Ndugu wanajamvi salaam,
Nimengi yamezungumzwa kuhusiana na shule za kata,
Shule ambazo serikali na ya sasa na chama chake imekuwa ikijinasibu kuwa imefanikiwa
kuleta mapinduzi makubwa ya kielimu kwa kujenga shule hizo kila kata,huku suala la walimu na nyumba zao likibaki kuwa halina ufumbuzi wa wazi.
Mwisho wa juma hili nilipanda daladala kwenda kimbiji,tuliondoka feri saa tatu na nusu,
Ndani ya dala dala kulikuwa na wanafunzi pia wa shule ya sekondari somangira,nikajiuliza hawa kwa muda huu wataenda kusoma nini?
Tulifika kama saa tano hivi wanafunzi walikuwa hoi,wamesweti njia nzima walikuwa wamesimama,mmoja alikuwa amevaa fulana imeandikwa "education for positive change" nikajiuliza which positive change????????????
Nikatafakari hivi watawala wetu na wanasiasa wanajua hatari inayolinyemelea taifa letu kwa kuendelea kuwa na shule hizi?nikawa na majibu mchanganyiko,nikaendelea na safari yangu,mwanafunzi wa mwisho alishuka kimbiji toka feri umbali wa kama saa moja na nusu au mawili.
Wakati narudi ilikuwa saa nane na nusu niliwakuta kituoni wanafunzi hao tena,wakapanda daladala lililokuwa limejaa wakasimama,nikajiuliza tena hii hali mpaka lini?nilimwuliza mmoja wao kuwa anakaa wapi akaniambia tandika,pia akasema wapo wanafunzi wengi wanakaa mjini,nikasema MUNGU WANGU!
Niliuliza tena mwaka jana f4 matokeo yalikuwaje?akasema hakukuwa na one wala div two,kati ya wanafunzi zaidi ya 100 three hazikuzidi tano wliobaki wachache 4 na wengi ziro.
Kwa ufupi hii ndo hali halisi ya shule zetu za kata,nimezunguka hata ktk shule nyingine mikoa mbalimbali hali haiko tofauti.
Nimetafakari sana nikajaribu kulingaisha na shule za wenzetu,ambazo kama si bording,basi watoto wanapelekwa na kurudishwa wakila na kunywa wanachotaka.
Watoto zaidi ya sitini kupata sifuri ni hatari kwa ustawi wa Taifa,
CCM itaondoka lkn Tanzania itabaki,
Wanajamvi na watanzania hili Taifa ndo ccm inataka kutuachia ikishaondoka madarakani?Au ndo inalijenga ikiendelea kuwa madarakani?
Vyama mbadala mpo?mnaiona nchi inavyo uliwa?
Tafadhari nawaomba waungwana tuisaidie hii roho ya nchi,wanasiasa hawa ndo wapiga kura wenu wa kesho,hawa ndo tutawatumia kuondoka na umaskini lkn wamepoteza miaka 4 na kutoka bila kitu kichwani.
Pia rafiki zetu wanaojiandaa kufungua matawi ya ccm NYC,nao tunaomba msaada wao wa kimawazo.Suala la elimu si lakungoja mtoto akishamaliza f4 nikazi kubwa tena kumrudisha aanze upya tunapoteza rasilimali kubwa ya Taifa,tunaua vipaji jambo ambalo ni hatari kubwa kwa ustawi wa nchi yetu
Ebu tutoe maoni kwakuwa serikali sikivu inapita humu inaweza ikayafanyia kazi,watoto wa walala hoi wanaenda shule kukua na wanatoka f4 mikono mitupu.
Naomba kuwasilisha.