#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

Ficha ujinga wako. Mwaka jana Magufuli alitangaza corona imeisha akapewa na ''kombe'' la ushindi kwa kuishinda corona. Kila mtu akamsifia (wajinga ofcourse ) na wengine wakasema wakawa wana-mock njia zinazochukuwa hatua au watu wanaokufa. Matokeo yake kuanzia mwaka jana mwezi wa 12 mpaka wa tatu corona ikarudi kwa kasi na vifo vikaondoka na watu wengi. Sasa wewe unarudia tena kosa lile lile. Hivi unajua hata India walikuwa wanasema corona imeshapita? Corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya sana lakini watu wanapoanza kuugua na kufa inakuwa ni kishindo kikuu. Hata Tanzania sasa hivi haiko salama na inaweza kurudi tena tena hali ikawa mbaya mpaka kila mtu akashangaa.
 
India ambao wanatengeneza hizo chanjo wanakufa kama kuku wa kideli, pamoja na kutokufuata mashariti yeyote ya WHO bado tunadunda maisha yanaendelea kama kawaida,wacha kutisha watu, mbona Kenya walio nunua vaccines mbona maambukizi yanaendelea? vaccines zenyewe zina effect mataifa mengi yameanza kuzikataa nyinyi mnataka ziletwe huku.
 
Corona ni changamoto sema wabongo toka walivyoambiwa ishu ya nyungu kila siku wanaona mzaha tuu ila hiyo ishu ni hatari mno kuliko maelezo...
Kuna dakatari kafa Kenya kwa korona. Na yeye kama Magufuli alikuwa anaidharau na kusema nyungu inatosha.
 
Kwahio data za maelfu ya watu waloambukizwa au kufa baada ya kuhudhuria shughuli za msiba wa kitaifa zafichwa?

Na pia data za maelfu ya watu walohudhuria leo sherehe za Mei Mosi ambao watakuwa wameambukizwa baada ya wiki moja nazo zitafichwa?
 
ACHENI KUTISHANA.
UGONJWA upo Huku India kuumwa mnaumwa nyie wa Huku bongo.
Kila MTU apambane na Hali yake
 
Sijaona dhamira ya Mh. Rais maana tangu ameongea kupata washauri amekaa kimya.
Huu ugonjwa sio wa kuundia tume bali unahitaji action.
Na kuonyesha hayuko serious bado maabara ya kupima covid wana fanya biashara na sample za wagonjwa. Huwezi niambia kupima sample ya covid ni 230,000/ wakati majirani zetu wana pima kwa 20,000/
Pia hii ina tunyima watalii maana ukiwaambia kupima covud ni 230,000/ wanasema ni ghali sana na wana ghairisha safari na kwenda nchi nyingine.
Waziri wa afya kakaa kimya tuu hana tamko????
 
Kwahio data za maelfu ya watu waloambukizwa au kufa baada ya kuhudhuria shughuli za msiba wa kitaifa zafichwa?

Na pia data za maelfu ya watu walohudhuria leo sherehe za Mei Mosi ambao watakuwa wameambukizwa baada ya wiki moja nazo zitafichwa?
Mikutano ilikuwa nje. Mwendo wa hewa inapunguza kuongezeka kwa pumzi lenye virusi mahali pamoja. Sitegemei vifo vya maelfu. Makumi hakika. Nategemea zaidi kuona mavuno ya futari za Ramadan.

Kuficha: hadi hospitali haziruhusiwi kupima wenyewe (hospitali kubwa zinaweza) hatuoni data. Wewe uite hali hii "kutuliza umma", mimi nasema "kuficha".
 
Si Tanzania tu, nchi nyingi walidhani Corona imeisha na wakalegeza lockdowns.

Baadae wakawa na second lockdown na wengine wamekuwa kwenye third lockdown.

Lockdowns zimewashinda nchi nyingi tu na leo wote wanafikiria kuweka masharti ya kuondoka kwenye hiyo kitu.

India wamefeli wapi ndugu?
 
Mikutano ilikuwa nje. Mwendo wa hewa inapunguza kuongezeka kwa pumzi lenye virusi mahali pamoja. Sitegemei vifo vya maelfu. Makumi hakika. Nategemea zaidi kuona mavuno ya futari za Ramadan.
Lakini India pia walifanya mikutano ya kisiasa nje na pia kuoga maji ya mto Ganges kwenye tamasha la kutambika la Kumbh Mela.

Leo hii watu milioni 19.1 wameambukizwa na zaidi ya 200000 wamekufa.

Yote hayo si yalifanywa nje au ?
 
Kufa Ni mara moja. Jikinge na uwapendao
 
Kuna dakatari kafa Kenya kwa korona. Na yeye kama Magufuli alikuwa anaidharau na kusema nyungu inatosha.
Daah huku usipovaa barakoa unaweza kwenda jela mpaka kesho kuingia duka lolote lazima unapewa sanitizer inasaidia sana sana na mambo ya social distance yanasaidia mno na viwanjani washabiki hawaendi ila bongo kila kitu wanachukulia poa tuu..
 
Hii tume ya Corona kama imeundwa na zinafanya kazi, basi ina lengo la kuona Mpango anachukua hatamu za serikali hivi karibuni.

Mama akili za kuambiwa hajachanganya na za kwake?
 
Mbona unadandia bila hata kujua gari linakoenda? Kuweka Lockdown na kulegeza hilo jambo haliepukiki. Na hasa ndiyo njia ya ku deal na corona. Ni vizuri ujue kuwa walikuwa wanajua kabisa corona haijaisha na itarudi tena lakini kila inapopungua masharti yanalegezwa. Kitu ambacho umekwepa kusema ni kuwa pamoja na nchi hizo kulegeza masharti lakini bado kulikuwa hakuna mikusanyiko ya watu wengi na ni baadhi ya masharti tu yalilegezwa. India waliamua kujimwaga kama kila kitu kipo sawa na kukawa na mikusanyiko mikubwa ya kampeni na ya kidini.
 
Nakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia Magu na sera zake za porini za covid. Uliwazodoa sana CHADEMA walipokuwa wanasisitiza standard measures ambazo umezigusia. Nini kimebadilika mkuu? Si ingefaa sera za nyingi ziendelee?
Hata Magu alipowazodoa wanaovaa Barakoa na kutamba kwamba yeye na wasaidizi wake, mkaona ni poa tu. Vipi tena?
 
Daah huku usipovaa barakoa unaweza kwenda jela mpaka kesho kuingia duka lolote lazima unapewa sanitizer inasaidia sana sana na mambo ya social distance yanasaidia mno na viwanjani washabiki hawaendi ila bongo kila kitu wanachukulia poa tuu..
Wabongo namna tuna laana ya aina fulani. Ila uzuri (japo inasikitisha) ni kuwa yule aliyekuwa analisha watu ujinga wa nyungu alishindwa kuitumia hiyo nyungu alipougua.
 
Nimedandia na comment namba 110 hapo juu.

Hivyo naelewa mwenendo wa mada.
 
Ahahahah, na wewe unaijua tabia ya korona tayari. Eti "unajua corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya".

Nimekuelewa virologist MWEREVU.
 
Ahahahah, na wewe unaijua tabia ya korona tayari. Eti "unajua corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya".

Nimekuelewa virologist MWEREVU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…