Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,719
- 42,739
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa Watu wasio Wazanzibar.
Saada ametoa kauli hiyo Juni 8, 2026 wakati akijibu hoja kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia vikao vinavyoendelea vya kujadili bajeti mbalimbali.
“Mtu ambaye sio Mzanzibar anakwenda katika hospitali zetu anaonesha matibabu kadi, pili Watu kuzuiwa nadhani nilitoa maelezo sana, sio ZHF inaanza bali inaendelea kuwasajili wengine ambao sio wa sekta ya umma”
“Wakati Wanachama wa ZHF wakiendelea kusajiliwa kulikuwa na Matibabu Kadi zikitolewa unakwenda kwa Sheha unachukuliwa taarifa zako unakwenda hospitali hakuna anayekurudisha ilo moja, la pili kilichokuwa kikibainika kwa wenzetu wa hususan kwa ngazi ya Masheha si waaminifu, Mtu si Mzanzibar anakwenda kwenye hospitali zetu anaonesha matibabu kadi na wale waliokuwa wanakaa pale wanamwambia atoe kitambulisho cha Mtanzania”
Soma Pia: Zanzibar: Naibu Waziri wa Vijana, Hassan Khamis: Wanaofanya kazi kwenye Mahotel Zanzibar siyo wazawa inabidi tufanye Mapinduzi
“Bajeti yetu ya trilioni 8 tutaweza kuwatibu Watu milioni 60 ? Tumeona wengine sio Wazanzibar wanatibiwa kwa kutumia matibabu kadi,”amesema Kaimu Waziri wa Afya.
N.B: Huyu mama tukumbuke alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya Muungano