Maoni kwa mtaala mpya wa elimu: badala ya somo la dini ondoa iwepo falsafa

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,072
Katika pitiapitia yangu mitandaoni nimeona mapendekezo ya maboresho ya mtaala wa elimu.

Tumekuwa tukilialia kuhusu oooh, mfumo wa elimu/mtaala unatufundisha kukariri sana. Mara haufundishi watu kujiajiri. Mambo mengi tu. Je katika mtaala mpya tumeweka jambo lipi la kuwafundisha hawa watoto namna ya kufikiri kwa usahihi???

Sitazungumzia saana mengi niliyoyapenda kama masomo ya ufundi stadi na kadhalika, ambayo ni kufundisha watu mbinu zitakazowezesha kujiajiri. Safi sana 👏..... kiukweli nimeziona zile 'highlights' tu.

Sasaa bandugu, kuna utata ama mkanganyiko utakaojitokeza na hata kuleta mijadala ya uhaki na usawa kimitihani. Na pia hata suala la uhalali wa matumizi ya pesa ya walipakodi.

Mfano ikitokea mtu akafaulu kawaida sawasawa na mwenzake katika masomo mengine yote. Wakatofautiana katika somo la dini tu. Je tukimchukua aliyefaulu vizuri dini yake tunajuaje labda walitungiana mitihani rahisi ili tu wafaulu🤨. Maana kuna baadhi wanaamini elimu ni vile mtu anafunuliwa na roho/malaika wake. So mwalimu ni kuweka tiki tu.

Lakini pia ni kama ubinafsi fulani serikali kutumia rasilimali zake kufundisha watu dini zao. Sasa misikiti, masinagogi na makanisa vina kazi gani? Elimu mahsusi ya dini mahsusi itolewe na dini husika tu. Serikali haina dini, au nakosea ndugu zangu?

Kinginee, hayo masomo ya dini (yakitolewa kiutengano, kila mtu kivyake kama sasa) yatakuwa yanatusaidia vipi kujenga umoja wa kitaifa?. Kusimamisha jamii moja? Taifa moja.

Nimeamua kutokuwa mtu wa kupinga tu bila kusema suluhisho. Walishasema wajuvi kuwa; ukiongelea tatizo tu bila suluhisho, basi na we unakuwa sehemu ya tatizo.

Mimi ni sehemu ya suluhisho na si tatizo pekee.

Suala ninalopendekeza mezani ni kuleta somo la FALSAFA
. Hizo ngazi zote mahala walipoweka dini waondoe waweke falsafa. Na haimaanishi hawatafundishwa dini kabisa tena. La!

Dini watafundishwa ndani ya falsafa. Tena kitu kizuri zaidi ni kwamba, masuala yote ya dini zote yatakuwa ni moja ya mada/topics katika somo la falsafa.

Hivyo katika kujifunza itampasa mwanafunzi kuzifahamu nadharia mfano ya dhambi kulingana na imani mbalimbali. Kiotomati itamfanya ajifikirie hivi kimsingi/in essence dhambi hasa ni kitu gani. Mungu ni nini.

Atakuwa mdadisi sana na udadisi ndiyo akili. Na atakapotambua kipi afuate kipi aache basi atakuwa amepata hekima.

Hivi mnafahamu kuwa 'sapiens' kwenye Homo sapiens inamaanisha hekima? Je tunafanya nini kuhakikisha jamii yetu inakuwa na hekima? Lets teach the kids how to think sasa.

Tumewekeza sana katika kufundishana mbinu, mara ujuzi, mara veta na mengineyo ili kuyakabili maisha kwa mbinu. Tuende mbele sasa. Kwani sie bado ni Homo habilis!!??

Turudi katika falsafa yetu ya mtaala mpya. Wanafunzi wote watafanya mtihani wa hilo somo moja na ufaulu (au ufeliji) wao utakuwa wa haki. Watakaofaulu zaidi watakuwa wenye uwezo wa uelewa mpana zaidi usiofungwafungwa na imani bali falsafa. Watu hawa ni wazuri sana hata katika kujenga nchi, siasa na uongozi.

Itasaidia kila mwanafunzi na mwananchi wa baadaye, kuelewa mambo mawili matatu ya imani kinzani na yake. Hili litaongeza;
Kuvumiliana
Kushirikiana
Kuaminiana
Kuelewana
Kujadiliana kwa hoja
Kijengana
Kusaidiana uelewa baina ya dini zote hivyo UMOJA wa kitaifa na ulimwengu wote.

Faida za falsafa zitakuwa nyingi sana. Ukiacha tu hiyo baab kubwa ya 'harmonization' ya dini zooote kuna mambo kama;
Utambuzi wa ukweli na vipimo vyake
Mantiki
Ufikiri
Namna ya kujenga hoja
Kujipima na kupima uhalali wa mambo
Ufanisi wa wazo
Majukumu na makusudi ya mambo anuwai.

Falsafa itasaidia kujenga taifa thabiti lenye mawazo mbalimbali baina ya watu lakini yenye uwezo wa kuunganishwa na kuleta maendeleo. Hivi ndivyo mataifa kama Roma na Marekani hata China na Urusi yalifanikiwa.

Naomba kuongeza kidogo kuhusu madhara ya dini, kufundishwa kwa kifichokificho na kiutengano;

Kuna hatari ya kutengeneza 'cult mindset' ambapo watu hufikiri mawazo yanayoaminiwa na kikundi chao kuwa sahihi maana kwao wanaona 'kila mtu' aliye karibu yao anaamini. Lakini falsafa itasaidia kuchunguza na kujichunguza maana watu wa nje watahoji hivyo akili itashtuka! Kaangalie McKenzie, Kibwetere na hata nje kuna kesi za bwana Jim Jones.

Imani zisipocheckiwa zinazalisha uchawi na ushirikina. Unafahamu kuwa ushirikina na uchawi vinashadadiwa sana na waganga na viongozi wa dini. Jamii ikizidi kuamini kiupofu ndio yanatokea mambo kama;
Kansa ni mapepo
Umasikini ni laana fulani
Tuwaache waovu, Mungu atalipia
Haujafanikiwa? Umelogwa nk.
Sasa imani hizi zikitamalaki tutaendelea kweli!?????

Falsafa itatusaidia saana hata isipoondosha kabisa, basi itawezesha tuulizane na tujiulize maswali sahihi. Na kujiuliza maswali sahihi ni hatua kubwa sana kuelekea suluhisho. Maana tutaanza kupata majibu tokea nyanja mbalimbali kona zote za dunia, ya kale hadi yajayo
 
Tatizo dini nyingine hazifundishi kumpenda Mungu kwa kutumia Akili. Ni Yesu tu ndo alifundisha watu wampende Mungu kwa moyo wote, nguvu zote na kwa AKILI zote.
Kufundisha falsafa ni kutaka watu watumie imani na akili kumjua Mungu. Hilo jambo kuna watu hawatalikubali
 
Kwa hiyo ukitaka kumjua mungu akili uweke pemben ?
 
Tatizo dini nyingine hazifundishi kumpenda Mungu kwa kutumia Akili. Ni Yesu tu ndo alifundisha watu wampende Mungu kwa moyo wote, nguvu zote na kwa AKILI zote.
Kufundisha falsafa ni kutaka watu watumie imani na akili kumjua Mungu. Hilo jambo kuna watu hawatalikubali
Yaani, inasikitisha.

Maana kutumia akili hakuepukiki kama tunataka kuufaidi kweli ufalme wa mbinguni.

Na ni kitu tumejaaliwa wanaadamu na Mola wetu sasa kwa nini tuikatae zawadi hii ya akili/hekima?

Atakayesisitiza kuwa watu wasitumie hekima (kutumia akili kuchagua na kuamua lipi nichukue lipi niache) zao katika imani huyo ni mwenye kutamani tungeumbwa kama wanyama(wameishia vi akili bila uchaguzi ).... au at least anatamani baadaye huko peponi/mbinguni tubadilishwe kuwa kama wanyama.

Ni masikitiko na matusi kwa yule aliyetuumbia akili na zaidi aliyeona ni vema tukaiishi HEKIMA. Kwamba kwa sasa amekosea kutupa jambo hilo?
 
Katika pitiapitia yangu mitandaoni nimeona mapendekezo ya maboresho ya mtaala wa elimu.

Tumekuwa tukilialia kuhusu oooh, mfumo wa elimu/mtaala unatufundisha kukariri sana. Mara haufundishi watu kujiajiri. Mambo mengi tu. Je katika mtaala mpya tumeweka jambo lipi la kuwafundisha hawa watoto namna ya kufikiri kwa usahihi???

Sitazungumzia saana mengi niliyoyapenda kama masomo ya ufundi stadi na kadhalika, ambayo ni kufundisha watu mbinu zitakazowezesha kujiajiri. Safi sana ..... kiukweli nimeziona zile 'highlights' tu.

Sasaa bandugu, kuna utata ama mkanganyiko utakaojitokeza na hata kuleta mijadala ya uhaki na usawa kimitihani. Na pia hata suala la uhalali wa matumizi ya pesa ya walipakodi.

Mfano ikitokea mtu akafaulu kawaida sawasawa na mwenzake katika masomo mengine yote. Wakatofautiana katika somo la dini tu. Je tukimchukua aliyefaulu vizuri dini yake tunajuaje labda walitungiana mitihani rahisi ili tu wafaulu. Maana kuna baadhi wanaamini elimu ni vile mtu anafunuliwa na roho/malaika wake. So mwalimu ni kuweka tiki tu.

Lakini pia ni kama ubinafsi fulani serikali kutumia rasilimali zake kufundisha watu dini zao. Sasa misikiti, masinagogi na makanisa vina kazi gani? Elimu mahsusi ya dini mahsusi itolewe na dini husika tu. Serikali haina dini, au nakosea ndugu zangu?

Kinginee, hayo masomo ya dini (yakitolewa kiutengano, kila mtu kivyake kama sasa) yatakuwa yanatusaidia vipi kujenga umoja wa kitaifa?. Kusimamisha jamii moja? Taifa moja.

Nimeamua kutokuwa mtu wa kupinga tu bila kusema suluhisho. Walishasema wajuvi kuwa; ukiongelea tatizo tu bila suluhisho, basi na we unakuwa sehemu ya tatizo.

Mimi ni sehemu ya suluhisho na si tatizo pekee.

Suala ninalopendekeza mezani ni kuleta somo la FALSAFA
. Hizo ngazi zote mahala walipoweka dini waondoe waweke falsafa. Na haimaanishi hawatafundishwa dini kabisa tena. La!

Dini watafundishwa ndani ya falsafa. Tena kitu kizuri zaidi ni kwamba, masuala yote ya dini zote yatakuwa ni moja ya mada/topics katika somo la falsafa.

Hivyo katika kujifunza itampasa mwanafunzi kuzifahamu nadharia mfano ya dhambi kulingana na imani mbalimbali. Kiotomati itamfanya ajifikirie hivi kimsingi/in essence dhambi hasa ni kitu gani. Mungu ni nini.

Atakuwa mdadisi sana na udadisi ndiyo akili. Na atakapotambua kipi afuate kipi aache basi atakuwa amepata hekima.

Hivi mnafahamu kuwa 'sapiens' kwenye Homo sapiens inamaanisha hekima? Je tunafanya nini kuhakikisha jamii yetu inakuwa na hekima? Lets teach the kids how to think sasa.

Tumewekeza sana katika kufundishana mbinu, mara ujuzi, mara veta na mengineyo ili kuyakabili maisha kwa mbinu. Tuende mbele sasa. Kwani sie bado ni Homo habilis!!??

Turudi katika falsafa yetu ya mtaala mpya. Wanafunzi wote watafanya mtihani wa hilo somo moja na ufaulu (au ufeliji) wao utakuwa wa haki. Watakaofaulu zaidi watakuwa wenye uwezo wa uelewa mpana zaidi usiofungwafungwa na imani bali falsafa. Watu hawa ni wazuri sana hata katika kujenga nchi, siasa na uongozi.

Itasaidia kila mwanafunzi na mwananchi wa baadaye, kuelewa mambo mawili matatu ya imani kinzani na yake. Hili litaongeza;
Kuvumiliana
Kushirikiana
Kuaminiana
Kuelewana
Kujadiliana kwa hoja
Kijengana
Kusaidiana uelewa baina ya dini zote hivyo UMOJA wa kitaifa na ulimwengu wote.

Faida za falsafa zitakuwa nyingi sana. Ukiacha tu hiyo baab kubwa ya 'harmonization' ya dini zooote kuna mambo kama;
Utambuzi wa ukweli na vipimo vyake
Mantiki
Ufikiri
Namna ya kujenga hoja
Kujipima na kupima uhalali wa mambo
Ufanisi wa wazo
Majukumu na makusudi ya mambo anuwai.

Falsafa itasaidia kujenga taifa thabiti lenye mawazo mbalimbali baina ya watu lakini yenye uwezo wa kuunganishwa na kuleta maendeleo. Hivi ndivyo mataifa kama Roma na Marekani hata China na Urusi yalifanikiwa.

Naomba kuongeza kidogo kuhusu madhara ya dini, kufundishwa kwa kifichokificho na kiutengano;

Kuna hatari ya kutengeneza 'cult mindset' ambapo watu hufikiri mawazo yanayoaminiwa na kikundi chao kuwa sahihi maana kwao wanaona 'kila mtu' aliye karibu yao anaamini. Lakini falsafa itasaidia kuchunguza na kujichunguza maana watu wa nje watahoji hivyo akili itashtuka! Kaangalie McKenzie, Kibwetere na hata nje kuna kesi za bwana Jim Jones.

Imani zisipocheckiwa zinazalisha uchawi na ushirikina. Unafahamu kuwa ushirikina na uchawi vinashadadiwa sana na waganga na viongozi wa dini. Jamii ikizidi kuamini kiupofu ndio yanatokea mambo kama;
Kansa ni mapepo
Umasikini ni laana fulani
Tuwaache waovu, Mungu atalipia
Haujafanikiwa? Umelogwa nk.
Sasa imani hizi zikitamalaki tutaendelea kweli!?????

Falsafa itatusaidia saana hata isipoondosha kabisa, basi itawezesha tuulizane na tujiulize maswali sahihi. Na kujiuliza maswali sahihi ni hatua kubwa sana kuelekea suluhisho. Maana tutaanza kupata majibu tokea nyanja mbalimbali kona zote za dunia, ya kale hadi yajayo
Wazo zuri!
 
Tatizo dini nyingine hazifundishi kumpenda Mungu kwa kutumia Akili. Ni Yesu tu ndo alifundisha watu wampende Mungu kwa moyo wote, nguvu zote na kwa AKILI zote.
Kufundisha falsafa ni kutaka watu watumie imani na akili kumjua Mungu. Hilo jambo kuna watu hawatalikubali
Kama uzi unavyopendekeza, hilo litakuwa suala la dini husika sio mtaala wa elimu wa Serikali.
 
Tatizo dini nyingine hazifundishi kumpenda Mungu kwa kutumia Akili. Ni Yesu tu ndo alifundisha watu wampende Mungu kwa moyo wote, nguvu zote na kwa AKILI zote.
Kufundisha falsafa ni kutaka watu watumie imani na akili kumjua Mungu. Hilo jambo kuna watu hawatalikubali
Hebu iweke sawa hii. akili sindio tambuzi ya kilakitu au kuna vitu huwa haviitaji akili ili uvifahamu?
 
Kama umzazi, mfundishe nyumbani na kokote mnakoenda kuabudu.
huko mashuleni ndipo wanapopindwa sana.lazma maadili yafundishwe wanakutana watoto wenye tabia mbalimbali kutoka kwao.dini inatakiwa ifundishwe kwa lazma.
 
Ni wajibu wa wote. Maadili ni mzazi zaidi, dini ni mnakoabudu. Elimu dunia ni shule
 
Back
Top Bottom