ndipo ibarikiwe Tanzania.Nchi za Afrika zisipokuwa salama(zikiwa na njaa na vita) basi na Tanzania haitakuwa salama

Hekima+ Umoja = Uzalendo,kwa kuwa hekima ya viongozi pamoja na umoja wao na watanzania utafanya kusiwe na ubinafsi ambao hupelekea ufisadi.Hekima ikizidi hutambua kuwa hii mali ni ya umma na huo ndio uzalendo wenyewe

Uhuru,hapa tunamuomba Mungu adumishe uhuru wetu,uhuru wa nchi kujiamulia mambo yake yenyewe kupitia ngazi nyingi za kata,wilaya,mkoa hadi Taifa BADALA ya kuamuliwa na watu toka mataifa mengine.Umoja ,hapa lazima tumuombe Mungu atuzidishie umoja kati ya watanzania,muungano wa Tanzania uzidi kudumu ili Tanzania ipate maendeleo

Kumbuka Mungu yupo japo serikali haina dini lakini watu wa Tanzania wana dini jiulize huo wimbo unaimbwa na nani?,unaimbwa na wanadamu(watanzania) ambao wana dini.
Pia unapofanya jambo lolote lazima umtangalize Mungu bila kujali wewe ni dini gani.

Kuhamasisha watu wafanye kazi,hii ni kazi ya viongozi ambao nao wanabarikiwa kupitia wimbo huu.

MWISHO : Hakuna haja ya kubadilisha wimbo wa Taifa ,mtoa hoja hana hoja ya msingi.Maana tukiacha craps hizi za kubadili wimbo wa taifa ziendelee basi mtatuletea craps nyingine za kubadili bendera ya taifa(ujinga)

Umekuja vizuri ila hapo kwenye crap unaonyesha ulivyo dikteta So unadhani wewe ndo una suliisho na kujua kilicho sahihi na kilicho kosa.

Hatukatai kukosoana lakini tupeane challenge kwa maneno ya kujenga haya maneno ya ajabu ajabu

Sasa sijui hiithread na hii uliyanzisha wewe ipi ni crap
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/116298-yu-wapi-mke-wa-rais-mama-salma.html
Jamani wana JF naomba kuuliza,yu wapi First Lady mama Salma Kikwete?.Siku hizi simsikii kabisa na hata jana kwenye maadhimisho ya miaka mia moja ya siku ya wanawake duniani sijamsikia.

Tatizo ni nini au ndoa imeingia mushkeri?Wenye taarifa zake naomba mtujulishe.
.
is this not among the crapest threads?
 
tuanze na wimbo wa taifa,baada ya hapo bendera.na kama ikiwezekana mipaka yetu pia.
nadhani nchi ni kubwa sana kama kwetu china
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom