Mapenzi ya mtandaoni yameniangushia kwa binti mwenye ulemavu, hakika huyu ndiye chaguo la moyo wangu

Mtunze sana mtoto wa watu, muheshimu na umthamini. Fanya kazi kwa bidii usije mkosesha haja za moyo wake
 
Mpende tu kaka
Kama Moyo wako uko tyr
Ana haki ya kupendwa na yeye
Kama Binadam
Hujafa hujaumbika.
 
Kama vile hulalamiki, ila unalalamika.

Anyway, kila la kheri kwenu
Ni kweli maana kiukweli Myebusi Mweusi hajitambui kuwa sasa yupo saa 12 asubuhi, bado yupo kitandani na macho yake hayaoni, baadaye akiamka saa 1 ataanza kuona; je ataishi naye huyo hadi saa 12 Jioni? Nadhani Ven26 unanipata.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa mpweke ila siku za karibuni kwenye mtandao nikawa niko busy na dada mmoja mzuri sana.

Basi tukaona kuna haja ya sisi kuonana kwani niko Dar na Yeye yuko Dar. Tukapanga kukutana naye Slipway.

Ijumaa jioni baada ya saa za kazi nikawa nimepiga kambi Waterfront Bar, nikaangiza kinywaji changu huku nikimsubiri mrembo.

Haikuchukua muda mrefu, angaingia msichana mrefu mweupe. Nikamkaribisha kwa hug moja matata sana.

Ule ulemavu wa mkono wake uliokatwa baada ya yeye kupata ajali, kwangu sijaona kwamba ni kasoro wala dosari. Nimeona ni chachu ya mimi kumpa moyo wangu wote, kumpenda zaidi na kumtunza kikamilifu.

Huyu binti sitaki nimuache, daima amekuwa akilini mwangu. Sijawahi kupenda namna hii.

Namuomba Mungu aliimarishe penzi letu hata tuufikie mwisho mwema
Kipendacho roho ni dawa
 
Back
Top Bottom