Maoni yangu: Benedict Wakulyamba amrithi IGP Sirro

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Salamu kwenu wadau!!!

Nchi yetu kupitia jeshi la polisi imeingia dosari kubwa baada ya polisi kuhussishwa na mauaji mengi ya RAIA nchini, hii nikutokana na aidha majukumu yao au ni ishara ya kuhitaji uongozi mwingine mpya. Au bahati mbaya yawezekana.

Rejea maujaji ya Mtwara ya mfanyabiashara, Mbeya kijana wa airport ya zamani Alifia cello, Mara n.k

Lakini pia wananchi wamepunguza imani na jeshi la polisi huku kukiwa na wananchi kuchukuwa sheria mkononi kwa kusema akienda polisi anatoka kesho.

Mawazo yangu sasa ni kwamba uongozi wa juu pasi na shaka umechoka nikimaanisha kiongozi mkuu, na hii alipaswa kujiudhuri au Ku step down kwa hali ya mambo yanavyoendelea kwa ustawi wa nchi na jeshi letu LA polisi.

Siro anakribia kustaafu nafikiri ndo maana wanamvumilia lakini kama amebakiza miaka 2 Au 3 anaweza kustaafishwa tu kwa hiari. Kamanda amechoka amefanya kazi kubwa saaana, yatosha.

Napenda kupendekeza KWA MAMLAKA HUSIKA KUWA MBADALA WA IGP SIRRO AWE BENEDICT WAKULYAMBA KWA SASA NI KAMISHINA WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU UTAWALA DODOMA huyu Afande anafaa pia hata elimu yake ni ya juu ana masters Uganda, bachelor Udsm,Postgraduate chuo cha UONGOZI Institute ALIWAHI KUWA RPC TANGA

NI MTULIVU NA NI MKWELI ANA HOFU YA MUNGU

Huyu anafaa KUWA kiongozi mkuu WA polisi IGP MPYA

images (1).jpeg


images (2).jpeg
 
Ni mapendekezo tu ila tunahitaji mabadiliko
Mama hapangiwi.

Nyie makostable sijui makoplo acheni kumpangia mama cha kufanya.

"Ungejisikiaje; mmmh! Kama wewe ndiye ajipii halafu watu wanapiga jeramba huku wa kukurithi, ungejisikiaje. Wazazi msituletee watoto kama hawa"(alisikika mkuu mmoja)
 
Tunataka IGP mwanamke! Tena itapendeza aikitoka visiwani na sio bara.

Kuna jambo nimekumbuka, iliwahi kutokea RPC mmoja akauawa ili asiteuliwe kuwa IGP, angalia msije kuuana maana historian hujirudia!
Unamaanisha Suzan..??
R.i.P kamanda Barlow
 
NI MTULIVU NA NI MKWELI ANA HOFU YA MUNGU
Kamanda Siro ni mseminari kabisa lkn kafanya nn? Hata huyu hatofanya kitu cha maana zaidi ya kutumiwa na kutumika kisiasa.

Hata aje malaika kuwa IGP kama katiba itendelea kuwa hii hii sahau kuhusu ubora wa polisi
 
Bi. Mikopo anawaza kujaza wazanzibari kila mahali we unaleta habari za watanganyika wagalatia
 
Mkuu unapaswa kutambua hesabu ziendanazo na majira na nyakati za sasa. Kuna kila dalili za Awadh Juma kuwa ndiye ambaye ni chaguo sahihi.
 
Back
Top Bottom