Maoni yangu kuhusu Meru Residential Appartments

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Kweli uzee waweza kuwa kitu kibaya sana kwa sababu kila kukicha unapata mshtuko wa moyo kwa mambo yanavyoendelea duniani na haswa nchini mwetu!

Ni Tanzania hii hii ambayo kuna baadhi ya wajukuu zangu wanadumaa kwa kushindia muhogo na chai kila siku inayoenda kwa mungu lakini ndani ya nchi hii hii kuna watu wanamiliki magari ya kifahari na makasri kuliko walivyokuwa wakoloni wetu wajerumani.

Sitaki kupiga porojo sana lakini ninashangazwa sana na siamini kama kuna watanzania wenye uwezo wa kununua au sijui nisema kukodisha hizi nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba la Taifa (NHC) maarufu kama Meru Residential Apartments. Sielewi nyumba hizi zimejengwa kwa ajili ya watanzania wenye kipato cha namna gani. Naomba mwenye ufafanuzi anisaidie jamani. Mbona kama shirika hii linakomoa watanzania na kuwarudisha utumwani? Naona huruma sana kwa kizazi kitakachokuja miaka 50 baadae!

Ili uweze kutoa maoni zaidi hebu bofya www.nhctz.com/meru/
 
175 milioni kaka sijui ni mtanzania yupi wanayemtaka anunue hizi nyumba.....
nashukuru umesoma na wewe,mimi nildhani macho yangu mabovu.au ndio tuseme hii ni awamu ya mafisadi halafu watajenga za kina sisi kajambanani.
 
Katika Capitalist society lazima kutakuwa na tofauti za kipato na tofauti za mahitaji sidhani kama watakosa wateja.
kwa hiyo ni wazi tumeingia kwenye capitalism?lakini tumebadilisha katiba yetu au tumewaandaje watanzania kuingia huko au ndo tunarudishana utumwani kidogokidogo?hata mimi sidhani kama watakosa wateja lakini sina uhakika kama wateja watakuwa ni watanzania.sana sana wazungu wenyewe au wazungu kupitia majina ya watanzania wenye tamaa.
 
hii inahitaji ufafanuzi.tunajenga nyumba kwa maslahi ya watanzania ambao ni maskini au wawekezeji kutoka nje?hivi wanaopanga mipango ni watanzania au wangereza?this is so sad!
 
kwa hiyo ni wazi tumeingia kwenye capitalism?lakini tumebadilisha katiba yetu au tumewaandaje watanzania kuingia huko au ndo tunarudishana utumwani kidogokidogo?hata mimi sidhani kama watakosa wateja lakini sina uhakika kama wateja watakuwa ni watanzania.sana sana wazungu wenyewe au wazungu kupitia majina ya watanzania wenye tamaa.

Kwa hiyo wewe haujui kuwa Tanzania tunafuata capitalist system? Sina uhakika kama kuna kitu gani unataka kibadilishwe kwenye katiba. Mimi nadhani kuna watanzania wanaweza kuaford hizo nyumba kama watanzania tatazinunua ni swali lingine.
 
hivi katiba yetu inasema tanzania ni nchi ya kibepari?
 
Pengine inabidi tujiulize...........madhumuni hasa ya kuanzisha shirika la nyumba la Taifa yalikuwa ni nini hasa...........zile nyumba za Ilala, Temeke, Kinondoni, Mwananyamala, Ubungo na mikoani zilijengwaje na kwa madhumuni gani?......je madhumni hayo bado yapo?
 
Hawa NHC wameshindwa kujiuliza maswali ya msingi. Milioni 175(ninajua ni mkopo) inatosha kununua kiwanja cha acre moja.Kujenga nyumba yenye swimming poll na bado utabakiwa sehemu kubwa ya watoto kucheza, kujenga mabanda ya mifugo, store kubwa ya kuhifadhi vikorokoro vya aina zote na usafi wa mazingira una control wewe mwenyewe.Kwenye three bedrooms apartment vyote hivyo huwezi kuvipata na baya zaidi ukiwa na neighbour from hell imekula kwako.
 
mjukuu wangu ndio maana najiuliza hii mipango huwa tunapanga au tunapangiwa?mara nyingi tunasubiri mambo yaende mrama halafu ndio tunagutuka kutoka usingizini na kuanza kulaumiana.Tanzania kuna tatizo kubwa sana,sijui tuanzie wapi kulikabili.
 
Back
Top Bottom