Mapenzi yanaongezeka zaidi tarehe za mshahara tu

Mapenzi yanaongezeka zaidi tarehe za mshahara tu

Etiiiiiiiiiii…..!!!!!! Mbona ni hatari sana hiyo.!!
Ni wapi uko.?? 😳😳
Ni ndani ya mkoa wa mbeya...ningeweza kukutajia hata jina lake uthibitishe maana ilikuwa gumzo la mwezi mzima....kifupi alikuwa ni bro alietuacha shule ya msingi, akaingia kwenye mishe ya mafuta, baada ya kumaliza shule ya msingi, akatoboa, akawa hakamatiki tena....

akafirisika, akaumwa sana, kisha akafariki....
 
Ukitaka Kuvunja Ndoa Ulizia Pesa Ya Mwanamke.

Pesa Ya Mwanamke Ni Ya Kwake Na Wazazi Wake.

Pesa Ya Mwanaume Ni Ya Familia(Mama & Watoto) Na Ndugu.


Mtu Akioa Mwanamke Mwenye Kazi Ukitegemea Umepumguza Shida Hiyo Ndoa Ikitoboa Miezi Mitatu Utanikuta Pale.
Sahihi kabisa mkuu...na huu ndio ukweli wengi tunapitia na hawa viumbe
 
Ni ndani ya mkoa wa mbeya...ningeweza kukutajia hata jina lake uthibitishe maana ilikuwa gumzo la mwezi mzima....kifupi alikuwa ni bro alietuacha shule ya msingi, akaingia kwenye mishe ya mafuta, baada ya kumaliza shule ya msingi, akatoboa, akawa hakamatiki tena....

akafirisika, akaumwa sana, kisha akafariki....
Dah!! Sema km ni Mbeya sawa watu wa huko network ndogo 🤣
 
Hapo mwanaume ndio mpumbavu,mi ndo nasema sitaki mwanaume jina!
Mwanaume lzm uwe na msimamo kwenye familia!

Ss anamruhusu vipi mke aweke dada wa kazi ilihali mke ni mama wa nyumbani?

Yeye ilitakiwa aweke msimamo, nyumbani kwangu sitaki dada,full stop!
Huo mshahara elf50 wa dada SI angefanyia mambo mengine?

Huyu mwanaume ndo maana mke anamletea drama
Nami nashangaa mama wa nyumbani anaajili house girl, mke kazi gani anafanya sasa
 
😂😂😂😂 Badae kama utaweka story naomba usinisahau.
Haya bonge
FB_IMG_17074712392880868.jpg
 
Sijawahi kununua mwanamke anayejiuza. Ila huyu mke wangu ni anajiuza kwangu. Kivipi?

Manjonjo na ushirikiano kitandani anautoa kwangu tarehe za mshahara tu. Yaani kuanzia tarehee 21 hadi 23 kila Mwezi, asikuambie mtu na enjoy vibaya mno utadhani tumejuana leo. Lakini akiona naanza kuacha 5000 hadi 10000 ya matumizi, anajua tu mume account ime dorola. Hapo ni kinyongo na masimango tu.

Huwa najitagidi kununua vitu kwa pamoja punde tu mshahara ukitoka. Lakini mke hapendi utasikia matumizi mabaya ya pesa, mafuta lita 5, unga kg 25 unataka kufungua duka? Mara tuta kula wali kila siku, sijui ugali kila siku. Na tarehe za mshara shida kwao haziishi, mara mama mgonjwa, dogo hana kalo, sijui msimu wa parizi.

Niliwahi kukodi shamba alisimamie aisee nilitamani kulia, nae alajifanya boss wakampiga pesa ya Pembejeo, mahindi yakageuka na kuwa tumahindi. Biashara ndo kabisaaa alishashindwa. Anachojua yeye ni kupendeza, avae abadili nguo mpya kila uchwao. Katoto kenyewe kamoja tuliko nako amekatelekeza kwa binti wa kazi.

Kwakuwa ndoa ni Changamoto navumilia. Ila wanawake nimewaogopa naweza piga chini huyu nikadondokea kaa la moto. Maana braza yeye kanishauri nitafute mwanamke anayejua maisha na nikiangalia yeye ameshaachana na wanawake tatu mpaka sasa na wote amezaa nao.

Nasoma tu comment zenu, maana sishauriki kama wanavyo niitaga kwetu.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Aisee hii story kama yangu!Kuna kipindi atabadilika ila itakuwa majuto mkuu,omba Mungu uendelee kuwa kwenye ajira maana atajuta na hakuna wa kumuokoa!
 
Yaani huyo kaka ake ndo anaenda kupata HIV kwa kwa kubadili wanawake 🤣🤣🤣🤣
Mtu mmoja ukaachane na wanawake watatu..?? Na kila mtoto na mama ake!!
Halafu huyo kaka ake ndo hawa humu wanaopinga single maza 😂😂😂
Imagine 🤣
 
Back
Top Bottom