Kwanini joto Malalamiko ya Muungano linapanda sasa?

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
251
Reaction score
970

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, mjadala kuhusu mustakabali wa Muungano wa Tanzania umeibuka kwa nguvu ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, huku masuala ya uhuru wa kifedha, ajira kwa wazawa na upatikanaji wa huduma za kijamii yakichochea mijadala mipya kuhusu uhusiano kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.​

Ingawa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Muungano wameendelea kusisitiza manufaa ya Muungano, baadhi ya wawakilishi na wanasiasa wameibua hoja zinazogusa kile wanachokiita haki za Wazanzibari ndani ya mfumo wa sasa wa Muungano.

Zanzibar na hoja ya uhuru wa kukopa​

Mojawapo ya hoja zilizozua mjadala ni uwezo wa Zanzibar kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo yake. Mwakilishi wa ACT-Wazalendo wa Jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk, ameeleza kuwa Zanzibar imekuwa ikikumbana na changamoto ya kuhitaji idhini kutoka mamlaka za Muungano kila inapokusudia kukopa fedha kutoka nje.

Kwa mujibu wa Mbarouk, utaratibu huo wakati mwingine husababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuathiri mipango ya Serikali ya Zanzibar. Hoja yake imefungua mjadala mpana kuhusu kiwango cha uhuru wa kifedha ambacho Zanzibar inapaswa kuwa nacho ndani ya Muungano.

Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar imejibu kwa kueleza kuwa mfumo uliopo una manufaa makubwa kwa visiwa hivyo. Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akili, amesema Zanzibar inanufaika kwa kiwango kikubwa kupitia Muungano, ikiwemo kupata mikopo inayodhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Dkt. Akili, zaidi ya asilimia 50 ya mikopo ya ndani inayopatikana kwa Serikali ya Zanzibar hutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), taasisi ambayo Zanzibar ni sehemu yake kupitia Muungano. Aidha, amesema mikopo mingi ya nje inayopatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo hulipwa kupitia Serikali ya Muungano.

Kauli hiyo imeonyesha upande mwingine wa mjadala, kwamba pamoja na malalamiko ya kutaka uhuru zaidi wa kifedha, Zanzibar pia inanufaika na nguvu ya kiuchumi na hadhi ya kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma pia: Madeni ya Zanzibar yanadhaminiwa na kulipwa na Serikali ya Muungano

Akizungumzia hilo, mchambuzi wa masuala ya madeni na maendeleo kwa nchi za Afrika, Hebron Mwakagenda amesema Zanzibar haiwezi kukopa nje ya nchi kwa sababu haina utawala kamili.

“Inayokopa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo yenyewe haiwezi kukopa kwa sababu haina sovereignty. Hata kwenye alipo Zanzibar haijawahi kulipa,” amesema.

Mwakagenda aliyewahi kufanya kazi na Taasisi ya Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) amesema waliwahi kuzungumza na Serikali ya Zanzibar kuhusu madeni yao. “Walituonyesha deni lao, lakini kwa kiasi kikubwa linalipwa na Serikali ya Muungano.”

Mjadala wa matibabu waibua hisia​

Mbali na suala la mikopo, mjadala mwingine uliovuta hisia za wananchi ni kuhusu huduma za afya kati ya pande mbili za Muungano.

Soma pia: Bajeti ya Zanzibar haiwezi kutoa Matibabu kwa watu Milioni 60

Wiki iliyopita, Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa watu ambao si Wazanzibari kupitia mfumo wa bima ya afya wa Zanzibar.

Kauli hiyo ilitafsiriwa na baadhi ya watu kama ishara ya ubaguzi dhidi ya Watanzania Bara wanaoishi au kufanya kazi Zanzibar. Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar ilieleza kuwa suala hilo linahusu utaratibu wa bima ya afya na si ubaguzi wa wananchi.

Mjadala huo ulisababisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kutoa ufafanuzi kwamba mtu yeyote mwenye bima ya NHIF anaweza kupata huduma katika hospitali za Zanzibar zinazopokea bima hiyo, na vivyo hivyo kwa Wazanzibari wanaotibiwa Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwigulu, huduma za afya hazitolewi kwa kuzingatia mtu anatoka upande gani wa Muungano bali kwa kuzingatia taratibu za bima au malipo ya kawaida ya matibabu.

Kauli hiyo ililenga kuondoa hofu ya kuwepo kwa tofauti za kimatibabu kati ya wananchi wa pande mbili za Muungano.

Ajira kwa wazawa kuwa ajenda mpya​

Suala lililoibua mjadala mkubwa zaidi ni ajira kwa Wazanzibari, hususan katika sekta ya utalii ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa visiwa hivyo.

Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh, amesema takwimu zinaonyesha kuwa licha ya Zanzibar kuwa na hoteli zaidi ya 1,100 zilizosajiliwa, sehemu kubwa ya wafanyakazi katika baadhi ya hoteli hizo si wazawa wa Zanzibar.

Akitoa mfano wa hoteli moja aliyotembelea, amesema kati ya wafanyakazi 156 waliokuwapo, Wazanzibari walikuwa 27 pekee.

Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu ushiriki wa vijana wa Zanzibar katika fursa za kiuchumi zinazotokana na uwekezaji mkubwa wa utalii unaoendelea visiwani humo.

Hassan amesema Serikali imepewa jukumu la kuhakikisha vijana wa Zanzibar wanapata nafasi kubwa zaidi za ajira katika miradi inayotekelezwa visiwani humo. Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti, ambapo baadhi wanaiona kama juhudi za kulinda maslahi ya wazawa huku wengine wakihofia inaweza kutafsiriwa kama ubaguzi dhidi ya Watanzania kutoka upande mwingine wa Muungano.

Soma pia:Mbunge Mohamed Ali: Kama kuwatetea vijana wa Zanzibar kutavunja Muungano basi acha uvunjike

Je, kudai haki za Wazanzibari ni ubaguzi?​

Swali hilo limekuwa kiini cha mjadala unaoendelea Zanzibar.

Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia ACT-Wazalendo, Dkt. Nasra Nassor, amesema madai ya Wazanzibari kutaka nafasi zaidi katika ajira na masuala mengine ya kiuchumi hayapaswi kutafsiriwa kama ubaguzi.

Kwa mujibu wake, changamoto kubwa ipo katika kutokuwepo kwa muundo unaoeleweka vizuri wa Muungano unaofafanua kwa uwazi haki na wajibu wa kila upande.

Amesema vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara wanahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu haki zao ndani ya Muungano ili kuondoa migongano inayojitokeza mara kwa mara kuhusu ajira, huduma na fursa za maendeleo.

Kauli hiyo imeakisi mtazamo wa baadhi ya wanasiasa wanaoamini kuwa malalamiko mengi yanayotolewa leo yanatokana na masuala ya kimuundo ambayo hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu tangu kuundwa kwa Muungano mwaka 1964.

Serikali yakanusha madai ya ubaguzi​

Wakati mjadala huo ukiendelea, Serikali ya Zanzibar imeendelea kusisitiza kuwa hakuna sera ya ubaguzi dhidi ya wananchi wa Tanzania Bara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma, amesema wananchi wa pande zote mbili wamekuwa wakiishi, kufanya biashara na kupata huduma katika maeneo yote ya Muungano bila vikwazo.

Amesema madai kwamba Watanzania Bara hawapati huduma sawa Zanzibar ni upotoshaji usio na msingi, akisisitiza kuwa hata Wazanzibari wengi wanaishi na kufanya kazi Tanzania Bara bila changamoto.

Kwa nini chokochoko hizi wakati huu?​

Kwa wachambuzi wa siasa, mijadala inayoendelea sasa si jambo jipya. Hoja za ugawaji wa madaraka, ajira kwa wazawa, uhuru wa kifedha na nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kwa miongo kadhaa.

Kinachofanya mjadala wa sasa kuwa wa kipekee ni kwamba unaibuka wakati Zanzibar inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa sekta ya utalii, ongezeko la uwekezaji wa kigeni na matarajio makubwa ya vijana kuhusu ajira.

Katika mazingira hayo, maswali kuhusu nani ananufaika zaidi na fursa hizo yanaendelea kujitokeza. Wakati Serikali ikisisitiza kuwa Muungano una manufaa makubwa ya kiuchumi, kiusalama na kidiplomasia kwa Zanzibar, baadhi ya wananchi na viongozi wanaendelea kutaka marekebisho yatakayoongeza usawa na uwazi katika mgawanyo wa fursa.

Akitoa mtazamo wa jumla, Mwakagenda anasema malalamiko hayo yanakuja kwa kuwa Wazanzibari wameshauchoka Muungano, hivyo wanatamani kuwa nchi huru.

“Ni sawa na mke ndani ya nyumba, anaweza kuvumilia mambo madogo madogo, lakini siku akichoka, hata jambo liwe dogo kiasi gani, hatavumilia,” amesema.
 
Msipodhibiti kasi ya kuzaana, mtavunja muungano, huko Zanzibar, Pemba na Unguja zitatengana na Tanganyika itagawanyika pia.

Huwezi kuwa na nchi ya watu milioni takriban 70 yenye population growth ya around 3%, na uchumi wetu mbovu, elimu mbaya, halafu nchi iende tu bila mgawanyiko mkubwa
 
Kuna mambo inabidi yafike mwisho...
It is monitored.
Bora yajulikane, yaishe
 
"Tusiseme hatuna matatizo kwa kuyaficha matatizo yetu wenyewe. Ujasiri wa taifa hauko katika kuficha kasoro zake, bali katika kuzikubali na kuzitatua."

Mwalimu J K Nyerere.
 
Maisha yamekuwa sio, watu hawaelewi
 
Msipodhibiti kasi ya kuzaana, mtavunja muungano, huko Zanzibar, Pemba na Unguja zitatengana na Tanganyika itagawanyika pia.

Huwezi kuwa na nchi ya watu milioni takriban 70 yenye population growth ya around 3%, na uchumi wetu mbovu, elimu mbaya, halafu nchi iende tu bila mgawanyiko mkubwa
Hizi mambo inabidi zidhibitiwe kabla hazijafika mahala pabaya tatizo pale juu aliekaa sio suleiman ambae alipelekewa wanawake wawili na mtoto mmoja ili aamue kwamba yule mtoto ni yupi mama yake halisi
 
Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, mjadala kuhusu mustakabali wa Muungano wa Tanzania umeibuka kwa nguvu ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, huku masuala ya uhuru wa kifedha, ajira kwa wazawa na upatikanaji wa huduma za kijamii yakichochea mijadala mipya kuhusu uhusiano kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.​

Ingawa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Muungano wameendelea kusisitiza manufaa ya Muungano, baadhi ya wawakilishi na wanasiasa wameibua hoja zinazogusa kile wanachokiita haki za Wazanzibari ndani ya mfumo wa sasa wa Muungano.

Zanzibar na hoja ya uhuru wa kukopa​

View attachment 3611226
Mojawapo ya hoja zilizozua mjadala ni uwezo wa Zanzibar kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo yake. Mwakilishi wa ACT-Wazalendo wa Jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk, ameeleza kuwa Zanzibar imekuwa ikikumbana na changamoto ya kuhitaji idhini kutoka mamlaka za Muungano kila inapokusudia kukopa fedha kutoka nje.

Kwa mujibu wa Mbarouk, utaratibu huo wakati mwingine husababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuathiri mipango ya Serikali ya Zanzibar. Hoja yake imefungua mjadala mpana kuhusu kiwango cha uhuru wa kifedha ambacho Zanzibar inapaswa kuwa nacho ndani ya Muungano.

Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar imejibu kwa kueleza kuwa mfumo uliopo una manufaa makubwa kwa visiwa hivyo. Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akili, amesema Zanzibar inanufaika kwa kiwango kikubwa kupitia Muungano, ikiwemo kupata mikopo inayodhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Dkt. Akili, zaidi ya asilimia 50 ya mikopo ya ndani inayopatikana kwa Serikali ya Zanzibar hutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), taasisi ambayo Zanzibar ni sehemu yake kupitia Muungano. Aidha, amesema mikopo mingi ya nje inayopatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo hulipwa kupitia Serikali ya Muungano.

Kauli hiyo imeonyesha upande mwingine wa mjadala, kwamba pamoja na malalamiko ya kutaka uhuru zaidi wa kifedha, Zanzibar pia inanufaika na nguvu ya kiuchumi na hadhi ya kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma pia: Madeni ya Zanzibar yanadhaminiwa na kulipwa na Serikali ya Muungano

Akizungumzia hilo, mchambuzi wa masuala ya madeni na maendeleo kwa nchi za Afrika, Hebron Mwakagenda amesema Zanzibar haiwezi kukopa nje ya nchi kwa sababu haina utawala kamili.

“Inayokopa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo yenyewe haiwezi kukopa kwa sababu haina sovereignty. Hata kwenye alipo Zanzibar haijawahi kulipa,” amesema.

Mwakagenda aliyewahi kufanya kazi na Taasisi ya Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) amesema waliwahi kuzungumza na Serikali ya Zanzibar kuhusu madeni yao. “Walituonyesha deni lao, lakini kwa kiasi kikubwa linalipwa na Serikali ya Muungano.”

Mjadala wa matibabu waibua hisia​

Mbali na suala la mikopo, mjadala mwingine uliovuta hisia za wananchi ni kuhusu huduma za afya kati ya pande mbili za Muungano.

Soma pia: Bajeti ya Zanzibar haiwezi kutoa Matibabu kwa watu Milioni 60

Wiki iliyopita, Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa watu ambao si Wazanzibari kupitia mfumo wa bima ya afya wa Zanzibar.

Kauli hiyo ilitafsiriwa na baadhi ya watu kama ishara ya ubaguzi dhidi ya Watanzania Bara wanaoishi au kufanya kazi Zanzibar. Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar ilieleza kuwa suala hilo linahusu utaratibu wa bima ya afya na si ubaguzi wa wananchi.

Mjadala huo ulisababisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kutoa ufafanuzi kwamba mtu yeyote mwenye bima ya NHIF anaweza kupata huduma katika hospitali za Zanzibar zinazopokea bima hiyo, na vivyo hivyo kwa Wazanzibari wanaotibiwa Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwigulu, huduma za afya hazitolewi kwa kuzingatia mtu anatoka upande gani wa Muungano bali kwa kuzingatia taratibu za bima au malipo ya kawaida ya matibabu.

Kauli hiyo ililenga kuondoa hofu ya kuwepo kwa tofauti za kimatibabu kati ya wananchi wa pande mbili za Muungano.

View attachment 3611227

Ajira kwa wazawa kuwa ajenda mpya​

Suala lililoibua mjadala mkubwa zaidi ni ajira kwa Wazanzibari, hususan katika sekta ya utalii ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa visiwa hivyo.

Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh, amesema takwimu zinaonyesha kuwa licha ya Zanzibar kuwa na hoteli zaidi ya 1,100 zilizosajiliwa, sehemu kubwa ya wafanyakazi katika baadhi ya hoteli hizo si wazawa wa Zanzibar.

Akitoa mfano wa hoteli moja aliyotembelea, amesema kati ya wafanyakazi 156 waliokuwapo, Wazanzibari walikuwa 27 pekee.

Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu ushiriki wa vijana wa Zanzibar katika fursa za kiuchumi zinazotokana na uwekezaji mkubwa wa utalii unaoendelea visiwani humo.

Hassan amesema Serikali imepewa jukumu la kuhakikisha vijana wa Zanzibar wanapata nafasi kubwa zaidi za ajira katika miradi inayotekelezwa visiwani humo. Kauli yake imepokelewa kwa hisia tofauti, ambapo baadhi wanaiona kama juhudi za kulinda maslahi ya wazawa huku wengine wakihofia inaweza kutafsiriwa kama ubaguzi dhidi ya Watanzania kutoka upande mwingine wa Muungano.

Soma pia:Mbunge Mohamed Ali: Kama kuwatetea vijana wa Zanzibar kutavunja Muungano basi acha uvunjike

Je, kudai haki za Wazanzibari ni ubaguzi?​

Swali hilo limekuwa kiini cha mjadala unaoendelea Zanzibar.

View attachment 3611228
Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia ACT-Wazalendo, Dkt. Nasra Nassor, amesema madai ya Wazanzibari kutaka nafasi zaidi katika ajira na masuala mengine ya kiuchumi hayapaswi kutafsiriwa kama ubaguzi.

Kwa mujibu wake, changamoto kubwa ipo katika kutokuwepo kwa muundo unaoeleweka vizuri wa Muungano unaofafanua kwa uwazi haki na wajibu wa kila upande.

Amesema vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara wanahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu haki zao ndani ya Muungano ili kuondoa migongano inayojitokeza mara kwa mara kuhusu ajira, huduma na fursa za maendeleo.

Kauli hiyo imeakisi mtazamo wa baadhi ya wanasiasa wanaoamini kuwa malalamiko mengi yanayotolewa leo yanatokana na masuala ya kimuundo ambayo hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu tangu kuundwa kwa Muungano mwaka 1964.

Serikali yakanusha madai ya ubaguzi​

Wakati mjadala huo ukiendelea, Serikali ya Zanzibar imeendelea kusisitiza kuwa hakuna sera ya ubaguzi dhidi ya wananchi wa Tanzania Bara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma, amesema wananchi wa pande zote mbili wamekuwa wakiishi, kufanya biashara na kupata huduma katika maeneo yote ya Muungano bila vikwazo.

Amesema madai kwamba Watanzania Bara hawapati huduma sawa Zanzibar ni upotoshaji usio na msingi, akisisitiza kuwa hata Wazanzibari wengi wanaishi na kufanya kazi Tanzania Bara bila changamoto.

Kwa nini chokochoko hizi wakati huu?​

Kwa wachambuzi wa siasa, mijadala inayoendelea sasa si jambo jipya. Hoja za ugawaji wa madaraka, ajira kwa wazawa, uhuru wa kifedha na nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kwa miongo kadhaa.

Kinachofanya mjadala wa sasa kuwa wa kipekee ni kwamba unaibuka wakati Zanzibar inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa sekta ya utalii, ongezeko la uwekezaji wa kigeni na matarajio makubwa ya vijana kuhusu ajira.

Katika mazingira hayo, maswali kuhusu nani ananufaika zaidi na fursa hizo yanaendelea kujitokeza. Wakati Serikali ikisisitiza kuwa Muungano una manufaa makubwa ya kiuchumi, kiusalama na kidiplomasia kwa Zanzibar, baadhi ya wananchi na viongozi wanaendelea kutaka marekebisho yatakayoongeza usawa na uwazi katika mgawanyo wa fursa.

Akitoa mtazamo wa jumla, Mwakagenda anasema malalamiko hayo yanakuja kwa kuwa Wazanzibari wameshauchoka Muungano, hivyo wanatamani kuwa nchi huru.

“Ni sawa na mke ndani ya nyumba, anaweza kuvumilia mambo madogo madogo, lakini siku akichoka, hata jambo liwe dogo kiasi gani, hatavumilia,” amesema.
Leadership crisis
 
Watanganyika wenye akili timamu hatutaki muungano wa kinyonyaji. Ni bora uvunjike ili kila nchi ipambane kivyake.
 
Back
Top Bottom