Mapinduzi ya Zanzibar yako hatarini.. Wazanzibari wamelala...

Kinachofanywa - na labda kwa haki - ni kuwa Wazanzibari wanaambiwa mapinduzi hayakuwa sahihi; yalikuwa ni makosa na sasa wanataka kusahihisha makosa hayo. Na wana CCM wa Zanzibar (watu wa ASP) wamekubali kuwa mapinduzi ya kumng'oa Sultani na serikali ya Shamte yalikuwa ni makosa.

Wakati umefika kwa Serikali ya Jamhuri ya Zanzibar kumuomba radhi Sultani na uzao wake na kuwaomba radhi wale wote walioathirika na mapinduzi. Hii ni pamoja na kuandaa namna ya kuwalipa wale waliopoteza ndugu zao na mali zao.
 
mwanakijiji maelezo yako huwa sahihi kwakiwango kikubwa ila nasahihisha hili la majeshi .kwani JWTZ ni pamoja na hao wazanzibar ndio likaitwa hivyo na pia wanajeshi wa upande huo wameshiriki kikamilifu kuilinda Tanzania ikiwemo vita vya uganda na pia vya msumbiji hivi vya renamo nimeona kwa macho yangu mtwara makaburi mchanganyiko yapo .sasa ni vyema uka waamsha wazanzibar na ujanja unaopita hivi sasa na masikini hawajaelewa janja iliopo ya kubadili mapinduzi kwa njia ya ujanja .sio wote wanaotaka muungano uvunjike hawa wana wa ASP wapo lakini masikini nguvu zao zimepunguzwa wamebaki wakisikitika kwa chini chini .ole wao ole wao iko siku sio mbali zanzibar inawezekana iwe hapatoshi pindi hao wana wa ASP ambao wamekuwa wana CCM wakisema sasa basi, basi utaandika mambo mengine sio hayo .tuombe Mungu marais JK na Shein nao wataamka kwa haraka kuzuiya kero hii ya hao wasiotaka muungano .mie ni mkereketwa wa hali ya juu lakini iko siku ukiona maji yanayochemshwa hayangurumi kwenye sufuria ujue hayajawiva sasa tuombe mungu yasichemke kwani itakuwa hatari .endelea kuwa elimisha lakini na wewe punguza jazba. ushauri wa bure wazanzibar wasubiri kamati ya Warioba wa ende wakaeleze yote hata kama hawataki muungano pia waeleze hebu wawe wastaarabu wasiigeuze zanzibar kuwa afghanistan
 
nyinyi wachangiaji wa bara kwa kweli zanzibar yenyewe hamuijui mnaisoma tu ya 64, zanzibar hakukuwa na mapinduzi zilikua ni fitna tu za nyerere kutaka kuufuta uislamu kama alivomuondoa idd amini. walikodiwa watu kwenda kufanya mapinduzi wakati watu walikua wametulia.

Mkuu Same ORG burudika na hii video ya 1964

http://www.youtube.com/watch?v=aHqEXc3u6So
 
nyinyi wachangiaji wa bara kwa kweli zanzibar yenyewe hamuijui mnaisoma tu ya 64, zanzibar hakukuwa na mapinduzi zilikua ni fitna tu za nyerere kutaka kuufuta uislamu kama alivomuondoa idd amini. walikodiwa watu kwenda kufanya mapinduzi wakati watu walikua wametulia.

ndiyo walikuwa wametulia wala hapakuwa na vyama vya siasa vingi kama hivi leo bali kimoja tu tena chenye kuthamini maisha ya wanzanzibari wote ,,,,,,,, chechezea uamsho weye!!!!
 
Kinachofanywa - na labda kwa haki - ni kuwa Wazanzibari wanaambiwa mapinduzi hayakuwa sahihi; yalikuwa ni makosa na sasa wanataka kusahihisha makosa hayo. Na wana CCM wa Zanzibar (watu wa ASP) wamekubali kuwa mapinduzi ya kumng'oa Sultani na serikali ya Shamte yalikuwa ni makosa.

Wakati umefika kwa Serikali ya Jamhuri ya Zanzibar kumuomba radhi Sultani na uzao wake na kuwaomba radhi wale wote walioathirika na mapinduzi. Hii ni pamoja na kuandaa namna ya kuwalipa wale waliopoteza ndugu zao na mali zao.
Mzee Mwanakijiji,
Ulipoanzisha "Let Zanzibar go!" ulianzisha mjadala kwa mbwembwe nyingi.

Sasa imekuwaje tena ?

Naona unarudi rudi na mada za usultani, vitisho na kuwatia hofu kuwa Muungano ukiondoka za Zanzibar inadidimia baharini.

Hivi Zanzibar si ilishawahi kuwa nchi huru? Ilikuwa haijiendeshi yenyewe?

Zanzibar ilikuwa mwanachama wa UN, ilikuwa mwanachawa wa bodi ya sarafu ya Afrika mashariki, Balozi za ujerumani,ufaransa na Marekani zilifunguliwa Zanzibar .Wakati huo bado Zanzibar haikuwa katika/chini ya kivuli cha Tanganyika.

Kama unaamini katika kauli mbiu ya "Let Zanzibar go!" ulitakiwa uwaunge mkono UAMSHO, CUF , CHADEMA na wazanzibari kutaka Nchi yao. Au mkuu ulikuwa unatikisa kiberiti au kufanya usanii?

Let Zanzibar go! inayoambatana na propaganda za ki-CCM za kulinda mapinduzi daima na kuwatisha wananchi kuwa watachinjana au watabaguana huku kukiwa na mkono unaochoma makanisa ni jambo linalotilisha wasi wasi sana kuwa kampeni ya Let Zanzibar go inatokana na dhati ya moyoni.

Utafanya jambo la maana ukimshauri Rais wa Muungano au Pinda kama viongozi wa juu wa Tanganyika kubariki kura ya maoni wanayoitaka Wazanzibari na UAMSHO.

Kauli ya mmoja kati ya hao kuwa hawazuii au wanabariki kura ya maoni iitishwe itamaliza haya maumivu uyapatayo mkuu.

Rais Kikwete atoe tamko/kauli kuwa Serikali ya Muungano inaunga mkono kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu Muungano huko Zanzibar.

Au Mh. Pinda asimame bungeni aseme kuwa serikali ya Muungano haina pingamizi na uitishaji wa kura ya maoni huko Zanzibar.

Katika mada zako umejaribu kuonesha njia rahisi kwa Zanzibar au wazanzibari kujitoa katika muungano lakini ulisahau kutoa kauli ya kuwataka viongozi wa Tanganyika/ bara kutoa kauli ya kuwa hawana pingamizi yoyote juu ya kura hiyo.

Umesema hapo juu katika mada yako kuwa Polisi ya Muungano na Jeshi la Muungano ndilo(-Euphemism - linalolinda mapinduzi na serikali ya Mapinduzi) linalotoa kichapo au kuua raia wanapotetea haki zao. Ni wazi kuwa hata kura itakayoitishwa Zanzibar bila kauli ya kikwete au Pinda kuashiria amani, kuwa hakutakuwa na kichapo basi ikiitishwa ni vifo tu.

Sasa Let Zanzibar go! iende sambamba na kampeni ya kutaka Rais Kikwete au Waziri Mkuu Pinda kutoa kauli ya kuwa Serikali ya Muungano(Tanganyika) inaunga mkono uitishwaji wa Kura ya maoni huko Zanzibar.

Kwa mantiki hiyo uliyoitoa kuwa nguvu za Polisi na jeshi ziko mikononi mwa Tanganyika, basi Kauli watakayoitoa itakuwa ni kinga dhidi ya utumiaji nguvu za vikosi hivyo kwa wale wanaodai kura ya maoni.

Kauli ya mmoja wapo itazima "uchomaji wa makanisa","ugaidi" wa kubambikiziwa utakwisha, itasitisha ujengaji wa chuki, itasitisha propaganda za usultani utarudi Zanzibar, mzizi wa fitina utakatika. Faida itakayopatikana ni amani ya kweli na upendo baina ya watanganyika na wazanzibari.

Tuwashajihishe Kikwete na Pinda kutoa kauli ya kuunga mkono wazanzibari waitishe kura ya maoni.
Tuwashajihishe wabunge wanaotoka Tanganyika/bara wadai kauli kutoka kwa hao wawili ili hali ya Zanzibar ipate kupatiwa dawa ya kuondosha tatizo sugu la "kuuchokonoa" muungano.

Let Zanzibar go!
 
Watakapoamka watakuja counter revolution will be complete. Watch carefully, as long as there is the union the revolution of January 12, 1964 will be defended. Outside the union the revolution will be at its weakest and THERE WILL BE a counter revolution. As long as the people of Zanzibar will not defend their own revolution which toppled the monarch and the puppet government against counter-revolution elements their own future is at stake and the gains of the revolution will be abandoned.

It is for this reason, sisi watu wa bara tumechoka kulinda mapinduzi ambayo Wazanzibari wenyewe hawataki kuyalinda; hatutaki Muungano na vyombo vya Muungano viendelee kulinda mapinduzi wakati serikali ya "Mapinduzi" ya Zanzibar ikifikiria na kutoa hata baraka za kubadili jina lake! Hatutaki polisi na JWTZ la Muungano lilinde mapinduzi ambayo halikuyafanya! Wazanzibar walibnde mapinduzi yao nje ya Muungano!!!

Let Zanzibar Go!!!

a. Serikali ya Zanzibar ilete mswada wa kupiga kura ya maoni ili wananchi wa Zanzibar waamue kutoka kwenye Muungano
b. Waweke threshold ya asilimia 80 ya Wazanzibar watakaokubali kutoka basi Zanzibar itatoka kwenye Muungano ASAP
c. Serikali ya Muungano ijiandae kuondoa vyombo vyake Zanzibar na kufanya mpango wa mpito ili nchi ya Zanzibar iweze kujitegemea na kujiendesha.

Mkuu MMJ

Hii mbona kali namna hii hawa WAGUNYA wamekukosa nini aisee ha ha ha ha
 
Kinachofanywa - na labda kwa haki - ni kuwa Wazanzibari wanaambiwa mapinduzi hayakuwa sahihi; yalikuwa ni makosa na sasa wanataka kusahihisha makosa hayo. Na wana CCM wa Zanzibar (watu wa ASP) wamekubali kuwa mapinduzi ya kumng'oa Sultani na serikali ya Shamte yalikuwa ni makosa.

Wakati umefika kwa Serikali ya Jamhuri ya Zanzibar kumuomba radhi Sultani na uzao wake na kuwaomba radhi wale wote walioathirika na mapinduzi. Hii ni pamoja na kuandaa namna ya kuwalipa wale waliopoteza ndugu zao na mali zao.
Nadhani hata huku bara rais Kikwete anaona kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa ni makosa. Kama sivyo kwa nini amekaa kimya na wakati alikula kiapo kulinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Tafakari.
 
Hakuna kitu kibaya kinachotusumbua waafrika kama kutotaka kufikiri kwa kutumia vichwa vyetu. Muungano ndio unaolinda yale mapinduzi...wenye hela na nguvu wataichukua nchi yao the moment muungano utakapoondoka. Ila kama kawaida, aliye na masikio na asikie...maana tunaona fahari kulumbana bila kuleta hoja....as if maneno yamewahi kutengeneza bomu kama la nyuklia.

mm naona kama majority ya wazenji hawapendi kuongelea kitu mapinduzi niliwahi kuishi kule zenji wakati wa siku za sherehe za mapinduzi vijana wengi huwa hawahudhurii sherehe zile wanaona bora wapate ganja zao na kwenda beach ku Chill out:hand:

niliwahi kumuuliza mjamaa flani kuhusu mapinduzi akanijibu kuwa yale Mapinduzi yalipangwa na watawala wa Tanganyika Wajerumani na waengereza wakati bado wakiwa katika Serikali ya Tanganyika baada ya uhuru 1961 na kumtumia Nyerere kufanya njama zile Nyerere na baada ya Mapinduzi wazungu wakamtumia tena Nyerere kwenda kumdanganya Karume kama wakoloni wanafanya mipango ya kwenda kumpindua ndio akamwambia bora waunganishe nchi zao ili kuweza kuilinda Zanzibar:flame: majority ya Wazanzibari hivyo ndio wanavyoamini kuhusu nchi yao:embarrassed:
 
mm naona kama majority ya wazenji hawapendi kuongelea kitu mapinduzi niliwahi kuishi kule zenji wakati wa siku za sherehe za mapinduzi vijana wengi huwa hawahudhurii sherehe zile wanaona bora wapate ganja zao na kwenda beach ku Chill out:hand:

I know kwa sababu wanafikiri maisha yalikuwa hivyo raha raha kwa watu wote kabla ya mapinduzi; wameimbiwa wimbo kuwa Zanzibar ilikuwa pepo na wao wameamini!!!
 
mwanakijiji maelezo yako huwa sahihi kwakiwango kikubwa ila nasahihisha hili la majeshi .kwani JWTZ ni pamoja na hao wazanzibar ndio likaitwa hivyo na pia wanajeshi wa upande huo wameshiriki kikamilifu kuilinda Tanzania ikiwemo vita vya uganda na pia vya msumbiji hivi vya renamo nimeona kwa macho yangu mtwara makaburi mchanganyiko yapo .sasa ni vyema uka waamsha wazanzibar na ujanja unaopita hivi sasa na masikini hawajaelewa janja iliopo ya kubadili mapinduzi kwa njia ya ujanja .sio wote wanaotaka muungano uvunjike hawa wana wa ASP wapo lakini masikini nguvu zao zimepunguzwa wamebaki wakisikitika kwa chini chini .ole wao ole wao iko siku sio mbali zanzibar inawezekana iwe hapatoshi pindi hao wana wa ASP ambao wamekuwa wana CCM wakisema sasa basi, basi utaandika mambo mengine sio hayo .tuombe Mungu marais JK na Shein nao wataamka kwa haraka kuzuiya kero hii ya hao wasiotaka muungano .mie ni mkereketwa wa hali ya juu lakini iko siku ukiona maji yanayochemshwa hayangurumi kwenye sufuria ujue hayajawiva sasa tuombe mungu yasichemke kwani itakuwa hatari .endelea kuwa elimisha lakini na wewe punguza jazba. ushauri wa bure wazanzibar wasubiri kamati ya Warioba wa ende wakaeleze yote hata kama hawataki muungano pia waeleze hebu wawe wastaarabu wasiigeuze zanzibar kuwa afghanistan

Vipi ant unatype kwa keyboard kama una maumivi ya kichwa au vipi?
ninavyowajua wana ASP asili na wana mapinduzi wengi na watoto zao wamebadilika wanataka Jamhuri ya watu wa Zanzibar irudi..kama ilivyokuwa kabla ya muungano hasa mtu kama Mzee Nassor Moyo alikuwa Judge mkuu wa mwanzo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na shahidi wa siku ya kutia saini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar!!wengine ni amani karume,Mansour himid mtoto wa mwana mapinduzi late Yussuf himid bi asha bakari mwana asili wa ASP
ukitaka majina ya wana ASP asili wengine wanataka jamhuri ya watu wa zanzibar irudi feel free to ask:hand:
 
niliwahi kumuuliza mjamaa flani kuhusu mapinduzi akanijibu kuwa yale Mapinduzi yalipangwa na watawala wa Tanganyika Wajerumani na waengereza wakati bado wakiwa katika Serikali ya Tanganyika baada ya uhuru 1961 na kumtumia Nyerere kufanya njama zile Nyerere na baada ya Mapinduzi wazungu wakamtumia tena Nyerere kwenda kumdanganya Karume kama wakoloni wanafanya mipango ya kwenda kumpindua ndio akamwambia bora waunganishe

inawezekana kabisa wapo wanaoamini hivyo; hata hivyo hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wa hili. Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea kwa sababu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar iliyojenga ulazima wa watawala kupinduliwa.
 
Vipi ant unatype kwa keyboard kama una maumivi ya kichwa au vipi?
ninavyowajua wana ASP asili na wana mapinduzi wengi na watoto zao wamebadilika wanataka Jamhuri ya watu wa Zanzibar irudi..kama ilivyokuwa kabla ya muungano hasa mtu kama Mzee Nassor Moyo alikuwa Judge mkuu wa mwanzo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na shahidi wa siku ya kutia saini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar!!wengine ni amani karume,Mansour himid mtoto wa mwana mapinduzi late Yussuf himid bi asha bakari mwana asili wa ASP
ukitaka majina ya wana ASP asili wengine wanataka jamhuri ya watu wa zanzibar irudi feel free to ask:hand:

Hili naamini ni kweli ndio maana tunataka tuwasaidia Wazanzibar watoke walinde mapinduzi yao wenyewe au wawaombe radhi wale waliopinduliwa kwa mapinduzi yaliyopangwa na Tanganyika!!
 
Vipi ant unatype kwa keyboard kama una maumivi ya kichwa au vipi?
ninavyowajua wana ASP asili na wana mapinduzi wengi na watoto zao wamebadilika wanataka Jamhuri ya watu wa Zanzibar irudi..kama ilivyokuwa kabla ya muungano hasa mtu kama Mzee Nassor Moyo alikuwa Judge mkuu wa mwanzo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na shahidi wa siku ya kutia saini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar!!wengine ni amani karume,Mansour himid mtoto wa mwana mapinduzi late Yussuf himid bi asha bakari mwana asili wa ASP
ukitaka majina ya wana ASP asili wengine wanataka jamhuri ya watu wa zanzibar irudi feel free to ask:hand:

Hebu tujuze basi na wengine? vipi na mtoto wa Natepe na yeye anataka irudi? Hivi marehemu Kanali Seif Bakari alikuwa hakuacha uzao?
 
Vipi ant unatype kwa keyboard kama una maumivi ya kichwa au vipi?
ninavyowajua wana ASP asili na wana mapinduzi wengi na watoto zao wamebadilika wanataka Jamhuri ya watu wa Zanzibar irudi..kama ilivyokuwa kabla ya muungano hasa mtu kama Mzee Nassor Moyo alikuwa Judge mkuu wa mwanzo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na shahidi wa siku ya kutia saini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar!!wengine ni amani karume,Mansour himid mtoto wa mwana mapinduzi late Yussuf himid bi asha bakari mwana asili wa ASP
ukitaka majina ya wana ASP asili wengine wanataka jamhuri ya watu wa zanzibar irudi feel free to ask:hand:
Sawa sawa, nina kaswali kadogo. Hivi Jamhuri ya watu wa Wazanzibar ikirudi baraza la mapinduzi litavunjwa?

Kaswali kanyongeza, kama kina Aman Karume, Naosoro Moyo n.k wanataka Jamhuri irudi na wamebadilika,una maana wameyakana mapinduzi? Kwanini huwa tunaona shamra shamra January 12 ikiwa kila mmoja anaamini mapinduzi hayakuwa ya Wazanzibar? Hiyo 12 Jan akina Karume, Shen, Maalim Seif huwa wanaadhimisha nini?
 
Sawa sawa, nina kaswali kadogo. Hivi Jamhuri ya watu wa Wazanzibar ikirudi baraza la mapinduzi litavunjwa?

Nguruvi, as a matter of fact naamini hoja yao ya kutaka jina la Zanzibar libadilishwe imezungukwa tu; wanachotaka ni Baraza la Mapinduzi kuvunjwa lakini bado hawajawa na ujasiri wa kusema hivyo. Itabidi tuwasaidie.
 
Lazima myalinde maana nyie ndio mliopindua! .

naam nakumbuka enzi za Mkapa, kila akija zanzibar "mapinduzi daima, mapinduzi daima na yeye" yaani huku zanzibar hatuna chengine zaidi ya kutukuziwa mapinduzi tu. Mh Kikwete naye alipata kukiri ya kuwa "mapinduzi yao" pale kibanda maiti. waZanzibari tumetosheka na fitina hizi tena ..."Tuwachiwe .... Tupumueee " potelea pote!
 
Mwanakijiji, nyerereism camp, ....mnachosha kwa chuki zenu kwa wazenj
Nyereist yeyote hawezi kupinga Muungano, kwa hili suala Unyerere ulishamshinda Mwanakijiji zamani, wakati tunapigania haki na maslahi ya Watanzania Bara miaka yote hapa JF Mwanakijiji alitupinga vikali, aliweka mbele symbolism na utukufu wa "Baba wa Taifa."

Sasa anakula matapishi yake, ameona kweli tunaopinga Muungano tuna uchungu na nchi na tuna hoja za msingi, badala ya kushinda tunaimba nyimbo za kuabudu Nyerere this, Nyerere that. I mean, hata Wamarekani wanawatukuza founding fathers wao lakini kuna mambo ya karne zile wameyakataa leo hii, you know? Founding fathers wa Marekani walikua wana own slaves, kwa hilo wamekataa kuwatukuza.

Nyerere alichemka kwa kutuunganisha na ka nchi kadogo ambako kalikataa toka mwanzo kumezwa, kwa hiyo akakafanya eti kana hadhi sawa na Tanzania Bara. Matokeo yake ndio haya, Zanzibar kila uchwao wanadai more and more autonomy halafu CCM wanatudanganya eti tunaelekea "serikali moja." Serikali moja my foot, sasa hatutaki hata serikali saba, tunataka kuvunja Muungano, period!
 
Back
Top Bottom