BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,554
- 9,238
Unaweza kuniambia ni nani alikuwa anayaorodhesha hayo makabila? Unajua ni kwa nini Wajerumani na Waingereza wanaitwa wakoloni wakati Waarabu na Wareno wanaitwa wafanyabiashara? Historia ina tabia ya kuendelea kujiandika. Mwaka 1991 Tanzani ilikuwa na chama kimoja tu cha siasa, lakini baada ya mwaka 1992 bado Tanzania iliendelea kuwa na chama kimoja cha siasa? Hayo makabila yalihesabiwa mwaka gani na yalihesabiwa na nani? Hayo mambo ya kukaririshwa wengine hatuna habari nayo!!
Chiduo hapa hatuzungumzii ubaguzi bali tunazungumza kama Manji ni Mtanzania ama la! Mimi nataka kina Borat69 waniambie sifa za mtu kuwa Mtanzania ni zipi na waniambie Manji ni sifa gani kati ya hizo hana ili tujue wana hoja ya msingi wanaposema kwamba Manji si Mtanzania. Mandela angekuwa kama nyie leo sijui Afrika Kusini ingekuwaje?
Watu wenye sifa kama zenu ndiyo wale wamejazana Afrika Kusini kwa sasa wanaodhani waafrika wenzao toka nchi nyingine wamekwenda nchi kwao kuchuka nafasi zao za kazi. Mimi nachukia ubaguzi hata ufanywe na nani. Hakuna mahali kwenye bandiko langu nimesema kwamba wahindi hawabagui watu weusi, bali ninatetea sifa za mtu kuwa Mtanzania ambazo nadhani Manji anazo. Tatizo lenu badala ya kujadili hoja zangu mnanijadili mimi.
Nina shughuli zangu zinazoniweka mjini na kunipa uwezo wa kununua dona na kauzu wa kulisha tumbo langu!!
Tumia akili japo kiduchu tu, unawajuwa Wahindi? Jamal aliaminiwa na nyerere na akampa uwaziri wa fedha hebu tueleze alipokufa alikwenda kuzikwa wapi? hivi ujinga ni kipaji kumbe?@Elli ndiyo Tanzania ni nchi yake kwani ana uraia wa nchi nyingine? Kuna tatizo la watu kuwaza kwamba wahindi siyo watanzania. Ni bahati mbaya sana!!
Nitakuuliza maswali kadhaa naomba majibu mkuu.
A) Tembelea kwenye makampuni mengi ya Wahindi,Je hakuna ubaguzi wa wazawa huko?
B) Kwenye maghorofa Yao ya makazi huko Upanga na kwengineko hakuna ubaguzi katika upangishaji!? Hili limeshamkuta mdogo wangu.
C) Kama wao ni wabantu kwa nini wasikubali tuwaoe madada/mabinti zao!?
D) Katika shule zao (ie: Al muntazir etc) unajua ubaguzi unaoendelea huko!?
E) Umeshawahi kwenda BOA BANK!? Huduma kwa Golo zikoje!?
F) Unajua maana ya neno GOLO!? Wanatumia Wahindi kutuita sisi Watanzania wazawa.
Kuna watu huwa wanashindwa kujenga hoja na kukimbilia kutukana au kujaribu kuleta lugha za kihuni. Mimi na Manji hatujuani na wala sina maslahi naye kwa vyovyote vile. Hapa ninachotaka kujulishwa sifa za mtu kuwa mtanzania ni zipi? Mimi na Manji tuna tofauti kubwa sana.
1. Manji ni Muislam mimi ni Mkristo.
2. Manji CCM mimi CHADEMA
3. Manji anaishi Dar mimi naishi Iringa
4. Manji ni Yanga mimi ni Simba
5. Yeye Mhindi mimi Mnyamwezi
4. Yeye Mfanyabiashara Mkubwa mimi Machinga
Mjadala huu ni kutaka kujua sifa za mtu kuwa mtanzania na wala si mjadala wa ufisadi wa Manji au utajiri wake ameupataje. Ikifika kujadili ufisadi wake basi huko tutajadili ufisadi. Lakini katika hili hakuna mwenye hoja za kushiba kueleza ni kwa nini wengi wenu mnafikiri kwamba Manji si mtanzania. Kama tukizijua sifa za utanzania basi ndiyo tutaweza kujua kama Manji ni mtanzania au la.
Somji Juma alisema unaweza kuwa Raia wa Tanzania lakini usiwe Mtanzania. Nikataka kufafanuliwa inakuwaje uwe Raia wa Tanzania ingawa si Mtanzania. Mimi sikuelewa lakini Mzito Kabwela alimuelewa, na wengine pia labda wamemuelewa. Ninachotaka kueleweshwa ni hiki. Utanzania ni nini?
Sasa ili usionekane mjinga, fanya utafiti kwenye vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama kuna muhindi hata mmoja? au unadhani India hawana jeshi kwamba wahindi wa hapa hawawezi kutumikia jeshi? Idd Amin he was perfect.Kuna watu huwa wanashindwa kujenga hoja na kukimbilia kutukana au kujaribu kuleta lugha za kihuni. Mimi na Manji hatujuani na wala sina maslahi naye kwa vyovyote vile. Hapa ninachotaka kujulishwa sifa za mtu kuwa mtanzania ni zipi? Mimi na Manji tuna tofauti kubwa sana.
1. Manji ni Muislam mimi ni Mkristo.
2. Manji CCM mimi CHADEMA
3. Manji anaishi Dar mimi naishi Iringa
4. Manji ni Yanga mimi ni Simba
5. Yeye Mhindi mimi Mnyamwezi
4. Yeye Mfanyabiashara Mkubwa mimi Machinga
Mjadala huu ni kutaka kujua sifa za mtu kuwa mtanzania na wala si mjadala wa ufisadi wa Manji au utajiri wake ameupataje. Ikifika kujadili ufisadi wake basi huko tutajadili ufisadi. Lakini katika hili hakuna mwenye hoja za kushiba kueleza ni kwa nini wengi wenu mnafikiri kwamba Manji si mtanzania. Kama tukizijua sifa za utanzania basi ndiyo tutaweza kujua kama Manji ni mtanzania au la.
Somji Juma alisema unaweza kuwa Raia wa Tanzania lakini usiwe Mtanzania. Nikataka kufafanuliwa inakuwaje uwe Raia wa Tanzania ingawa si Mtanzania. Mimi sikuelewa lakini Mzito Kabwela alimuelewa, na wengine pia labda wamemuelewa. Ninachotaka kueleweshwa ni hiki. Utanzania ni nini?
Ubaguzi ni kama ugonjwa, humpata mtu yeyote yule. Waulize watu wanaosoma masomo ya Jamii kuhusu saikolojia ya watu wachache (Minority) dhidi ya watu walio wengi kwenye eneo husika.
London watanganyika husema Wazanzibar wanawabagua, Dar es salaam wazanzibar wanadaia wanagandamizwa na watanganyika. Hisia za kubaguliwa na ubaguzi ni vitu viwili tofauti. Mzee Mohamed Said anadai kuwa Waislamu wanabaguliwa katika mfumo wa uongozi na Elimu. Ni kweli?
SABABU ZA MANJI NA MAKANJUBHAI WENZAKE KUTOKUWA WATANZANIA
1. KATiba ya nchi yetu inatambua uraia wa nchi moja.. Hivyo basi ni lazima uwe na pasport moja.. Ila hawa wenzetu sio manji tu wana pasport zaid ya moja kinyume na katiba ya nchi inayotambua uraia wa nchi moja
2. Narudia tena Tanzania hakujawahi kutokea kabila likaitwa WAHINDI...Niambie mkoa wanaotoka wahindi... Tanzania kila kabila lina mtani wake wa kikabila kama vile Muha na mhaya au mjaluo... Msukuma na watu wa pwani...
niambie Hili mnalosema kabila la wahindi mtani wake nani kikabila... Kupitia mahusiano haya ya kikabila ndio chanzo hata cha kuoweana.. Sasa nikuulize wewe umeshawahi kuhudhiria ndoa ya Ndugu zangu waluguru na mhindi...
Nilikuwa sijui, kumbe Manji ana Passport ya India? Basi Chama chake cha CCM inabidi kishitakiwe kwa kusimamisha mtu wa taifa jingine kugombea udiwani Tanzania. Na pia inaonekana watu wa UKAWA ni wa ajabu kabisa, walishindwaje kumwekea pingamizi raia wa India hadi akachaguliwa kuwa Diwani wa Mbagala Kuu? Watu wa uhamiaji nao Magufuli awatumbue majipu, maana kuna mtu anajulikana kabisa na watu ambao hawafayi kazi Uhamiaji kwamba si Mtanzania lakini wao wanajifanya hawamjui!! Kamata Manji rudisha kwao India.
Mashabiki wa Timu ya Yanga nao walikosa mtanzania mwenzao kuwa kiongozi hadi wamchague mtu wa taifa lingine kuwa Mwenyekiti wao. Hivi simba wakipinga ushindi wao kwa kuwa wanaoongozwa na mtu ambaye si mtanzania watalalamika kweli?
Hebu Chiduo na Daud1990 nisaidieni kuujua Utanzania!!