SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
KUKARIBISHWA MAOMBIYA KUNUNUA NYUMBA 30 ZILIZOKO MJINI ARUSHA
Shirika la Nyumba la Taifa linawakaribisha watanzaniawakazi na wasio wakazi kuleta maombi yakununua nyumba zake zilizojengwa mjini Arusha. Nyumba hizo ambazo zinaitwa MeruResidential Apartments zinatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu (siku 90)kuanzia tarehe 1 Oktoba,2011.MRADI WENYEWE:Meru Residential Apartments zimejengwakwenye mandhari murua inayokupatia maisha bora katika jamii yenye usalama.Zimepewa jina hilo kama ishara ya kuuenzi Mlima wa Meru ambao ni mlima wenyeVolcano hai nchini Tanzania wenye urefu wa mita 4,566 (futi 14,980), ukiwa nimlima wa kumi kwa urefu barani Afrika.MAHALI ZILIPO:Meru Residential Apartments ziko mjiniArusha kwenye eneo la katikati kabisa, kwenye mtaa wa Wachaga, Kiwanja Na. 565/I. Eneo hilo likoumbali usiozidi kilomita mbili toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ukumbi wa mikutanowa Kimataifa wa Arusha (AICC), nyumba hizo zimepakana na hospitali ya Selian naChuo cha Ufundi, na kwa upande wa mashariki inakupatia muonekano mzuri wa MlimaMeru.MAELEZO YA NYUMBAHIZO.[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Idadi ya Nyumba [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
30 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Ukubwa eneo la nyumba [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
169.45 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Idadi ya Majengo [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
2 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Idadi ya ghorofa kwa kila jingo [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
Ghorofa nne [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Idadi ya vyumba kwa kila nyumba [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
3 (kimoja kinajitegemea) [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 235, bgcolor: transparent"]
Sifa nyingine za nyumba hizo [/TD]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
Sebule kubwa, chumba cha kulia, jiko,stoo,bafu na choo [ Nyumba zinauzwa bila samani (furniture)] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 300, bgcolor: transparent"]
Kila nyumba ina maegesho maalum ya gari, pamoja na tanki la maji la lita 1000. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
BEI ZA NYUMBA HIZO:Bei ya chini kabisa ya kila nyumba nishilingi za Kitanzania 175,314,366.48 bilakujumlisha kodi ya ongezeko la thamani. Mwombaji atakayetoa bei ya juu zaidi nakutimiza masharti yote yaliyoelezwa hapo chini ana nafasi kubwa zaidi yakuuziwa.TARATIBU ZA KUOMBA:Waombaji wanatakiwakuzingatia utaratibu ufuatao:1. Wanaopenda kununua nyumbawachukue fomu za maombi kutoka Makao Makuu ya Shirika, kwenye ofisi za Shirikazilizopo Arusha, au kwenye ofisi yoyote iliyo karibu nao. Fomu zinapatikana piakwenye tovuti wa Shirika (www.nhctz.com). 2. Fomu za kuomba kununua zijazwe nakuwekwa saini na kurejeshwa kwenye ofisi za Shirika pamoja na barua yakuonyesha kiasi ambacho mwombaji yuko tayari kulipa. Shirika litahitaji pia ushahidiwa malipo ya shilingi 10,000/=(Malipo yasiyorejeshwa) kama ada ya maombi namalipo ya asilimia kumi (10%) ya awali zilizolipwa kupitia benki kulingana nathamani ya nyumba uliyochagua. 3. Waombaji wote waliofanikiwawataandikiwa barua kujulishwa hivyo. Watapewa siku 90 toka tarehe ya barua hiyokukamilisha malipo ya asilimia tisini (90%) iliyosalia kulipia nyumba husika.Utaratibu wa kulipa unaweza kuthibitishwa kwa kulipa pesa kwenye akaunti yamradi au kuonyesha hati ya mkopo toka benki. 4. Kama uthibitisho wa malipohautawasilishwandani ya siku 90, mnunuzi atanyanganywa na nyumba hiyo kuuziwamtu mwingine toka kwenye orodha ya waombaji. Mnunuzi aliyeshindwa kulipa hiyoasilimia tisini (90%) ataruhusiwa kutumia asilimia kumi (10%) ya awali kulipianyumba kwenye mradi mwingine. Aweza pia kurejeshewa fedha zake kwa kukatwaasilimia mbili (2%) ya kiasi hicho. 5. Mwisho wa kuwasilisha maombi niJumatano tarehe 4 November, 2011 saa4:00 asubuhi. 6. Maombi yapelekwe ndani ya bahashayenye rangi ya hudhurungi/kahawia iliyoandikwa juu;Maombi ya Kununua Nyumba za Meru-Arusha. 7. Maombi yote yapelekwe kwa: Meneja wa Mkoa, Shirika la Nyumba la Taifa,S. L. P 883, ARUSHA