Kuna wakati nilikuwa naatend mafunzo fulani katika moja ya vyuo vya ufundi vya kijeshi hapa nchini. Na wakati wa mapumziko nilikuwa nimekaa na wanajeshi wapatao kama 30 had 40 hivi tunapiga story. Tulikuwa kwenye vikundi vya watu watatu hadi wanne tukipiga story.
Mimi nikaingiza tu wazo la hali ya nchi inavyokwenda na kuilaumu serikali akiwemo Rais Kikwete. I expected kwamba jeshi lingekuwa kinyume na mimi or wangenishambulia. Huwezi amini, baada ya kuanzisha topic hiyo wanajeshi wote walinyamaza kimya wakanisogelea kunisikiliza, na mmojawapo akasema yafuatayo: "Sisi kama jeshi hatuwezi kufanya mapinduzi, maana tukifanya hivyo tunaweza kujikuta tumekosa support ya wananchi. Ninyi wananchi ndiye mnayechangua serikali mnayoitaka, na sisi kama wanajeshi tunasimamia maamuzi ya wananchi. Lakini ikitokea kwamba wananchi hao hao walioichagua serikali wakaamua kuikataa serikali yao, sisi kama jeshi la wananchi bado tutakuwa upande wa wananchi" mwisho wa kunukuu.
Kwa hiyo wakuu habari ndiyo hiyo. Sina uhakika kuhusu usalama wa taifa, kwa kuwa hao najua wanaingia kwenye hizo nafasi kwa upendeleo na kujuana, kwahiyo wanaweza wasiwe tayari kuwaangusha wale waliowapa hayo maulaji. But kwa upande wa jeshi, ninawahakikishieni kwamba the moment wananchi wanaamua kwa dhati, jeshi litakaa pembeni kulinda maandamano yao. Jeshi ni la wananchi na lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi.
Ninajua na ninaamini kwamba jeshi litaua kadhaa siku za kwanza kabla ya jeshi kuintervene na kuamua kulinda na kusimamia maamuzi ya wananchi. Hata kama generali Mwamunyange ni swahiba mkubwa wa Kikwete, naamini atapingwa vikali na wenzake ndani ya jeshi iwapo ataamua kuwageuka wananchi.
Kwa upande mwingine fuatilieni matokeo ya kura za uchaguzi ya mwaka jana. Kambi nyingi za jeshi zilimpa kura Slaa. Kikwete alipata kura chache sana kutoka kwa wanajeshi. Kazi kwenu kufanya maamuzi.