SoC01 Mapendekezo ili Kupunguza vitendo vya unyanyasaji kwa wadada wa kazi za ndani (House Girls)

Stories of Change - 2021 Competition

Anita Makirita

JF-Expert Member
Jul 16, 2021
1,125
1,823
Habari wanajukwaa

Tumeskia vitendo vya kuogofya vya wadada wa ndani, kuumiza hadi kuua Watoto, ushirikina n.k. Ila pia Kumekua na Habari nyingi za vitendo vya unyanyasaji vya wafanya kazi wa ndani, wengi wanapewa kazi nyingi, maslahi hafifu, kupewa mimba na ma boss wao kisha kukataliwa hizo mimba nakadhalika, wengi hawajui wafanye nini, wamuone nani wa kumuelezea masahibu yao,wengine wanaishia kuua Watoto wa Waajiri wao sababu ya chuki ambayo imeachwa ndani ikakua kwa muda mrefu.

Leo nimeona ni vyema tuongelee kuhusu manyanyaso ya wadada wa nyumbani, nimechagua hii topic sababu wadada wa kazi ni wasichana ambao wako kwenye mazingira hatarishi zaidi, (vulnerable) kingono, kupigwa, kufanyishwa kazi kwa muda mrefu n.k..huwezi kusikia kijana wa kiume akiwa ananyanyswa kwenye eneo lake la kazi ila habari ni nyingi za wadada wa kazi kunyanyaswa na nyingine zinaibuka kila leo.

Binafsi napenda kupendekeza wizara ya Afya, Jinsia na Watoto ipanue kazi zake ijumuishe kazi ya kusaidia wadada wa nyumbani, kuhakikisha wanaishi bila hofu ya kunyanyaswa, wanapata maslahi yao n.k.

Ndio, Wizara ipo wazi kwa wanawake wenye malalamiko yao kwenda ustawi wa jamii lakini imekua ikipokea zaidii na kufanyia kazi maswala ya wanawake kutekelezwa na wanaume zao, utambuzi wa mtoto, mambo ya mirathi,nk kuna kundi kubwa la wasichana wa ndani ambalo limesahaulika na jamii/jamhuri na halijui pa kwenda kukiwa na matatizo.

Ni muda wa kufanya mabadiliko, Wasichana wa kazi hawapaswi kuishi kama hawapo, kama invisible beings. Hatua ya kwanza ambayo ningependa kuishauri serikali ,ni kujua ama kutambua uwepo wao. Ingekua vyema kuungekuwa na dawati ndani ya wizara linaloandikisha rekodi za wadada WOTE wa nyumbani.

Kwa mfano umri wa dada,mahali anapotoka,maelezo ya wadhamini wake,historia yake ya kazi alizowahi kufanya, picha n.k. hii itasaidia kujua mdada gani yupo mahali gani.

Hii ni nzuri ku ‘trace’ mdada yeyote mwenye tatizo lolote. Kwa mfano baadhi ya wadada hunyanyaswa na kufukuzwa ama kuumizwa na wakienda kupata msaada wa kisheria Muajiri anakana hata kumtambua huyo mdada, hivyo kukiwa na database inayoonyesha kila kitu hadi uwepo wa mdada wa kazi kwenye nyumba husika itakuwa rahisi kwenye kusuluhisha malalamishi na kusaidia kama malalamishi yataenda kwenye mkono wa sheria.

Ila pia kukiwa na hio ‘data base’ waajiri pia watamchukulia mdada kama mtu anayetambulika na Jamhuri hivyo watamheshimu na kuishi nae kwa utu, tofauti na sasa ambapo mdada ananyanyaswa kisa hakuna anayemtambua au hakuna mtu wa kuongea nae Zaidi ya familia aliyoajiriwa.

Hizi information/database za kuhusu wadada zinatakiwa kuwa ’updated’ kila baada ya muda, mfano mwaka mmoja. Mdada anaenda kila mwaka mmoja kuandikisha wizarani.Hii itasaidia kujua kama information za awali bado zinahusika/relevant ama zimebadilika na cha muhimu Zaidi ni kufunua matatizo yoyote ambayo yatakua labda yametokea ndani ya mwaka huo mmoja.

Ningependekeza pia kuwe na Sheria ya kuzuia Muajiri yeyote kutoajiri mdada wa kazi ambae hatambuliki na Jamhuri. Sijui mnaonaje ila nadhani kukiwa na huu utaratibu ,moja kwanza;, Waajiri watakua na’confidence’ mtu waayemuajiri anatambulika na Jamuhuri,na wanaweza kumfuatilia na kumpata kukiwa na matatizo, Ila la muhimu Zaidi ni kuwa hawa waajiri watafuata sheria ili wasiingie hatiani ,hivyo vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wadada kupungua.

Pia wizarani kuwe na ‘Advocacy Services’ hii ni huduma ya kumpa nafasi mdada wa kazi kuwa na mtu ambae atakua mtetezi au sauti yake, amsaidie kuongea kwa niaba yake kama anaona ugumu wa kufanya hivyo kwa mfano kwenye situation amefadhaika sana/traumatised. Ama Amuone nani kwa ushauri Zaidi juu ya jambo lake, Advocates wanakua watu wa ushauri wa kumsaidia dada aende kwenye mashirika husika,na pia wanaweza kuwa wawakilishi kuhakikisha wadada wanapewa haki zao.

Nakaribisha Mawazo zaidi juu ya nini tufanye kupunguza vitendo vya unyanyasaji vya wadada wa kazi??
 
Wazo zuri ila gumu kutekelezeka sababu, wengi wao hawatokei kwenye makapuni bali ni unaletewa kutoka popote pale...
 
Wazo zuri ila gumu kutekelezeka sababu, wengi wao hawatokei kwenye makapuni bali ni unaletewa kutoka popote pale...
Asante mkuu,ila ikiwekwa sheria hakuna muajiri kuajiri mdada wa kazi asiyetambulika na jamuhuri itasaidia kupunguza tatizo
 
Back
Top Bottom