Dada pole sana,yaliyokupata wewe yalinipata mimi,ingawa mie ni mwanaume.Yupo dada mmoja nilimpenda sana sana,na nilimkuta darasa la 7 nikamsomesha akafika diploma,nikampangia nyumba na nikamtafutia kazi,mie nina mke wangu wa ndoa yeye akawa nyumba ndogo.Tuliishi nae miaka 7 na kila nikimpa mimba anatoa,akaomba nimbunulie gari nikafanya hivyo na kila alichoomba nilijitahidi kumpa.Siku moja alinipigia simu akiwa na mama take mzazi na kuniambia nimkome na kwamba hana shida na mimi bali alikuwa na shida na hela zangu hivyo nisimjue tena.Nilisikia uchungu sana nikamjibu asante.Kila siku nilikuwa namuomba mungu anipe uwezo nimsahau na ansamehe yule dada,baada ya mwaka nilimsahau kabisa na nilipata mdada mwingine ambae tunaishi nae vizuri sana,sasa baaday ya miaka 4 hivi yule dada alipigika ile mbaya sasa hivi yupo tu hapa mjini anafanya vibarua vya kufagia ofisi za watu,nakuomba ujifunze kitu kwenye huu mkasa wangu