Niko tayari kujifunza mambo ya sheria - Ulega

Niko tayari kujifunza mambo ya sheria - Ulega

Nuel27

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2026
Posts
419
Reaction score
823
Kwani hii nchi tumerogwa na nani wakuu? Hivi unaweza kusomea udobi halafu ukaajairiwa kama Daktari?
Kwamba wabunge wote hakuna hata mmoja mwenye ujuzi na sheria apewe wizara?

Haya bwana
448471.jpg
Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega amesema yuko tayari kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu wizara hiyo na sekta ya sheria kwa ujumla ili kuhakikisha majukumu ya wizara hiyo yanabebwa na watendaji kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Dkt. Juma Homera kufuatia Mabadiliko wadogo ya Baraza la mawaziri yaliyofanywa Septemba 27, 2026 Ulega pia ameahidi kushirikiana kwa karibu na viongozi wa wizara hiyo.

“Mimi niko tayari kujifunza mambo mbalimbali kuhusu wizara hii na sekta ya sheria kwa ujumla pia kushirikiana na watumishi na viongozi ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa weledi na ubora na hatimaye kufikia malengo yaliyowekwa” amesema Ulega.

Pia Waziri Ulega amehimiza utekelezwaji wa majukumu ya wizara hiyo kwa weledi na kwa wakati na kusisitiza kuwa hatarajii kuona hali ya uzembe kazini.

Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba mosi, 2026 katika ofisi za wizara Mtumba Jijini Dodoma, na kushuhudiwa na viongozi wengine wa wizara akiwemo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba, Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Baraka Luvanda pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo vya wizara.��

Mhariri @moseskwindi
448470.jpg
 
Wanasema katibu mkuu wa wizara ndiyo mtaalamu wa mambo ya wizara yake, waziri ni mwanasiasa tu wa wizara hiyo hata kama haujui na hajasomea mambo yanayohusu wizara yake. Kimsingi inatakiwa kila waziri awe na ujuzi wa mambo ya wizara yake
 
Naam
 
Kuna managerial post (uwe unajua kuongoza na si lazima uwe mtaalam wa sekta husika) na technical posts (ambapo unakuwa na utaalam wa sekta husika). UWaziri, Ukatibu mkuu ni Managerial posts. Directors katika wizara ndiyo technical posts kwenda chini.
 
Amesomea mambo ya matawi kapelekwa kwenye sheria nchi hii aliyeturoga alifariki na hata kaburi lake halijulikani liko wapi.
 
Back
Top Bottom