FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,792
- 5,373
Mwanafalsafa mmoja wa kale katika China (tshan zuu-sijui kama nimeandika jina kwa ufasaha) alisema kila mwanaume ameumbiwa mke na kila mwanamke ameumbiwa mume. Tatizo ni kutambua mkeo au mumeo yuko wapi. Unaweza ukawa milima ya uporoto na mkeo au mumeo akawa milima ya elgon uganda.
ukimsomesha mkeo au mumeo au mkeo akifanikiwa kisha akakutema, ujue hakuwa mkeo, ulioa mke wa mtu mwingine.
Note kuwa wapo pia wanaume ambao wakishafanikiwa hawapendi kutoka hata na wake zao, wanashindwa tu kuwaacha physically wanakuwa wamekwisha kuwaacha. Wengi huogopa tu kama kuna ishu ya kulea watoto, wengi huogopa mama wa kambo kwa watoto.
tathimini zako nashindwa kuzipa 100% hazinipi majibu fasaha !