Mapenzi Na Mafanikio Ya Mwanamke

Matatizo ya aina yapo mengi sana katika jamii yetu na hasa baada ya kina mama kuendelea kielimu/taaluma/kipato. Lakini kwa maoni yangu siwezi kuwalaumu kina mama kwani ninahisi chimbuko kubwa la matatizo ya ndoa zetu ni namna tulivyoanza.
Jee kabla ya kuoana kila mmoja alikuwa anamuelewa mwenzake kihivyo au ilikuwa infatuation ikafikia mahala wote mkahisi mko kwenye dimbwi la mapenzi na kuamua kuoana[ wakati mnaamua hivyo kila mmoja wenu ana sababu zake za kutaka hiyo ndoa na hizo sababu ni tofauti sana kiasi hata baada ya muda haziondoki ila zinajificha moyoni. Kasheshe inakuja wakati kunakuwepo na mafanikio ya kimaisha kwa mmoja wa wanandoa na kuanza kufikiri kuwa mafanikio hayo ni yake binafsi ndipo vituko huanza [hata wanaume] na mwisho wa yote ni kutengana na kuwaachia mtihani mgumu watoto.
 
Ha-ha-ha-ha MTM unasomesha mke?...Pole! that's all i can say,,,subiria akisha graduate atataka talaka...Nimeshaona watu wengi (tena washikaji wa karibu sana)walisomesha hivyo hivyo mke kamaliza shule kachukua chake mapema...kamuacha mume anatoa macho!....but you never know labda wako mstaraabu...siyo wanawake wote though wako hivyo ila you never know....hahahahaha mnyalu umeula hahahaha pole in advance!
..BM..nimekugongea ka-senksi pale. kiukweli kuna baadhi ya wanawake ambao wakifanikiwa kielimu na kimaisha wakiwa ndani ya ndoa huanzisha kiburi na wakati mwingine hata kutishia kuondoka pindi ataona mambo si mambo. Kwa mujibu ya ufahamu wangu, wao hudai kuwa once akipata elimu nzuri e.g Master, PhD etc na mungu akamsaidia na kazi nzuri ikaja anaamini anakuwa amejikomboa sana katika suala kubwa la kipato ambacho wao hudai ndio jambo linalowatia wanawake wengi utumwani...Hata mimi mchuchu wangu aliwahi kuniambia kuwa once aki-graduate atatafuta kazi nzuri na wala sitamsikia akinipiga mizinga...si ndio dalili zenyewe hizo??!!
 
..BM..nimekugongea ka-senksi pale. kiukweli kuna baadhi ya wanawake ambao wakifanikiwa kielimu na kimaisha wakiwa ndani ya ndoa huanzisha kiburi na wakati mwingine hata kutishia kuondoka pindi ataona mambo si mambo. Kwa mujibu ya ufahamu wangu, wao hudai kuwa once akipata elimu nzuri e.g Master, PhD etc na mungu akamsaidia na kazi nzuri ikaja anaamini anakuwa amejikomboa sana katika suala kubwa la kipato ambacho wao hudai ndio jambo linalowatia wanawake wengi utumwani...Hata mimi mchuchu wangu aliwahi kuniambia kuwa once aki-graduate atatafuta kazi nzuri na wala sitamsikia akinipiga mizinga...si ndio dalili zenyewe hizo??!!

eh??? dalili ya mvua..... sasa halafu? lakini pia wanaume mnakwenda mnapatana na mrembo kasoma weeee mnatusahau sie mama za watoto wenu!! ati tumezeeka..hakuna time tena ya malavi davi..wengine wanasema wanataka wake presentable...mamabo yenyewe ndiyo hayo.
 
Haya ni mabadiliko ya kawaida ya binadam. Watu hubadirika mwili na mawazo. Ni mawe tu yasiyobadilika. Wengi hudhani kuwa kama mtu mnapendana mapenzi hayataisha. Mapenzi huisha na wataalam wengi wanaamini ndoa baada ya miaka miwili, ni commitment zaidi ya mapenzi. Elimu ni kati ya vitu vinavyobadilisha sana watu mtazamo; positively or negatively kutegemeana na mtu mwenyewe.

Kwa hiyo inategemea huyo aliyeasi alikuwa anahisi vipi ndani ya mahusiano yake. Mi naona mambo kama haya inatakiwa yae encouraged badala ya kung'ang'aniza watu kubaki na mahusiano yasiyo lipa au mahusiano yaliyochoka.

Tusipokuwe selfish, mwenzio akisema anasepa, we mpe farewell halafu u endelee. Kung'ang'ania mahusiano yaliyochoka sometimes ni kujihukumu maisha!!
 
Wazee wa zamani walisema kua uyaone. Hiyo ni pamoja na tabia research nyingi zilizofanywa zinaonyesha kwamba akina mama kati ya miaka 40 -50 huwa hawataki kuishi tena na waume zao hasa kama wanaweza kujitegemea kimaisha. Vile vile usisahau kuna kuoana kwa kupendana kiukweli na kiuongo. Wengine huoa kwa sababu hawana namna na wengine huwa wanategemea vitu fulani fulani wakivikosa basi tafrani. Life is too short enjoy.


Kwenye bold....una point ndugu yangu.
Ndoa ni taasis ngumu na isiyotabirika.Mahusiano ya kwenye ndoa huenda yakibadilika kadiri miaka inavyozidi kwenda.Mwanzoni wana ndoa huweza kuanza kwa style yoyote - chini na pole pole kupanda kimaisha...hapo kuna wanaume wengine hujikuta wakibadilika kitabia kwa kulewa mafanikio... hapo wanawake hupata mateso makubwa sana lakini kwa vile mtu anataka kupigania ndoa na labda wanae basi hukomaa na kuvumilia tu.
Pia wapo wenye kuendelea kuleana na kufurahia maisha pamoja kadri maisha yanavyoendelea kuwa mazuri.

Kuna wanaoanza maisha katika hali iliyo bora kifedha - hapa inategemea pia.Mafanikio haya ya mwanzo huweza kujenga tension na migogoro isiyoisha kutegemeana na sababu zilizowafanya wanandoa hao kuoana.Kama ndoa ilianza kwa kufuata mali/vitu pasipo na mapenzi ya kweli basi wanandoa huweza kujikuta wakijutia ndoa zao na hivyo kuanza harakati nyingine za kuishi hata kama wapo pamoja kwa kujionyesha tu.


Tukirudi katika ishu aliyoleta MTM - NAWEZA kusema kuwa inategemea mafanikio hayo unayapima vipi maana cheti tu na huku hakijaleta chochote si waranti wa kuondokea.Tuangalie mafanikio na hali halisi ya ndoa ya mwanamke husika.Nitaomba kutoa maelezo yafuatayo:

1.Mwanamke mwenye amani hawezi kuchukulia mafanikio yake kama sababu ya kuvuruga amani na uhusiano katika ndoa.Mwanamke anayefanikiwa mara nyingine hujikuta akiingia katika matatizo mengine ndani ya ndoa yake kutokana na hali halisi ya fikra na mitizamo ya kijamii akiwemo mumewe.

2.Kuna wanaume hawajiamini kuwa na mwanamke wa namna hiyo na kila mara hujikuta wakitaka kuonyesha bado wao ni wanaume na kupelekea ukatili wa ajabu - maneno ya kejeli, vipigo wakati mwingine n.k na mifano ni mingi sana. -Hii hupelekea mwanamke kuona hakuna sababu kuishi maisha ya masimango ha hasa kama anataka kuendeleza career yake.

3.Kipindi cha maisha nacho kinachangia.Wanawake wengi hutaka security ya aina fulani. Ni wachache sana wa umri mdogo utawakuta wakiwa na mafanikio ya kutisha na ya kuwapa jeuri ya kujiondosha. Mpaka mtu apate kwa mfano PHD au awe kwenye hali nzuri ya kuridhisha kikaziau biashara atakuwa angalau amevuka miaka 30. wanawake katika umri huo na hasa 40-50 wengi hujikuta wameshapitia mengi katika ndoa zao.Wameonja nini kuwa kwenye ndoa - raha na karaha zake, wamelea watoto wao.Wenye kufanya kazi au biashara, ni umri ambao wameshakomaa na wako katika hali nzuri sana ( cheo, fedha, kujiamini).Umri huu pia couples wengi wanakuwa katika maisha wanayoyajua wenyewe - kama ni maamuzi basi mtu anakuwa anajipanga kwa muda mrefu na hadi afikie umri huu tayari anakuwa yuko tayari kwa matokeo yoyote.Hivyo si ajabu kuona mama wa umnri huu akiamua kuachana na ndoa isiyompa faraja/furaha na amani kwa kutumia style mbalimbali - wengi hawatapoteza muda kudai talaka ambazo ni gharama( muda na fedha), watatafuta njia ya kistaarabu kuondokea kama kutafuta kazi nje ya nchi/mkoa, kuhama nyumba n.k.Ukichunguza sana utakuta wanatoka katika ndoa zenye migogoro ya muda mrefu sana.Hakuna mwanamke wa umri huo atakayeamka siku moja tu na kuishia.
Haya ni maoni yangu kufuatana na niliyoyaona.
 
WoS
Welcome back! Napitia mjadala kwanza then ntachangia.
 
kuna ukweli flani, wanawake wengi wako hivyo.

hata mi najiuliza sana naomba yasinikute maana ndo anamalizia shule ph D yake.

Mungu apishe mbali
 
Sasa najiuliza, hivi kuna uhusiano kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa??? Nafahamu humu ndani kuna matawi yote na nategemea msaada maana mie nasomesha mke na nimeshaanza kuogopa

Please advice

Mafanikio ya mwanamke (au mwanaume) kielimu, fedha au hata madaraka inaweza ikaathiri (chanya au hasi!) ndoa na mifano ya haya ipo mingi tu including hiyo miwili unayoishuhudia.

Kuna parameters nyingi tu zinazofanya watu wafikie kuoana. Kiwango cha elimu, kipato (real or potential) ni baadhi tu. Nyingi (kama si zote) ya parameters hizi zipo subject to change (zipo dynamic). Lakini kubwa ya yote inapaswa kuwa mapenzi.

Mafanikio kiuchumi, elimu au madaraka yanaweza kuleta athari hasi katika ndoa endapo kitu kikubwa kilichokuwa kinafanya ndoa iwepo sio mapenzi baina ya wanandoa.

Kama ndoa haitokani na mapenzi, wanandoa wanatend kujiona kama individuals na si 'mwili mmoja' (i.e. sio 'taasisi'). Hii ni hatari sana, maana mafanikio ya mmoja wa wanandoa yataonekana ni yake binafsi na si ya taasisi.

Pia kama mwanandoa yupo kwenye ndoa zaidi kwa ajili ya kujikimu (wengine huita 'economic refuge'!), then akifikia mahali anaweza kujitegemea umuhimu wa hiyo ndoa unatoweka.

Kuna wengine kupata mafanikio kunamfanya ajihisi yupo level nyingine na hivyo mwenza wake katika ndoa hamfai tena katika level hiyo. Hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na ubinafsi (kama nilivosema hapo juu).

Binaadamu tupo dynamic kwenye aspects zote (physically, emotionally etc), hivyo mitazamo yetu pia hubadilika. Kila ndoa ipo unique lakini hii haiondoi ukweli kuwa kuna baadhi ya vitu vipo common kwa kiasi kikubwa tu kwa ndoa zote.

MTM, ni kumsomesha mkeo ni suala muhimu na hupaswi kuliacha hata kama ukiona kuna uwezekano atakukumbia baada ya hapo. Bila shaka ungependa watoto wako wawe na mama 'msomi' hata kama mama huyo sio mkeo tena!
 
Hata mimi sasa mnanitisha ingawa ni mwanamke!! Kama ni kweli takwimu hii inaongezeka then kuna tatizo somewhere. But ninachowezasema kama mimi ni kuwa kama ndoa ina amani, upendo wa dhati, kuheshimiana, kushirikiana na kusupportiana katu mafanikio hayaweziibomoa.

Kama haya yanakosekana basi itafika wakati uvumilivu utatoweka na ndoa itavunjika bila hata ya PhD, Masters wala certificate
 
.........Msiogope kusomesha wake zenu jamani, muhimu ni heshima, upendo na masikilizano.
Kama kweli wapo wanawake wanaoamua kuacha waume zao kwa ajili ya elimu zao wanasababu toka zamani.
Elimu/mafanikio sio kigezo cha kumuacha mwenzio kama kweli mlipendana kidhati.
 
In anyway, mwanamke asome atakavyo, lakini asimzidi mume!

Akikuzidi madarasa tu, umeuawa, nina mifano mingi sana ya incidence hizi!..Wanakuwa uncontrollable, kelele mingi and so on!, na anakuwa free kukudanganya kuwa anaenda safari kikazi, kumbe wapi!

Ni asilimia 10 ya wanawake ambao watabaki kuwa waaminifu wapatapo mafanikio kielimu!
 
Hizo ni hulka tu kama kweli mnapenda na mmeoana kwa dhati yaani thati hapo ni msisitizo yaani kila mmoja anamdhamini mwenzake ni vigumu sana kutokea hilo jambo kwa wale wenye uelewa kama ndoa za kufuruhishana tegemea hilo
 
In anyway, mwanamke asome atakavyo, lakini asimzidi mume!

Akikuzidi madarasa tu, umeuawa, nina mifano mingi sana ya incidence hizi!..Wanakuwa uncontrollable, kelele mingi and so on!, na anakuwa free kukudanganya kuwa anaenda safari kikazi, kumbe wapi!

Ni asilimia 10 ya wanawake ambao watabaki kuwa waaminifu wapatapo mafanikio kielimu!

jamani mume wangu si mwenza wangu, aibu yake yangu, mafanikio yangu yake.

sasa ya nini nimletaa nyodo ilhali ntakua najidhalilisha mwenyewe??? wanawake wanaofanya hivo wana hulka chafu and I dare to say hawakuwa na mapenzi ya dhati kwa hao waume zao.

hivi nimuache mume wangu ninayempenda kwa kuwa eti sasa elimu yangu imemzidi??? hainiingii akilini kwa kweli!!!
 
Asalaam Aleykum

Suala la mwanamke kufanikiwa na kuanza kumuona mumewe yuko chini au hamfai linatokana na sababu nyiingi tu, inawezekana ndoa ilijengwa kwa misingi tegemezi badala ya mising mapenzi hivyo mwanamke akishamaliza tegemezi ndoa inakuwa void. Pia inawezekana kabisa mtu anakuwa hampi mkewe unyumba wa kutosha hivyo bond ilikuwa kwenye support tu na support ikiisha basi tena hakuna hitaji

mengine ni mahusiano ya nje, marafiki wabaya na pia hulka ya kibinadamu ya mwanamke ambaye kwa mwanaume anahitaji ulinzi kabla ya yote, hivyo akikosa huo ulizi basi dume linakua joka la kibisa


samtaim wanawake wengine ni wabaya tu na malezi mabaya kwahiyo akishapata anachotaka basi

kuna dada mmoja yeye anasema jamaa yake hampi tena penzi tamu na huyo dada ana pesa kwa hiyo ana options kibao
 
Habari za siku tele? Nimesoma mawazo machache kati ya yaliyoandikwa na wengi ila nimegundua jambo moja kubwa sana hapa na ndilo liliotawala.
"mwanamke hapaswi kuwa na elimu zaidi ya alionao mumewe"
Kwa kusema haya ina maana kuwa mwanamke ni kiumbe ambaye siku zote atawaliwe na mwanaume. Na mawazo kama haya ndio yanazaa matatizo mengi kwa kina mama hasa wale ambao wanapiga hatua kielimu. Ukimwuliza mwanaume kwanini binti fulani mwenye elimu mtaani haolewi atasema "atashikika wapi yule". Ina maana wanaume wanatambua elimu ni ukombozi. Na ukombozi humweka huru mtu. Na mwanamke akiwa na elimu atakuwa mtu huru wakati kiutamaduni mwanamke anatakiwa 'AKALIWE'. Mawazo haya huleta uwoga kwa wanaume wengi.
mbaya zaidi wakipata mwenza mwenye kupenda maendeleo basi hutafsiri kuwa mwenza huyu anataka awe 'HURU' yaani asikaliwe na mumewe.

Sasa kwa wale wanaoingia katika ndoa wakiwa na fikra potofu kama hizi, lazima 'ukombozi' kwa mwanamke utawatia hofu sana. Matokeo yake wengi hujiwekea 'defense mechanisms' mapema sana katika ndoa zao. Na hizi mechanisms huzaa matatizo mengi ambayo wanawake hawa wenye kiu ya maendeleo wanatafsiri wakati mwingine kama 'mume hanipendi niendelee', 'mume ananinyanyasa' n.k. Vitu vidogo kama hivi huzaa matatizo hasa pale mwanamke anapoendelea kwenda mbele au akafanikiwa kujikomboa kwa kupata elimu basi masengeyo ya waziwazi kutoka kwa mwanaume akitaka kuhakikisha kuwa je bado mimi niko juu ya huyu mwanamke au la. Kwa wanandoa wengine huzaa vipigo vya waziwazi, dharau za waziwazi tena usisahau kuwa ni mwanaume anayefanya haya. Unategemea mwanamke aliyekombolewa atafanyaje katika hali kama hiyo? Wenye mioyo myepesi wanakimbia, wenye mioyo migumu wanakaa na kuvumilia. Nina rafiki yangu aliniambia kuna mambo matatu ambayo mwanaume asiyetaka mke wake anayetafuta maendeleo aendelee anamfanyia. Visa hivi vitatu ni

1. Kwenda nje ya ndoa na kuwa na mahusiano ya wazi na mwanamke mwingine

2. Kumpiga mwanamke ili atambue kuwa yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho

3. Kuamua kuwa na gubu na ugomvi wa mara kwa mara na kuonyesha dharau mbele za watu mbali mbali ili mwanamke ajione si lolote na hafai

Jamani kuta nne zinaficha mambo mengi. Kutokana na tabia hizi wanaume wengi huwa ni wasahaulifu sana wa matendo yao kwa wake zao. Kwa kuwa wao ndio watendaji wanakuwa wepesi wa kusahau, mwanamke ambaye ni mtendewa huwa hasau. Mambo haya yanamjaa moyoni mpaka pale aseme yatosha!!
HUU NI UPANDE MMOJA TU.

Upande mwingine wanawake sisi wenyewe tunakuwa hatuna nia njema na ndoa zetu au tunagundua kuwa yule tuliyefunga naye ndoa hafai hii inatokana na kutokuwa na penzi la dhati. Wengine sasa wanapiga hesabu ya namna ya kumkimbia mume mapema sana. Na hili nasema ni rahisi kwa mume kugundua tokea mwanzo. Maana utamwona mke ana calculations kibao ila ukiangalia katika calculations zake, wewe kama mume you do not exist. hii ni red flag kwa mwanaume.
Jamani tusipende kukimbilia ndoa kwa kuwa ni fashion au the next big thing. Ndoa inahitaji utulivu sana tena mkubwa mno.

Kwa MTM, kila ndoa ina formula yake. Usijeukachukulia unayoambiwa na mtu mwingine kuwa ndio yatakayotokea kwako. unless otherwise unaanguka katika kundi la mwanzo nililolitaja. Fikiria tabia za mke wako, kitu kilichofanya muunganike, je bado ni kile kile na ndio kina-apply hadi leo. Kumbuka pia ndoa kama tasisi yoyote ya kibinadamu, hubadilika kutokana na nyakati na mapitio yenu. Kuwa tayari kubadilika sambamba na mkeo. Umpe support ya kutosha tena kwa upendo mwingi, hesabu kusoma kwake kama baraka kwa familia yenu na pia usisahau kusisitiza kuwa familia ni kitu muhimu sana kwako kama ilivyo kwake na unaamini anayoyafanya ni kwa faida yenu sote.

Usije ukaweka mawazo ya watu wengine au mifano ya watu wengine kama vigezo vya kuendeshea ndoa yako. Kumbuka yale yaliwakuta watu tofauti na nyakati zilizo tofauti na wana tabia tofauti na nyie. DO NOT USE THEM AS A STANDARD FOR YOUR RELATIONSHIP. YOUR RELATIONSHIP IS HOW YOU CHOOSE TO DEFINE IT.

Mimi binafsi ninaamini nini:

1. Ninaamini mwanamke ana haki ya kuendelea kimasomo (si kwa sababu mimi ni mwanamke) kwa kuwa yeye ni binadamu kama binadamu mwingine na ni haki yake ya msinig

2. Ninaamini ndoa ni taasisi inayopaswa kuheshimiwa na mume na mke, na mume na mke watambue wajibu wao kwa kila mmoja wao katika kuhakikisha haki sawa inapatikana kwa wote.

3. Ninaamini kwa kuwa mwanamke na mwanaume wako sawa, basi vivyo hivyo katika uhusiano wao katika ndoa wako sawa.



kazi njema
 
Mwanafalsafa mmoja wa kale katika China (tshan zuu-sijui kama nimeandika jina kwa ufasaha) alisema kila mwanaume ameumbiwa mke na kila mwanamke ameumbiwa mume. Tatizo ni kutambua mkeo au mumeo yuko wapi. Unaweza ukawa milima ya uporoto na mkeo au mumeo akawa milima ya elgon uganda.

ukimsomesha mkeo au mumeo au mkeo akifanikiwa kisha akakutema, ujue hakuwa mkeo, ulioa mke wa mtu mwingine.
Note kuwa wapo pia wanaume ambao wakishafanikiwa hawapendi kutoka hata na wake zao, wanashindwa tu kuwaacha physically wanakuwa wamekwisha kuwaacha. Wengi huogopa tu kama kuna ishu ya kulea watoto, wengi huogopa mama wa kambo kwa watoto.
 
Bimkubwa nimeipitia posts yako mara nyingi aisee.... iko deep sana hii post; kweli weye ni bimkubwa, nakubaliana kabisa na maoni yako,

ila bado naona kuna point moja umeimiss... lengo langu si kuaddress ukandamiza au ukaliaji au masuala ya haki sawa... hayo!!! lengo ni kujua chanzo cha matukio ya mama kuota mbawa akishapata "tools" na namna ya kumsaidia mwanaume kuzuia haya yasitokee kwani mwisho wa siku watoto ndio watateseka

Kuhusu kumuendeleza mke, mimi kwangu hiyo ni moeal responsibility kwani kumuendeleza yeye ni kuendeleza familia na jamii kwa ujumla, maana hata watoto wangu wataishi bomba kama nikitangulia mbele ya haki
 
In anyway, mwanamke asome atakavyo, lakini asimzidi mume!

Akikuzidi madarasa tu, umeuawa, nina mifano mingi sana ya incidence hizi!..Wanakuwa uncontrollable, kelele mingi and so on!, na anakuwa free kukudanganya kuwa anaenda safari kikazi, kumbe wapi!

Ni asilimia 10 ya wanawake ambao watabaki kuwa waaminifu wapatapo mafanikio kielimu!
Hivi unasema kweli PJ ..nina mpango wa kuendelea na elimu mpaka nimzidi mme wangu kabisaaaaaaaaaaa ..sijui na mie nitabadilika ??:eek:
 
Back
Top Bottom