Leo ni siku ya familia duniani. Hii ni taasisi ya msingi katika ujenzi wa Nchi, Uchumi na Taifa lolote duniani.
Moja ya changamoto kubwa kiuchumi inayokabili familia zetu nyingi ni changamoto ya uzazi wa mpango.Hivyo ukubwa wa familia zaidi ya uwezo wa wazazi kumudu gharama za watoto kuwapa wepesi kufanya wawe rasilimali watu yenye ubora kufikia ndoto zao na hivyo kutegemea Serikali kwa kiasi kikubwa.
Ongezeko la watu Tanzania la zaidi ya asilimia 3% kwa mwaka ni zaidi ya wastani wa kasi ongezeko la watu Bara la Afrika ambalo ni asilimia 2% na ni zaidi ya kasi ya ongezeko la watu duniani ambalo ni asilimia 1%.
Kwa sasa Tanzania ambayo ipo nafasi ya 81kwa ukubwa wa uchumi na ya 165 kwa pato la mtu mmoja duniani kati ya nchi 193, Tanzania ipo nafasi ya 20 kwa idadi ya watu duniani, na endapo tutaendelea na kasi hii, Mwaka 2050 tunapofunga utekelezaji wa Dira, tutakuwa nafasi ya 14.
Kama kazi itaendelea kwa kasi hiyo hiyo , mwaka 20100, Tanzania itakuwa nchi ya 9 kwa idadi kubwa ya watu duniani.
Tunaweza kusema China ina watu wengi lakini inakwenda kasi kiuchumi(ya pili au ya kwanza, mjadala siku nyingine),Ni ukweli kwamba, moja ya sababu ya mafanikio ya kiuchumi ya China ni pamoja na uamuzi wa kupunguza kasi ya kuzaa (one child policy mwaka 1979/1980). Leo ongezeko la watu China ni ukuaji hasi (negative growth).
Tunaweza kusema India inaongoza kwa watu duniani lakni inakua kiuchumi ( nafasi ya5) hata kuipita mkoloni wake Uingereza( nafasi ya6), lakini ukweli ni kwamba wakati kwa ukubwa wa uchumi India ni ya 5 duniani ikiwa na Dola trilioni 4.15, kwa uwiano wa uchumi kwa pato la mtu ni ya 141 duniani (kiwango cha chini cha chini ya Dola 3,000) wakati Uingereza ni 21 kwa pato la mtu ambalo ni zaidi ya dola 57000 ikiwa na kipato mara 20 ya India.
Tumepanga kuwa na Uchumi wa Dola Trilion 1 mwaka 2050, lakini mwaka 2050 Tanzania itakuwa na idadi ya watu takriban milioni 137 hivyo kuwa na wastani wa pato la mtu kwa mwaka la dola 7000.
Tukifikia ukubwa wa uchumi wa Dola Trilion1 tutakuwa nafasi ya kati ya 35-45 duniani kwa kubwa wa uchumi lakini kwa kipato cha mtu cha dola 7000 tutakuwa nafasi ya karibu 100 duniani mwaka2050.
Lakini Endapo tutaendelea kukuza uchumi kama tunavyokuza Leo kwa asilimia 6%, maana yake uchumi wetu utakuwa takriban Dola bilioni 380 mwaka 2050 na hivyo tutakuwa nafasi kati ya 65- 75 kutoka nafasi ya 81 sasa.
Na kama idadi ya watu itabaki katika ukuaji wa sasa, Hivyo kipato cha mtu kwa mwaka kwa uchumi huo kitakuwa dola 2,770 ambapo kwa wakati huo nchi itashika nafasi ya chini sana (kati ya nchi 30 za mwisho) duniani.
Ripoti ya Hali ya Umasikini na Maendeleo mwaka 2014 ilionesha kwamba, ili Tanzania ifikie Dira 2025 katika sekta ya elimu, pamoja na mambo mengine ilitakiwa kuajiri walimu 900,000 kati ya mwaka 2015 na 2025, sawa na ajira 90,000 kila mwaka.
Huu ni ushahidi wa namna changamoto ya uzazi wa mpango inatuchelewesha kasi ya maendeleo hasa katika mazingira ya uchumi wa sasa na huko tuendako ambao ubora wa watu ndio sarafu ya dunia na hivyo tunahitaji kujenga familia yenye watoto wenye Maadili, Bidii, Afya na Maarifa ili waweze kumudu ushindani wa dunia.
Kundi hili la watoto leo( umri miaka15 kushuka chini) litakuwa watu wenye umri kati ya miaka 24 na 39 tunapofunga utekelezaji wa Dira2050.
Kundi ambalo ndio nguvu kazi yenye kutegemewa hasa. Tunayo changamoto kujenga uchumi mkubwa utakao mudu kuwapa afya na maarifa bora yanayohitajika katika dunia inayokwenda kasi huku ikibadilikabadilika!. Hayawezekani kwa kodi na mikopo tu . Yanawezekana kwa kwa pamoja na PPP
HAPPY FAMILY DAY.
newsroom3602025.blogspot.com

Kafulila: Familia Ndogo, Uchumi Imara Ndiyo Njia ya Tanzania Kufikia Maendeleo
Leo ni Siku ya Familia Duniani. Familia ndiyo taasisi ya msingi katika ujenzi wa taifa, uchumi na maendeleo ya nchi yoyote duniani. Akizun...