Maisha na mahusiano ya mapenzi

Roca fella

JF-Expert Member
May 13, 2023
1,247
2,338
Habari za muda ndugu zangu watanzania.
mada husika hapo inaeleza maisha na mahusiano ya mapenzi katika Karne hii ya 21, na kizazi kijacho kwa Karne ya baadae itakuwaje.

kwa Sasa maisha kwa hapa Tanzania kwa asilimia 60% bado yanasua sua, asilimia 40% ni wale wapigaji wa fedha katika miradi na taasisi mbali mbali ili kusongesha gurudumu la maisha yao na kuwa na unafuu kwa siku za usoni.

hii imepelekea maisha yetu kuwa na sintofahamu kwa kijana wa leo, hafahamu kesho yake itakuwaje kulingana mfumo wa maisha ya kitanzania, hivyo kupata unafuu wa leo na kesho basi hujikita katika eneo tofauti tofauti ili mradi maisha yake yanaenda.

kwa miaka ya hivi karibuni tumeona vijana hasa mabinti wakiwa wanadanga ili kujipatia fedha ya kukidhi maisha yao, ingawaje sio wote wenye kudanga ni kutokana na uhaba wa maisha hapana, wengine wanafuata mkumbo, wengine ni hulka hayo, wengine ni kwa mujibu wa shinikizo, na kadhalika......

kwa upande wa vijana wa kiume hivyo hivyo pia, huhatarisha maisha yao pasipo kuwa na fikra za baadaye katika kutengeneza kizazi Bora kijacho, kijana anapitia changamoto nyingi pengine kwa kujitakia ama kweli anapitia mtihani mgumu Kama moja ya hatua ya maisha kwa mwanadamu.
naamini hakuna mwanaume aliyezaliwa na tabia ya ushoga bali tamaa za vijana kutamani maisha mazuri, basi anaangukia huko na kuharibu future yake na maisha kwa ujumla.

Mahusiano pia yamechukua nafasi kubwa mno kuharibu vizazi vyetu kwa mfano wazazi kuuana, wazazi kuua watoto wao kisa ugomvi wao, kupeana ulemavu kisa migogoro kimahusiano, kusababisha vifo kwa mazingira ya kutatanisha ( kulogwa kiuchawi ) kisa mahusiano,


dini za kisasa zimekuwa chanzo Cha kuvunjika kwa mahusiano na maisha kuwa mabaya mbeleni, mwanamke kurubuniwa na mchungaji ama kiongozi wa kanisa kufanya mapenzi, ama muda mwingi kushinda katika nyumba ya ibada na kwa asilimia chache hufanya majukumu yake. Hii imepelekea ndoa ama uhusiano kuvunjika mara kadhaa.


miaka ya Sasa na miaka 50 ijayo kwa mtazamo wa fikra zenye kuona mbali basi pesa imetawala kwenye kila sekta hasa nchi zetu maskini mfano wake Tanzania, vijana wamekuwa wakithamini pesa kuliko utu, zama hizi Imani juu ya kupata mume au mke Bora imetoweka Sasa hivi mwanamke anaolewa kisa pesa, mwanaume anaoa mwanamke mwenye pesa, ama mwanaume anaoa mke atakaye hata Kama hampendani sababu ni fedha, wengine hufanya unyanyasaji, masimango, dharau kisa fedha.

katika familia ili kipato kikuwe Basi binti anaozeshwa bila kujali matakwa yake hata akiwa mwanafunzi anaolewa.

mzazi amemfuma mwanae yupo na mahusiano na mwanaume fulani Basi atakwenda kushtaki ili pesa itoke wamudu maisha,

mabinti wapo radhi kuzaa na waume za watu ili mradi huyo mwanaume anao uwezo kiuchumi atahudumia na gharama zote juu yake.

kwa Karne hii mapenzi yamekuwa ni biashara hakuna upendo wa dhati, huna pesa hupati penzi, unataka pesa toa penzi.


Screenshot_20230703-214501_(1).png


KWA MCHANGO , UCHAMBUZI NA MAONI YANA KARIBISHWA KUJADILIANA ZAIDI.
 
Ningekuzingatia lakini ulishasemaga unatumia kilevi au mmea aina ya ""bangi ""toka ukiwa unapata elimu ya msingi
Screenshot_20230704-142544.jpg
 
Oya, out of topic,mbona siku hizi hauposti wale madem wenye mawezenga kwenye ma comment??
 
Back
Top Bottom