Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,378
- 39,319
MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA BARAZA LA MAWAZIRI 2010- NA SABABU ZAKE
Na. M. M. Mwanakijiji
Ni mara chache sana katika kipindi cha utawala tunaweza kupata nafasi ya kutoa mawazo juu ya muundo wa Baraza la Mawaziri. Hakuna wakati mzuri wa kufanya hivyo kama kufuatia uchaguzi mkuu kwani ni wakati huu ndipo mwelekeo wa serikali unaonekana. Wakati mbaya ni wakati ambapo baraza jipya linaundwa katikati ya vipindi vya uchaguzi kufuatia kujiuzulu, kifo cha Waziri Mkuu au kuvunjwa na Rais.
Baraza la Mawaziri ndilo hutoa dalili ya mwelekeo wa serikali inayoingia madarakani. Ilani ya Uchaguzi ya chama na kampeni za siasa ni kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi na baada ya kuchaguliwa chama kilichoshinda hujiandaa kushika madaraka na baada ya taratibu zote za kurasimisha ubunge kukamilika kinachosubiriwa ni kuundwa kwa Baraza la Mawaziri a.k.a Serikali. Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha ushauri kwa Rais na usimamizi wa serikali. Hivyo, kwa kuangalia Baraza lilivyo unaweza kupata picha ya nini kitafanywa na serikali inayokuja. Hakuna haja ya kusikiliza hotuba, kuangalia maneno, semina bali kuangalia baraza limepangwaje ili kutekeleza ilani ya uchaguzi na pili nani anaingia kwenye bara hilo. Timu inaweza kuwa na jina kubwa, bajeti kubwa na kocha mzuri; hata hivyo kazi ipo katika wachezaji wake na mfumo na mikakati yao ya ushindi.
Mapendekezo haya ninayatoa yakiakisi mwelekeo wa serikali ya CCM na Ilani yake. Endapo Dr. Slaa angetangazwa mshindi basi ningetoa mapendekezo yenye kuakisi mabadiliko makubwa ya kimfumo ambacho Chadema ilikuwa imeyaahidi. Kwa vile ajenda ya CCM haikuwa inalenga mabadiliko makubwa ya kimfumo wa utawala mapendekezo yangu basi yameegemea katika mambo makubwa manne tu:
Kupunguza ukubwa wa serikali (lean government)
Kupanga wizara kwa mantiki ya utendaji wake (logical flow of operation)
Kurahisisha mtiririko wa utendaji (streamlining performance)
Kulenga ufanisi wa matokeo kuliko mchakato (result oriented government)
Mapendekezo haya pia yamezingatia mfumo wa baraza la mawaziri ya baadhi ya nchi zinazoendelea na hata zilizoendelea ambazo zimefanya mageuzi makubwa ya mifumo yao ya utawala na kujiweka katika nafasi za kufanikiwa. Nchi ambazo nimepitia mabaraza yake ni:
Indonesia
Korea ya Kusini
Namibia
Botswana
Afrika ya Kusini
Canada
Marekani
Kwa ujumla nimeweza kufikia wizara 23. Kati ya hizi wizara 19 ziko wizara kamili nje za ofisi za Rais, Makamu na Waziri Mkuu. Ina maana ofisi hizo za kiutendaji zinabakia na wizara nne tu au tatu kutegemea na wapi Wizara ya Utumishi wa Umma itawekwa. Kati ya wizara hizo 23 ni saba tu zitakuwa na Manaibu Waziri.
Ninazigawa wizara hizi katika makundi makubwa matano kulingana na mwelekeo wa majukumu yao. Mgawanyo huu hauchori mipaka isiyovukika kati ya wizara na wizara (nyingi zinaingiliana) bali ni mgawanyo wa kuzielewa tu na kuziwezesha kuonekana vizuri katika mwelekeo wa utendaji wake. Ni sawasawa na jinsi wachezaji wa soka wanvyojipanga uwanjani wakati wa mpira kuanza huku kila mmoja akionekana vizuri katika nafasi yake lakini wakianza kucheza tunaweza kuwaona wanavyohusiana, kupishana, kusaidiana na hatimaye kuweza kuleta ushindi.
Wizara za Usalama na Ulinzi
Wizara za Kijamii na Maisha
Wizara za Mambo ya Uchumi na Uzalishaji Mali
Wizara za Utawala na Uwajibikaji
Wizara za Nchi
Katika makala ya mapendekezo ambayo nimeambatanisha hapa nimechangua sababu za kwanini wizara fulani iwe au iko mahali fulani. Hivyo, kabla ya kukosoa nashauri mtu apitie makala hiyo ili kidogo awe ameingia kichwani mwangu kuelewa the reasoning behind ili mtakaponikosoa mnikosoe kwa haki. Kauli ya "mwanakijiji mimi sijasoma makala yako lakini.." ni dalili ya kuwa presumptuous. So, nashauri take time to read halafu kosoa, halafu tujadiliane kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumegonganisha vichwa (brain storming) na kutoa mchango hata usiozingatiwa au kukubaliwa wa serikali tunayoona itafaa.
WIZARA ZOTE

- Wizara ya Ulinzi na JKT - Ministry of Defense & National Service
- Wizara ya Mambo ya Ndani, Uhamiaji na Vikosi vya Uokoaji - Ministry of Home Affairs, Immigration and Rescue Forces
- Wizara ya Usalama wa Taifa- Ministry of National Security
- Wizara ya Afya - Ministry of Health
- Wizara ya Elimu - Ministry of Education
- Wizara ya Maendeleo ya Jamii - Ministry of Community Development
- Wizara ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia - Ministry of Science and Technological Development
- Wizara ya Ardhi, Nyumba Vijijini na Maendeleo ya Miji - Ministry of Land, Rural Housing and Urban Development
- Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ministry of Culture, Arts and Sports
- Wizara ya Fedha na Uchumi - Ministry of Finance and Economic Affairs
- Wizara ya Biashara, Viwanda, Masoko, na Uwekezaji - Ministry of Trade, Industry and Investments
- Wizara ya Nishati na Raslimali za Mafuta - Ministry of Energy and Oil Resources
- Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu - Ministry of Infrastructure Development
- Wizara ya Mazingira, Utalii na Uhifadhi wa Wanyama Pori - Ministry of Environment, Tourism and Wildlife Conservation
- Wizara ya Madini - Ministry of Mining
- Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries
- Wizara ya Maji na Usalama wa Chakula - Ministry of Water Resources and Food Security
- Wizara ya Mambo ya Nje - Ministry of Foreign Affairs
- Wizara ya Haki na Usimamizi wa Sheria - Ministry of Justice and Law
- Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala - Ministry of Public Service and Administration
- Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Masuala ya Muungano - Ministry of State Vice President's Office - Union Affairs
- Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa - Ministry of State Local Governments and Regional Administrations
- Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Masuala ya Bunge.