Habari zenu wanaJF,
Nimefuatilia kwa muda mrefu sasa siasa za nchi yetu, nimefuatilia uwakilishi wetu (wabunge), wapinzani, wanaharakati n.k hitimisho langu ni kwamba wote hawapo kwa maslahi ya nchi na wananchi kwa ujumla wao bali maslahi binafsi.
Nasema hivi kulingana na mwenendo mzima wa matukio yanayoendelea kutukia bila hatua zozote za makusudi kuchukulia, hoja zinazojengwa zisizo na mwelekeo wowote kuleta mabadiriko bali kujitengenezea umaarufu kwa maslahi binafsi. Katika Kipindi kigumu kama hiki tulicho nacho, matatizo tuliyo nayo kama kupanda gharama za maisha, kukosa umeme, kashifa nyingi za rushwa na hivi karibuni suala la Rushwa Bungeni (David Jairo na hatua nyepesi kabisa zilizochukuliwa), bado hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa, hakuna waitwao Upinzani, Wanaharakati, wanazuoni etc. Nilitarajia wanazuoni, wapinzani, wana-asasi zisizo za kiraia, n.k kuhamasisha umma, kuonyesha njia sahihi za kudai kwa nguvu haki zao stahiki, ikiwa ni pamoja na kuandaa maandamano nchi nzima kushinikiza serikali inayoonyesha kushindwa kutatua matatizo ya wananchi kuondoka madarakani ili wenye uwezo kufanya hayo wapewe fursa.
Ni Mtanzania gani karne hii asiyeweza kuona wazi kushindwa kwa serikali ya Rais Kikwete kuwafikisha Watanzania kule walikotamani na kuota kwa takribani miaka 50 ya Tangu Uhuru wa Taifa hili bila punje y a ndoto hizo kufikiwa.....yaani taifa lenye Heshima itokanayo na kuwa na, uchumi imara, utawala bora, afya, miundombinu n.k. Badala yake ahadi hewa, zisizotekelezeka, mipango mingi isiyokuwa na tija wala mikakati, Miradi rukuki isiyo na tija wala mantiki hata kidogo.
Wawakilishi wetu Bungeni wamefanya nini, wamechukua hatua gani za makusudi kabisa katika kuhakikisha kuondoa serikali hii ambayo wananchi wamekosa imani nayoi? ni kweli hakuna njia mbadala ya kuweza kutuondoa katika balaa hili (Serikali ya JK) ambalo kwa takribani Miaka 6 sasa tangu kupewa dola linatupeleka shimoni? je tunasubiri kuzikwa kabisa ndiyo watanzania tustuke? Miaka 4 iliyobaki si haba hata kidogo....kama siku moja inaweza kubadirisha sura nzima ya nchi, iweje kwa miaka 4 iliyobaki!
Watanzania tutafakari, tuchukue hatua, kuondoe serikali hii dhaifu madarakani, imeshindwa ku-deliver, imeshindwa kuwaondolea matatizo wananchi, imeendekeza starehe na safari zisizo na tija, imekosa mwelekeo, imeshindwa kupambana na rushwa, imeshindwa kupambana na madawa ya kulevya, imeshindwa kupambana na ajali zinazomaliza ndugu zetu, imeshindwa kila kitu. Hakuna sababu hata moja kuistahilisha kuendelea kushika dola hata kidogo.
Ni serikali goigoi, zembe, mbumbumbu, dhaifu, isiyoweza kufikiri, imekosa maono, imekosa utashi na Ushawishi kila mahali
Nawasilisha Hoja.
Asanteni.