SoC04 Maporomoko ya maji ya asili katika vijiji, yawe chanzo cha umeme katika Kijiji husika na vijiji jirani, ili kuongeza ufikiwaji wa umeme nchi nzima

Tanzania Tuitakayo competition threads

Story Zaukweli

New Member
May 17, 2024
4
3
Utangulizi;
Kurahisisha ufikishaji wa umeme nchi nzima na utoshelevu, ni lazma vyanzo vipya vya uzalishaji wa nishati viongezeke kutokana na mazingira husika. Kama sehemu yenye milima iliyo na maporomoko ya maji Kama njombe na milima ya upare, ambayo ina maporomoko mengi ambayo hayatumiki kuzalisha japo umeme kidogo unao tosheleza Kijiji kimoja au viliwi na zaidi, Kama watafanya utafiti huenda ukakidhi mahitaji ya mji nzima, kuzingatia Kuna sehemu zenye maporomoko ya maji zaidi ya matano.

Itapunguza gharama za kutengeza maporomoko ya maji bandia.
Ambayo hutumia fedha nyingi, hivyo kwa kutumia maporomoko ya maji ya asili yaani (natural water falls) kuta rahisisha ufikiaji wa umeme vijijini kwa gharama ndogo, pia itaongeza uhakika wa utoshelevu wa umeme nchi na gharama za umeme kuwa chini kulingana na hali za wananchi.

Ita punguza pia gharama za usafirishaji wa umeme tutoka kwenye grid ya taifa mapaka kwenye vijiji husika, gharama ambazo zingewekwa kwenye uboreshaji wa miundo mbinu ya umeme.

inbound3214614448633177615.jpg

Credit:is stock,shutterstock,images

inbound6621348461958400680.jpg

Credit; shutterstock.com, images

-haihitaji kujenga kingo kubwa kwa gharama nyingi,ni uzalishaji wa kiasi kidogo Cha umeme kitakacho kidhi mahitaji ya Kijiji au vijiji husika.

Umeme utakuwa toshelevu kwa ukuaji wa sekta zingine.
Sekta mbalimbali Kama sekta ya viwanda inayohitaji umeme mwingi na wa uhakika, vijiji vile vitakavyo bainika kuwa na vyanzo vya nishati yaani maporomoko ya maji ya kiasili havita unganishwa na grid ya taifa, na umeme huo kupelekwa kwenye vijiji vingine ambavyo havina vyanzo vya nishati yaani maporomoko ya maji, pia kuboresha sekta ya umeme wa jua ili yale maeneo yaliyo na joto jingi kwa mwaka yaweze kuwekewa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, ambao utatumika katika maeneo hayo ili tuweze kuuhifadhi umeme wa grid ya taifa kwa matumizi mengine, umeme ukiwa toshelevu utachochea ukuaji haraka wa sekta ya viwanda na uzalishaji utaongezeka Sana, kwa sababu kutachochea uingizwaji wa viwanda vikubwa vinavyotumia umeme mwingi na vyenye uzalishaji mkubwa vilevile.

Kutengenezwa kwa vituo vidogo vya umeme katika vijiji vyenye maporomoko ya maji kutachochea ongezeko la ajira katika sekta ya nishati
Vijana wengi walio na taaluma ya nishati na wasio na taaluma ya nishati watapata ajira, kuanzishwa kwa vituo hivyo kutahitajika wasimamizi wa kituo na wafanya kazi hivyo itaongeza vigo wa ajira, na ajira sisizo rasmi katika ujenzi na sisizo hitaji taaluma na walizi watahitajika hivyo utachochea ukuaji wa kipato kwa hao wananchi. Uwepo na umeme utachochea ajira binafsi au kujiajiri kwa wananchi wa maeneo hayo, Kama kufungua saluni ya kike na ya kiume, vijiwe vya kuchomelea, fotokopi na huduma za intaneti na vingine vingi.

Kujengwa kwa vituo hivyo vya umeme kwa haraka kutarahisisha ufikishwaji wa huduma muhimu na ufanyaji kazi kwa ufanisi
Kuwepo kwa umeme kutachochea ongezeko la huduma muhimu kuwafikia wananchi wa maeneo husika kwa urahisi na haraka, kama zahanati zina hitaji umeme ili magonjwa anapokuja usiku apatiwe huduma hususani wamama wajawazito. Pia itasaidia mashuleni watoto watajisomea mpaka usiku na hata watakaokua majumbani kwao watajisomea usiku pia kama mchana.

Kuwepo kwa umeme kwenye vijiji ambavyo bado havijafikiwa, kutaongeza usalama wao na usalama wa nchi hasa vijiji vilivyo mipakani mwa nchi
Kuwepo kwa umeme wakati wa usiku kutaongeza usalama kwa wanakijiji na kwa nchi kiujumla, kwa kuwa kutakua na mwanga wa taa ambao utarahisha ulinzi wa mali za wananchi na uhai wao pia.

Kuwepo kwa usalama kutafanya wananchi wa maeneo husika kuendelea na biashara zao hata wakati wa usiku, yani ule mda ambao walitakiwa kuwa wamelala watautumia kuingiza kipato hata mpaka saa nne au saa sita za usiku, hasa wauzaji wa chakula, vivyaji, saluni na maduka, hivyo itawasaidia kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa taifa pia utakuwa kwa kuwa watalipa Kodi, Kwa kuwa usalama wao upo hivyo hufanya biashara kwa Uhuru hata wakati wa usiku.

Kutaipunguzia mzigo serikali kwa kupunguza vijiji vilivyo takiwa kufikishiwa umeme.
Hivyo ita rahisisha Kama serikali ilitakiwa kutenga bateji kubwa, itatenga bajeti ya wastani kwa ajili ya kujenga vituo vingi vya uzalishaji wa umeme kupitia chanzo cha maporomoko ya maji, hata Kama chanzo ni kidogo yaani kinakadiriwa kuzalisha umeme kidogo kijengwe hivyohivyo ili ukikusanywa uweze kutosha kuhudumia Kijiji angalau kimoja, maporomoko yoyote yanayoweka kutumika yatumike ili tukamilishe zoezi la kufikishiwa umeme kila Kijiji na vijiji.

Kama Kijiji kilicho na chanzo cha nishati yaani maporomoko ya maji kina umeme, ukatwe upelekwe kwenye vijiji vingine, alafu kizalishiwe umeme wake kwa kutumia chanzo chake
Kwa kufanya hivyo kutapunguza utumiaji wa umeme kutoka katika grid ya taifa hivyo nchi itakua na akiba nyingi ya nishati kwa ajili ya kuendeleza sekta zingine. pia itapunguza idadi ya vijiji vilivyo hitajika kufikiwa na serikali, hivyo itachochea ukuaji wa uchumi wa taifa kwa ujumla yaani uchumi wa nchi na wananchi.

Hitimisho;
Kutafuta vyanzo vipya vya umeme kutafanya ukuaji wetu wa uchumi ukue kwa Kasi, na kukuza uchumi ambao ni jumuishi na ufikishwaji wa huduma sawa kwa wananchi. Hivyo serikali iwekeze nguvu katika vyanzo vingine pia Kama vyanzo vya umeme wa jua, na wa upepo na vyanzo vingine vingi.
 
punguza pia gharama za usafirishaji wa umeme tutoka kwenye grid ya taifa mapaka kwenye vijiji husika, gharama ambazo zingewekwa kwenye uboreshaji wa miundo mbinu ya umeme.
Siki zote mimi ni mdau wa 'decentralization' ya umeme wa Taifa hili. Vyanzo vya kutosha ni usalama hata kwa nchi.

Kama Kijiji kilicho na chanzo cha nishati yaani maporomoko ya maji kina umeme, ukatwe upelekwe kwenye vijiji vingine, alafu kizalishiwe umeme wake kwa kutumia chanzo chak
Mmmh hapo sio mbaya wakiendelea kuunganishwa na gridi ya taifa. Ikitokea dharula waweze kuhudumia gridi. Vijiji kumi hivi vikichangia umeme wake kwenye gridi ya taifa unaweza kukuta vikaokoa jahazi pale ambapo labda mtambo wa gridi ya taifa umezingua na hauzalishi. Sijajua kama tunazo mbinu za kuhifadhi hadi sasa au bado..

Na nikuulize kidogo mtoa mada, unaonaje huu mtindo wa vijiji/mashirika na watu binafsi kuzaliaha umeme na kuiuzia Tanesco??
 
Na nikuulize kidogo mtoa mada, unaonaje huu mtindo wa vijiji/mashirika na watu binafsi kuzaliaha umeme na kuiuzia Tanesco??
Hilo ni wazo zuri sana, ila serikali inaonekana Kama haitaki kuihusisha sekta/mashirika binafsi kuzalisha umeme inataka ku cover kila kitu yenyewe ndo tatizo
 
Back
Top Bottom