SoC04 Tanzania ya Uongozi wa Vijiji ni Barabara ya Maendeleo Madhubuti

Tanzania Tuitakayo competition threads

Economist Jay

Member
Feb 18, 2016
41
50
Ni miaka mingi sana imefika Tangu taifa letu lipate uhuru toka likiitwa Tanganyika na leo ni Tanzania baada ya kuunganisha jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika.

Kumekuwa na mipango mingi sana tangu mwaka 1964 ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa lakini bado wananchi wengi wana maisha magumu sana, ukiwa mjini na una mshahara kila mwezi huwezi kuelewa ugumu uliopo kwa wananchi wengi.

Robo tatu ya maisha yangu hadi sasa nimeishi kijijini kwetu, elimu yangu ya msingi na sekondari nimesomea kijijini kwetu, kwa uzoefu nilionao, ninafikiri kwamba ikiwa serikali ya Tanzania itakubali haya mawazo yangu, basi miaka 30 kuanzia sasa Ugumu wa maisha utakuwa umepungua kwa kasi kubwa sana.

Kwanza, tufahamu kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanaishi kijijini, nguvu kubwa kabisa ya uwekezaji katika huduma za kijamii inapaswa kuelekezwa vijijini. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa barabara za vijiji zinaboreshwa sana kufikia kiwango cha lami, zahanati ziwe na mahitaji yote yanayotakiwa na pia watumishi waajiriwe wa kutosha.

Shule zetu vijijini ziboreshwe sana, kuhakikisha kuwa ni sehemu salama kabisa ya wanafunzi na walimu kuishi.

Kule vijijini watu wengi wanategemea kilimo, masoko ya mazao yanapaswa kuwa karibu na wananchi vijijini na kuhakikisha kwamba bei za mazao zinaimarishwa kuwabeba wananchi wanaofanya biashara ya kilimo ili iwasaidie waone kuwa kilimo ni biashara.

Tuimarishe mifumo ya uongozi katika ngazi za vijiji. Wananchi wahamasishwe waone kuwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni jambo la maana kabisa na lenye maslahi mapana kwa taifa.

Kwa kiasi kikubwa Maendeleo ya vijiji vyetu yanaathiriwa na viongozi wabovu wa vijiji, mitaa na vitongoji. Kwani asilimia kubwa yao hawajui kusoma wala kuandika, hili ni tatizo kubwa sana katika kuwaongoza watu.

Serikali kuu kwa kiasi kikubwa inakuwa mbali sana na wananchi wa vijijini, waliokaribu kabisa na wananchi wa vijijini ni viongozi wa serikali za vijiji. Hii ni kutokana na mfumo wa mlolongo ulivyo kwa mwananchi wa Kijijini kuwafikia viongozi wakuu.

Kwa hiyo serikali za vijiji zikitengenezwa vizuri na kuwezeshwa zinaweza kubadilisha sura ya vijiji vyetu vya Tanzania na hatimaye tutakuwa tumefikia maendeleo. Ni muhimu kufahamu kuwa kama serikali za vijiji hazihusiki moja kwa moja katika kuratibu mipango ya maendeleo vijijini, hakuna vijiji vitakavyokuja kufanikiwa kuwa na maisha mazuri kwa wananchi kuanzia nyumba za kuishi hadi huduma za maji, umeme na barabara pamoja na afya.

Serikali za vijiji zinapaswa kuwa na ofisi nzuri ya kuheshimika, ziwe na maghara ya kuifadhi mazao ya chakula kwa ajili ya dharura vijijini.

Serikali za vijiji zinapaswa kusaidia kusomesha watoto wanaotoka katika familia duni zaidi, siyo kutegemea serikali kuu na wahisani.

Vijiji vinapaswa kuwa na account benki kwa ajili ya kufanya ukusanyaji wa fedha zitakazosaidia kukarabati na kuboresha mifumo ya maendeleo kule vijijini.

Kwa kifupi ni kwamba, nguvu kubwa kabisa kwa miaka 25 ijayo ijikite katika kuboresha vijiji vyote vya Tanzania viwe na maendeleo ya juu na kuhakikisha kuwa hakuna familia ambayo bado inaishi kwenye nyumba za makuti au nyasi.

Katika Karne hii ya 21, ni ajabu sana kuona kuwa wananchi bado wanaishi kwenye nyumba za nyasi.

Kwa miaka 25 ijayo, vijiji viboreshwe kwa sababu wananchi wengi wako huko na maisha yao bado ni duni.

Nawasilisha.
 
Kwanza, tufahamu kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanaishi kijijini, nguvu kubwa kabisa ya uwekezaji katika huduma za kijamii inapaswa kuelekezwa vijijini. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa barabara za vijiji zinaboreshwa sana kufikia kiwango cha lami, zahanati ziwe na mahitaji yote yanayotakiwa na pia watumishi waajiriwe wa kutosha.
Well miundombinu bora ni msingi

Kule vijijini watu wengi wanategemea kilimo, masoko ya mazao yanapaswa kuwa karibu na wananchi vijijini na kuhakikisha kwamba bei za mazao zinaimarishwa kuwabeba wananchi wanaofanya biashara ya kilimo ili iwasaidie waone kuwa kilimo ni biashara.
Mfumo wa nchi nzima wa ugavi na ubadilishanaji wa kibiashara wa bidhaa za nchi nzima. Isitokee tena upande mmoja kukosa bidhaa fulani wakati huo upande mwingine wanahangaika kwa kukosa zoko la hiyohiyo bidhaa.

Data na takwimu zitusaidie kukabiliana na jambo hili linaumiza sana pande zote.
Kwa hiyo serikali za vijiji zikitengenezwa vizuri na kuwezeshwa zinaweza kubadilisha sura ya vijiji vyetu vya Tanzania na hatimaye tutakuwa tumefikia maendeleo
Yas kijiji kwa kijiji, hadi kuja kufikia maendeleo ya nchi nzima. Lakini lisisubiriwe kufanyika kwa upendeleo kijiji kupewa pesa tu kizembe. La. Bali ni kuangalia kijiji kinazalisha nini halafu kukazia sasa soko na maslahi kwa hilo jambo. Win win.
 
Back
Top Bottom