Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,652
- 13,077
toeni mashairi basi ili tuchague ni upi wa kuuchagua
Sikubaliani na wewe. Yawezekana kwa nyakati fulani tumechikuzwa na baadhi ya viongozi ambao pengine hawatendi haki kama ilivyotarajiwa. Lakini kumbuka siku zote hatutapata viongozi wabaya tu; kuna nyakati pia watainuka wazuri. Je, wazuri pia tusiwaombee? Kumbuka wimbo wa taifa hudumu vizazi na vizazi labda uniambie tubadili kila mwaka au kila baada ya uchaguzi. Labda ingesomeka hivi:
WABARIKI VIONGOZI WAITUMIKIAO NCHI YETU KWA MOYO MNYOFU NA UZALENDO
Nawasilisha.
huu wimbo unaimbwa kipindi gani mkuueee vijanaaaavijanaaa, vijanaaa - vijanaaa tayarikulitumiataifa - taifa - taifakulitumikataifa - taifa - tanzania.Ngeleja anaujua huu wimbo? naye si bado kijana au?
yeah ni wimbo mzuriMie nauzimia sana ule wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote....
Umenikumbusha mbalii...Ilikua primary mwaka 1991 kuna shule nilisoma tulikua tunaimba mstarini jioni kabla hatujatawanyika.Nikahamia shule ingine ndo sikuusikia tena!eee vijanaaaavijanaaa, vijanaaa - vijanaaa tayarikulitumiataifa - taifa - taifakulitumikataifa - taifa - tanzania.Ngeleja anaujua huu wimbo? naye si bado kijana au?
Mie nauzimia sana ule wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote....
naukumbuka haswaa pale kibosho girls wakati nakimbia mchakamchaka......kuwasha mwenge kuwasha mwenge nakuuweka kilimanjarosisi tunataka kuwasha mwenge tunataka kuwasha mwengeee, na kuuweka juu ya mlima, mlima kilimanjaroo, kuwasha mwenge........wanaoukumbuka vidole ju!
mimi naupenda wimbo wa tazama ramani utaona nchi nzurii.......