Unakijua kisa cha Mapenzi Bikra? Leyla na Majnun

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
5,689
8,925
Leyla na majnun ni kisa maarufu duniani kilichotokea kweli katika eneo la uarabuni... Na kwa kisa hiki kimepelekea kutungiwa mashairi mbali mbali duniani.... Wengine hukiita kisa hiki kama "Romeo na Juliette wa mashariki".....ni kisa chenye mafunzo kwa makubwa

Qays ibn al -Mullawah alipendana na bint mrembo aliyeitwa Layla al aamiriya...Qays mapenzi yalimzidia ikawa kila mara analitaja jina la mrembo Layla.... Ikafikia hatua anatunga mashairi ya kuonyesha mapenz yake kwa Layla, mashairi ya kuonyesha urembo wa layla, na kila muda haachi kulitaja jina la bibie layla

Yale mapenz yaliyomzidia hadi akashindwa kujitambua kwa mapenz yake kwa Layla hadi watu wa jamii yake walimuita Majnun (mwehu)

Qays alipeleka posa kwa ajili ya kumuoa Layla lakini baba ake na Layla alikataa posa ile akidai binti yake hawezi kuolewa na mtu mwehu

Na haikupita muda Layla akaolewa na Mwanaume mwengine... Mwenye hadhi ya juu na mfanyabiashara mkubwa na inasemekana alikuwa na mvuto mno (handsome) .....Uzuri wa mume wa Layla ulisababisha hadi ikawa anaitwa Uwaridi

Baada ya Majnun kusikia habari za ndoa ya Layla aliumia sana na kuamua kukimbia ule mji na kwenda jangwani.... Huko alilia sana huku akiimba mashairi ya mapenzi na mengine akiyaandika kwenye mchanga wa jangwani

Licha ya Familia ya Majnun kujitahidi kumpa Moyo ili arudi nyumbani lakini hawakufanikiwa

Baadae Layla na Mumewe waliamua kuhama mji na kwenda kaskazini mwa uarabuni ....huko aliumwa sana na kufariki.... Watu wengi wanasema kuwa kilichomuua Layla ni maumivu ya moyo kwa sababu baba yake amekataa kumuoza kwa mtu ampendaye (majnun)

Baada ya miaka kadhaa Majnun nae alikutwa amefariki pembeni mwa kaburi la Layla huku akiwa ameandika shairi lenye mistari mitatu kwenye mwamba uliokaribu na kaburi LA Layla

Shairi hilo limeandikwa kama ifuatavyo (shairi liliandikwa kwa kiarabu lakini hapa limetafsiriwa kwa Kingereza)

I pass by these walls, the walls of Layla
And I kiss this wall and that wall
It’s not Love of the walls that has enraptured my heart
But of the One who dwells within them ”

"Nimevuka Kati ya hizi kuta, kuta za Layla
Na nimezibusu kuta hizi
Sio mapenzi ya kuta ndio yalonipa furaha na amani katikaw moyo wangu
Bali ni huyu alive ndani ya hizi kuta "

Nb* tafsiri ya kiswahili sio rasmi .

Qays na Layla wote walipendana... Tena mapenzi ya dhati lakini walikosa nguvu za kupigania penzi lao kwahiyo kila mmoja akabaki na maumivu yake moyoni ....Majnun Alichanganyikiwa kweli kweli na Layla hakupata furaha na amani ya ndoa

Walipendana lakini hawajawahi kuoana Waka kukutana kitanda kimoja na ndio maana yameitwa mapenzi bikra

umejifunza nini kupitia kisa hiki??

IMEANDALIWA KWA HISANI YA BWANA FACT
 
Ubaguzi haukuanza leo, uwe wa rangi, utajiri, ukabila, utaifa
Ubaguzi ni ubaguzi unauma
 
Layla na majnun hata kanga zilitoka. Hivi kulikuwa na kitabu cha hii stori.
 
Mm nimejifunza akielewa mistari tu shusha chupi mapema usisubiri risiti za wazee Mara unaambukia patupu
 
Back
Top Bottom