Pamoja na hayo,bado naamini kabisa kwamba mtu aliye feli hawezi kukufundisha uka faulu,....
binafsi nakumbuka kugombana na walimu kibao toka primary pale unapo muuliza swali kwa msisitizo ukitaka kujua nae hajui,......
Ni sawa ndugu yangu, lakini unajua ni kwa nini waliofeli ndo wanaenda ualimu? serikali ndo inatakiwa kubeba lawama zote manake ualimu ndo chaguo la mwisho baada ya posts nyingine kushindikana. Pia hata waliofaulu wapo wengi tu, mfano huwezi kuniambia mtu aliye na shahada ya ualimu alifeli. Tatizo hawaendi kufundisha kwa sababu ya maslahi mabovu. Kwa hiyo wanaenda sehemu zinazolipa.