MAONI: Shule za kata zifikiriwe upya

kweli kabisa kuna watu wanaenda mjengoni sijui ni kwanguvu za giza ama ni nini. Maana hata komba juzi kajitetea kwamba hajalala bungeni ila alikua anakemea
 
CCM oyeee!!! Division four oyeee na waliopata zero(sio division) oyeeee
Kata oyeee:A S 20::clap2:
 
Shule za kata ilikuwa ni move yao, hakuna siku wataipinga au kukubali failure hadharani!!
 
Nimekaa na kuwaza sana hasa matokeo ya Form four 2010 yaliyopita.Shele nyingi za kata zaidi ya 70 ya wanafunzi walilamba zero na hawapati cheti.Viongozi wa kisiasa wanasema ni mafanikia,ila simjui mtoto hata mmoja wa kigogo anayesoma shule ya kata.Hii ikiwa na maana watoto wa vigogo huenda shule za academia na wa maskini ndio waende shule za kata.Baada ya miaka 5 watoto wote wa vigogo ndio watakua wameshika uchumi na nafasi za juu..Kama kweli shule za kata ni nzuri hebu nitajie ni mtoto wa kigogo yupi anasoma shule ya kata?Maskini tumeisha,ili wananchi waelimike ni lazima kuwapa elimuu.Kwa nini shule hizo zisifutwe kabisa?
 
Ni kweli shule hizi ziko chini ya viwango kutokana na kukosekana kwa miundombinu muhimu lakini pia kukosa rasilimali watu (waalimu na watenda kazi wengine).

Kuendelea kuziendesha katika hali hii ni kujenga kaburi la kitaaluma la vizazi vya sasa na vijavyo katika taifa letu....

Hata hivyo, bado ukweli unabaki pale pale kwamba nchi yetu inazihitaji sana kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto wetu.

Tunachopaswa kufanya sio kuzifuta au kuzivunja bali kushikamana kuzijengea uwezo na kuitaka serikali isimamie mpaka ziwe zimekamilika na kuwa na mazingira ya kufaa kusomea.

Ambacho mimi ningeshauri ni kufungwa kwa shule zote za kata ambazo hazijajitosheleza katika kutoa elimu ya sekondari sawasawa na viwango vilivyo. Kwa mfano, vituo vyote vya afya ambavyo viko chini ya viwango vinafungwa mpaka vitakapojitosheleza kimiundo mbinu na rasilimali kisha huomba tena kibali ili kuviendesha kwa upya.

Ninauhakika hali ya shule zetu za kata kama ingekuwa ni shule binafsi siku nyingi serikali ingefunga na kutoa tamko mpaka vijitosheleze....Nadhani umefika wakati ichukue hatua hii kabla haijatuumizia vizazi vyetu zaidi

ZISIFUTWE, BALI ZIFUNGWE MPAKA ZIJITOSHELEZE na wananchi tushike bango serikali kufanya hivyo maana hazina maana kuwepo wakati hazina miundombinu na rasilimali watu

Nawakilisha
 
zikifutwa watoto watasoma wapi? Waende mtaani au wote waje dar kutafuta kazi? Badala ya kusema ziboreshwe wewe unataka zifutwe tena ? Nzmna gani ndugu yangu.
 
Shule hizi zisifutwe. Tujaribu kuangalia faida zake baada ya miaka kadhaa ijayo. Uwepo wake utawafanya wanajamii husika pamoja na serikali kuwajibika. Walimu na vitendea kazi vimekuwa vikiongezeka japo si kwa kasi sana, ila ni swala la muda na jitihada kwa wadau wote.

Wanafunzi wengi wa sasa ni vilaza na hawajali. Jaribu kutizama hata kwa shule zilizokuwa zikisifika awali zi wapi sasa. Katika mazingira ya mjini kwenye vyombo vingi vya habari mwanafunzi anashindwa kumjua hata waziri mkuu!
Wanafunzi wamekuwa walevi, wahuni na wazazi wengi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao wakidhani ni kazi ya walimu peke yao.
Ni bora ndege mmoja mkoni kuliko wengi msituni.
Shule za kata zisifutwe.
Nami nawasilisha.
 
Babkey unafahamu Wizara ya afya huendesha opresheni na kufungia vituo vyote vya aftya ambavyo havikidhi vigezo ili kuokoa maisha ya watu wanaopatya huduma hapo?

Unadhani haifai pia hatua kama hii ikachukuliwa kwa shule hizi za kata kufungiwa mpaka pale shule inapokidhi vigezo (sio kwa serikali kufanya hivyo peke yake bali na wananchi kushiriki) ili kuokoa vijana kutokuwa mambumbumbu zaidi?

Mwaka jana 80% wamefeli, mwaka huu sitazamii tofauti, na mwakani na labda baada ya miaka hiyo kadhaa ya kupima, je huoni ni wengi tutakuwa tumewaua kitaaluma?

Kwa nini zisifungiwe kwa muda (SIO ZIFUTWE TAFADHALI) hadi zikidhi?
 
Naendelea kusimama pale pale. Kwenye swala la afya haliitaji mzaha hata kidogo, vivyo hivyo kwenye elimu. Tukumbuke moja ya sababu za kufeli 2010 ni kwa wanafunzi kutochujwa kidato cha pili.
Pia hamasa inakuwepo baada ya kuonekana udhaifu flani. Ni rahisi zaidi kuhamasisha jamii ikiwa inaona uhalisia kuliko kubaki na nadharia pekee.
Inauma kuona wanafunzi wanafeli, lakini inauma zaidi wakibaki kuzura mitaani. Wengi waliosoma shule za serikali wanajua taabu iliopo. Wanafunzi wengi hutoka kwa jitihada binafsi. Walimu walituambia kwa tunapata 10-25% kutoka kwao, nyingine tuhangaike wenyewe.
 
Sophia Simba anazisifu shule hizi kwa kusema yafuatayo:

1. zinasaidia watoto wa kike kuwa na uwezo wa kuchagua mume wanapomaliza masomo yao na kufeli.

2. zinapunguza mimba.

hiyo ndiyo kazi ya hizi shule za kata kwa mujibu wa Sofi.

au tuseme hizi shule ni aina nyingine ya Jando na Unyago.
 
Naendelea kusimama pale pale. Kwenye swala la afya haliitaji mzaha hata kidogo, vivyo hivyo kwenye elimu. Tukumbuke moja ya sababu za kufeli 2010 ni kwa wanafunzi kutochujwa kidato cha pili.
Pia hamasa inakuwepo baada ya kuonekana udhaifu flani. Ni rahisi zaidi kuhamasisha jamii ikiwa inaona uhalisia kuliko kubaki na nadharia pekee.
Inauma kuona wanafunzi wanafeli, lakini inauma zaidi wakibaki kuzura mitaani. Wengi waliosoma shule za serikali wanajua taabu iliopo. Wanafunzi wengi hutoka kwa jitihada binafsi. Walimu walituambia kwa tunapata 10-25% kutoka kwao, nyingine tuhangaike wenyewe.

Babkey bila kuingilia mtazamo wako, ninafikra pana zaidi katika hili

Kwa mtazamo wangu, mtoto anaemaliza kidato cha nne akiwa hajafundishwa masomo mengi kwa kuwa hakukuwa na mwalimu hana tofauti na mgonjwa anaekosa tiba sahihi. Kwangu mimi ninamuona sawa na yule aliemaliza darasa la saba kwa kuwa kila anachokifahamu ni kile anachokifahamu mtoto wa darasa la saba.

Namna pekee ya kuzinduana (wananchi na serikali kwa ujumla) ni kuzifunga kwa muda hata zitakapokuwa zimekidhi haja...hapo ndipo wananchi (kwa kujua umuhimu wake) tutakimbizana kukamilisha serikali ilipoishia na serikali nayo kwa kuumbuka (kufungua shule zisizo na vigezo ambazo kama ingekuwa binafsi zisingeruhusiwa na kupewa kibali kufanya kazi) ita-supplement pale panapobakia

Ni mtazamo wangu
 
shule za kata zitaendelea kuwa muhimu na kadri siku zinavyokwenda zitaonekana umuhimu wake. Kama ni swala la watoto wa vigogo kutosoma kwenye hizo shule mbona hilo ni la cku nyingi hata kabla hazijaanzishwa hizo shule za kata! Na hilo si kwa viongozi walio kwenye madaraka, limekuwa ni kwa kila mtanzania mwenye uwezo kumtafutia mtoto wake shule nzuri na pengine nje ya nchi kwani wengi tunaamini kuwekeza kwenye elimu ni njia bora. Nani hataki mtoto wake apate elimu nzuri ili kesho aje anitunze! Kwenye hizi shule zetu hizi ni changamoto zitakazo zifanya ziwe bora zaidi cku za mbele. Kama kufeli kidato cha 4 imeanza miaka mingi sema wizi wa mitihani ilikuwa inazibeba shule. Wamebanwa sasa ndo matokeo yamekuwa hivi.
 
KUNA WATU WANAPINGA KILA KIYU KILICHOBUNIWA NA KUTEKELEZWA NA SERIKALI YA CCM(hata kama ni kizuri)......NA KUNA WATU WANASAPOTI KILA KITU KINACHOBUNIWA NA KUFANYWA NA CHADEMA....(hata kama ni utumbo)......!
HIYO INAONDOA CREDIBILITY YA U-GREAT THINKER!
 
MFANO: NDESA PESA ametoa helikopta kwa waendao kwa babu loliondo, lukuvi akaunga mkono matibabu ya babu,mahita akaenda kupiga kikombe,HOSEA WA TAKUKURU naye ameshapiga kikombe chake..... wote hawa pasipokujali itikadi zao lao ni moja......! ila kwetu sisi wanazi wa vyama vyetu...tutawabagua kwa kusema kuna waliofanya sawa na kuna waliopotoka na hoja hizi zikiegemea zaidi kwenye unazi wa vyama
 
Ni ukweli usio pingika kuwa pamoja na kuwa shule za kata zina matatizo mengi sana na hata kuitwa magofu,ni dhahiri kuwa vijana wano maliza huko upeo umebadilika na kuelewa ni nini maana ya siasa na hii ndio sababu kuu ya kura za ccm kupungua uchaguzi uliopita na sidhani kwa hali hii kama ccm itavuka 2015
 
Mie huwa nawapiga elimu ya uraia mpaka huwa wanatoa machozi peke yao,na kuwalilia wazazi wao...Je,TUTAFIKA?????
 
Hili ni bomu in the making! Bahati mbaya watawala wanawaona kama watu wasiojua wanalostahili.
 
Ni ukweli usio pingika kuwa pamoja na kuwa shule za kata zina matatizo mengi sana na hata kuitwa magofu,ni dhahiri kuwa vijana wano maliza huko upeo umebadilika na kuelewa ni nini maana ya siasa na hii ndio sababu kuu ya kura za ccm kupungua uchaguzi uliopita na sidhani kwa hali hii kama ccm itavuka 2015

Ni ukweli usiyo pingika juu ya hilo kuwa Watanzania sasa wameanza kupata mwamko fulani. Suala linalo takiwa kwa sasa ni elimu ya uraia huko vijijini ambako ndiyo wapiga kura wapo wengi. Hizo shule za kata zita wezesha usambazaji wa elimu hiyo husika ya uraia ili 2015 pawe hapatoshi yaani Ngoma inogile ili tuweze kutembea KINDAKINDAKI.
 
Back
Top Bottom