MAONI: Shule za kata zifikiriwe upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAONI: Shule za kata zifikiriwe upya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Speaker, Jan 26, 2011.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa jinsi matokeo yalivo katika shule hizi za kata,...
  Ni wakati sasa wa kutafuta ufumbuzi maalumu kuhusu elimu ya watoto wa Tanzania wasio na uwezo wa kusoma shule za kimataifa (International).

  Tusije kuwa tuna kimbilia kutimiza malengo ya milenia kwa kuzalisha makada (mazuzu) wengi ambao ni kama bomu baadae!

  kwa matokeo haya?
  kwa mfano:
  shule ina wanafunzi 207
  DIV-I = 0 DIV-II = 1 DIV-III = 18 DIV-IV = 109 FLD = 79
  duh.jpg
  hawa waliofeli ni kama bomu ambalo siku likiripuka,sipati kutoa mfano!
  Naamini kabisa kwamba wangeweza kufanya vyema,ila mazingira wanayo somea mmmh!
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Unategemea mwl. ambae halipwi mshahara unaoweza kukidhi mahitaji yake kujituma kuwafundisha hao watoto badala yakuweka akili yake kwenye mambo yanayompa kula?Hapo chakufikiriwa sio shule bali ni mwalimu...ili awe na mwamko wakufundisha!
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu hiyo imefanya vizuri. Kuna moja hapa Bariadi ina wanafunzi 237:
  Division four 4, waliobaki ni zero.
   
 4. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  jamani, nchi inakoelekea ni kubaya, kuna ingine ipo moshi vijijini uko inaitwa kisuluni, division 0, zipo 89, mdogo wangu miongoni mwao, kapata F masomo yote... Ivi taifa linaelekea wapi jamani??,hata pakuanzia kumsaidia mdogo wangu sipajui
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sasa fikiria,hao woooote wenye division 4 wanaenda kusomea ualimu waje kufundisha watoto wetu baadae et,unategemea miujiza hata kama angekuwa analipwa 1,000,0000/=?
   
 6. E

  ESCO Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Du! wache nishangae. Sio mbay ni vijana wa chama hao. Ukiwaendeleza kielimu wakikata chama twala. bora wawe hivyo. Mzee wa vijisent yupo?
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We nawe...hamkuwahi kumuuliza wanajifunza nini huko shuleni?
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hata kama angepewa 7,000,000/= kwa mwezi kama mbunge!
  Tatizo huyo mwalimu ni mtu wa aina gani?

  Wengi ni wale walio feli ndo wanaenda kusomea ualimu,....
  waliofeli form4 wanaenda kufundisha primary...
  walofeli form6 wanaenda kufundisha secondary...

  katika hali kama hii unategemea muujiza wa watoto kufaulu kweli?
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Suala la shule za kata ni la kisiasa zaidi wala si kiutendaji.Kijijini kwetu ipo moja ya kata wanafunzi mia tatu hivi na walimu wako wanne kweli mnategemea nini? Kati ya hao maticha h/mistress yuko included!
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280

  Maisha Tanzania ni tofauti sana. Waliofauli ndio baadaye watakuwa mabomu; waliofeli tangia sasa wanajifahamu wao si wa kuajiriwa moja kwa moja wanajikita kwenye ujasiria mali; baada ya miaka kama 7, yule wa Div. II atakuwa mtu mdogo sana kwa baadhi ya failure. The rate of increase in University graduates is inversely proportional to rate of creating new employment. Mabomu yanazalishwa vyuo vikuu na siyo wale wanaoishia Form IV
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahahaha,pole sana aisee!
  Yani kwenye shule niliyo weka hapo juu kuna ndugu zangu watatu,....woote walikua shule za kata ikiwemo hiyo wana 0 (zero) mmoja tu ndo ana three(3) yaani hali inatisha kwenye shule za kata kwa kweli
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kuna reform kubwa inahitajika kwenye elimu mimi nilisoma Uhuru Primary pale Dodoma halafu nikahamia Darajani Tanga, Secondary nimesoma dodoma Sec waalimu wetu ni tofauti na hawa wa sasa mie siwezi kukubali mtoto wangu akasomeshwe na mwalimu aliefeli form four "voda faster" Waalimu wa zamani walikuwa katika ile walioiita "cream" siku hizi imekuwa kinyume.

  Serikali iboreshe sifa za watakaojiunga na mafunzo ya ualimu ili kuweza kupata waalimu wa kweli naamini shule sio madarasa mazuri ila waalimu wa kweli
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahahaha,yawezekana ni kweli na hapo ndo naona maana ya matokeo haya!
  Kwamba serikali ina lazimika kuweka mazingira magumu ya kusoma ili watu wajiendeleze kivyao waje kujiajiri?
  wow,what a strategy ngoja tuone tunako elekea
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Vincent hapo juu kasema hawa waliofeli ndo wajanja na ndo watakao jiajiri sio walio faulu na baadae kufika vyuoni,so huu ni utaratibu mzuri sana kama ndo mpango wa serikali,.....
  naona makada watakuwa wengi
   
 15. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo la kufeli si kwamba walimu hawajiwezi, tatizo ni kwamba hakuna walimu kabisa kwenye hizo shule, mfano kijijini kwetu mkoa wa tsbors wilaya ya nzega, tarafa ya bukene kata ya Mambali. Mwaka huu ni form four wa kwanza ndo wamemaliza, na matokeo yao ni mabaya sana ni dv 4 na zero, mmoja tu amepata division two hadi nimeshangaa kaipataje. Manake toka ile shule ianzishwe huwa anakuwepo mwl mmoja tu ambaye ni mkuu wa shule. Na shule zote za kata wakuu wa shule hawakosekani manake kuna ulaji na mafungu ya pesa angalau kuliko mwalimu wa kawaida. Hata kama mazingira ni mabovu wakuu wa shule huwa wanajitahidi kuvumilia na kinachowapa uvumilivu ni zile pesa. Hivi jamani tuseme ukweli ni mwl gani atakaa kijijini ambako maji shida, usafiri, umeme, mawasiliano na hata nyumba hakuna.
  My take hizi shule zimeanzishwa kisiasa zaidi, matokeo yake mabinti wakichaguliwa wanaenda kujifunza umalaya na kutoa mimba kwa sababu hata hostel hakuna.
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  \

  Inabidi tulete Net Group Solution.....................
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama wangekua wanawalipa vizuri wangekua na standard ambazo lazima zifuatwe...na waliofanya vizuri wangekua tayari kuwa walimu kwasababu inalipa!Sasa hivi waliofeli ndo kimbilio lao kwasababu hawana choice..na wajanja hawawezi kufanya kazi ya kilo 1.5 wakati akiendelea kusoma atakuja kula zaidi ya hizo!
   
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hayo,bado naamini kabisa kwamba mtu aliye feli hawezi kukufundisha uka faulu,....
  binafsi nakumbuka kugombana na walimu kibao toka primary pale unapo muuliza swali kwa msisitizo ukitaka kujua nae hajui,......
   
 19. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Walimu wapo pengine ni wazuri zaidi ya wale wa ile miaka, tatizo wakimaliza vyuo vya ualimu wanatafuta kazi nyingine, kama serikali inataka wanafunzi wafaulu iboreshe maslah ya walimu, uone kama matokeo hayajawa mazuri. wewe hujiulizi mbona shule za seminari wanafaulu? Kwa sababu wana uhakika wa mkate wa kila siku. Wengi wa walimu katika shule za serikali wanayeyusha tu kufundisha kwa sababu wana mambo mengi ya kufanya kujitafutia chochote kwani mshahara wanaopata hautoshi kwa hali halisi ya maisha.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa we utategemeaje kazi isiyolipa vizuri wala kuthaminiwa WASOMI waikimbilie??Itabaki kua ya vilaza mpaka watakapoboresha swala la mishahara na makazi ya walimu!
   
Loading...