Gazeti la Rai leo limelalamika ya kuwa fitna zimetawala katika uteuzi wa baraza la mawaziri................................
Baadhi ya fitna ilizozibainisha ni kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa kwa makusudi mazima wakivujisha siri za uteuzi huo na huku wengine wakishinikiza kupewa nyadhifa za uwaziri wakati ni viongozi wadhaifu........................
Hizi habari siyo za kuzipuuza hata kidogo ....ieleweke gazeti la Rai lina sikio lake pale Ikulu na hivyo yaonyesha migawanyiko na mifarakano ya CCM inatokota ya kugombania vyeo.................ipo na inakolea.................................
Ingelikuwa ni Chadema imekumbwa na vurugu hizo ungeliyasikia magazeti ya CCM na serikali kama vile Uhuru, Habari leo, Daily News yakiona hicho ni kivuno cha kuuza magazeti..................................................
Nyufa hizi za kugombania vyeo ndani ya CCM ndizo baadaye zitaamua hatma ya Chama hiki kama kweli ni cha mkulima na mfanyakazi au watajwa hawa hutumiwa tu kama ni mtaji wa kisiasa......................
Kumbuka mwenye RAI ndiye anayejua nai kiongozi dhaifu na yupi si dhaifu , mwacheni atengeneze baraza bila kuingiliwa