Mapenzi kweli yalikuepo zamani

KASHAMBURITA

JF-Expert Member
Mar 27, 2021
200
630
Unakijua kisa cha Leyla na Majnun (mapenzi bikra)?

Leyla na Majnun ni kisa maarufu duniani kilichotokea kweli katika Uarabuni, na kwa kisa hiki kimepelekea kutungiwa mashairi mbali mbali duniani. Wengine hukiita kisa hiki kama "Romeo na Juliette wa Mashariki," ni kisa chenye mafunzo kwa makubwa.

Qays ibn Al -Mullawah alipendana na binti mrembo aliyeitwa Layla al Aamiriya. Qays mapenzi yalimzidia ikawa kila mara analitaja jina la mrembo Layla. Ikafikia hatua anatunga mashairi ya kuonyesha mapenzi yake kwa Layla, mashairi ya kuonyesha urembo wa Layla, na kila muda haachi kulitaja jina la bibie Layla.

Yale mapenzi yaliyomzidia hadi akashindwa kujitambua kwa mapenzi yake kwa Layla hadi watu wa jamii yake walimuita Majnun (mwehu). Qays alipeleka posa kwa ajili ya kumuoa Layla lakini baba yake na Layla alikataa posa ile akidai binti yake hawezi kuolewa na mtu mwehu.

Na haikupita muda Layla akaolewa na mwanaume mwengine, mwenye hadhi ya juu na mfanyabiashara mkubwa na inasemekana alikuwa na mvuto mno (handsome), uzuri wa mume wa Layla ulisababisha hadi ikawa anaitwa Uwaridi.

Baada ya Majnun kusikia habari za ndoa ya Layla aliumia sana na kuamua kukimbia ule mji na kwenda jangwani. Huko alilia sana huku akiimba mashairi ya mapenzi na mengine akiyaandika kwenye mchanga wa jangwani.

Licha ya familia ya Majnun kujitahidi kumpa moyo ili arudi nyumbani lakini hawakufanikiwa. Baadaye Layla na mumewe waliamua kuhama mji na kwenda Kaskazini mwa Uarabuni, huko aliumwa sana na kufariki.

Watu wengi wanasema kuwa kilichomuua Layla ni maumivu ya moyo kwa sababu baba yake amekataa kumuoza kwa mtu ampendaye (Majnun). Baada ya miaka kadhaa Majnun nae alikutwa amefariki pembeni mwa kaburi la Layla huku akiwa ameandika shairi lenye mistari mitatu kwenye mwamba uliokaribu na kaburi la Layla.

Shairi hilo limeandikwa kama ifuatavyo (shairi liliandikwa kwa Kiarabu lakini hapa limetafsiriwa kwa Kingereza);

I pass by these walls, the walls of Layla,
And I kiss this wall and that wall,
It’s not Love of the walls that has enraptured my heart,
But of the One who dwells within them.

***

Nimevuka kati ya hizi kuta, kuta za Layla,
Na nimezibusu kuta hizi,
Sio mapenzi ya kuta ndio yalonipa furaha na amani katikaw moyo wangu,
Bali ni huyu aliye ndani ya hizi kuta.

NB: tafsiri ya Kiswahili sio rasmi, nimeitafsiri tu mimi.

Qays na Layla wote walipendana, tena mapenzi ya dhati, lakini walikosa nguvu za kupigania penzi lao kwahiyo kila mmoja akabaki na maumivu yake moyoni.
 
We unafikiri kitanda hakizai haramu huu msemo umetungwa tu bila sababu usichojua zamani hekima zao ziliambtana na ujinga
 
WAZAZI wako wamekaa pamoja zaidi ya miaka 30 kwenye NDOA na bado unasema hakuna mapenzi ya kweli, mpendwa utakuwa unakutana na wapita njia wenzako. 🙄😥😓
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom