Mapenzi yanaongezeka zaidi tarehe za mshahara tu

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
904
526
Sijawahi kununua mwanamke anayejiuza. Ila huyu mke wangu ni anajiuza kwangu. Kivipi?

Manjonjo na ushirikiano kitandani anautoa kwangu tarehe za mshahara tu. Yaani kuanzia tarehee 21 hadi 23 kila Mwezi, asikuambie mtu na enjoy vibaya mno utadhani tumejuana leo. Lakini akiona naanza kuacha 5000 hadi 10000 ya matumizi, anajua tu mume account ime dorola. Hapo ni kinyongo na masimango tu.

Huwa najitagidi kununua vitu kwa pamoja punde tu mshahara ukitoka. Lakini mke hapendi utasikia matumizi mabaya ya pesa, mafuta lita 5, unga kg 25 unataka kufungua duka? Mara tuta kula wali kila siku, sijui ugali kila siku. Na tarehe za mshara shida kwao haziishi, mara mama mgonjwa, dogo hana kalo, sijui msimu wa parizi.

Niliwahi kukodi shamba alisimamie aisee nilitamani kulia, nae alajifanya boss wakampiga pesa ya Pembejeo, mahindi yakageuka na kuwa tumahindi. Biashara ndo kabisaaa alishashindwa. Anachojua yeye ni kupendeza, avae abadili nguo mpya kila uchwao. Katoto kenyewe kamoja tuliko nako amekatelekeza kwa binti wa kazi.

Kwakuwa ndoa ni Changamoto navumilia. Ila wanawake nimewaogopa naweza piga chini huyu nikadondokea kaa la moto. Maana braza yeye kanishauri nitafute mwanamke anayejua maisha na nikiangalia yeye ameshaachana na wanawake tatu mpaka sasa na wote amezaa nao.

Nasoma tu comment zenu, maana sishauriki kama wanavyo niitaga kwetu.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
I mean no malice to nobody
Screenshot_20240116-162151_1.jpg
 
Mkiambiwa oeni wanawake wenye kazi hamtaki. Mwanamke mwenye kipato asilimia kubwa mapenzi yake kwako ni genuine.

Sasa unaoa mwanamke anakaa tu nyumbani anategemea umpe hela ya chakula abane atoe hela za kikoba, za kusaidia ndugu nk, halafu unalalamika mapenzi yanaongezeka tarehe za mishahara?

Pole sana mkuu, pole sana. Vumilia tu.
 
Mkiambiwa oeni wanawake wenye kazi hamtaki. Mwanamke mwenye kipato asilimia kubwa mapenzi yake kwako ni genuine.

Sasa unaoa mwanamke anakaa tu nyumbani anategemea umpe hela ya chakula abane atoe hela za kikoba, za kusaidia ndugu nk , halafu unalalamika mapenzi yanaongezeka tarehe za mishahara?

Pole sana mkuu, pole sana. Vumilia tu.
Aisee siwezi oa mwanamke mwenye kazi, Wana shida haoo🤣😀😀
 
Back
Top Bottom