Ili uamini wahindi wa nchi hii sio watanzania.. katika kipindi cha uchaguzi mkuu asilimia kubwa ya wahindi walikuwa wanajiandaa kurudi kwao kama nchi ingechukuliwa na upinzani..(hii ni according to them)... nakumbuka hotuba moja ya magufuli alisema " Ndugu zangu wenye asili ya asia nipeni kula zenu achaneni na propaganda kuwa mtarudi kwenu kama nikishinda uraisi"
Mtu kuwa na mawazo hayo ni sababu tosha wewe sio mtanzania.... mbona maswali hayo hakujiuliza mchaga,mfipa au mzaramo.... Hawa na makibila mengine ndio watanzania...
Kama utaniita mimi ni racist poa ila hata bendera ya taifa ya nchi hii hakuna rangi inayoonesha uwepo wa hawa wadudu...
Ili swali liwe swali unajua kuwa ni lazima liwe na vigezo vyake. Kuna swali gani sijalijibu? Mimi ndiyo nimewaulizeni nyinyi mtaje vigezo vya mtu kuwa Mtanzania mpaka sasa hakuna jibu. Somji Juma katoa maelezo ya kujikanganya kuonesha kwamba kuna mtanzania na raia wa Tanzania, ambayo mimi nayashangaa sana. Hivi unaweza kuwa Raia wa Tanzania na usiwe mtanzania? Semeni basi sifa za mtu kuwa "Mtanzania" na mseme kuwa Manji hana sifa hizo!!
ISina uhakika kama Magufuli anamchukia Manji, anachukia ufisadi. ila ukitaka kumjua Manji kwa undani soma thread zinazomhusu, zimo tele humu JF, zipo kibao sanamagufuli anamchukia sana Manji, sijui alimfanyia nini...manji amesaidia watu wengi sana mpaka club yetu ya Yanga
Allen,Borat69 ingawa maswali yako unayaona ya msingi lakini si ya msingi hata kidogo. Kwanza shule nyingi unazoziita za wahindi zinaendeshwa kwa mfumo wa Kiseminari kama shule za Makanisa. Kuna watu wanafadhiliwa na "Jamaat" au The Aga Khan Foundation kwa hivo ni lazima ada itatofautiana na wewe unayelipa ada yote mwenyewe.
Hilo la kuhudhuria ndoa ya Mhindi na "Mswahili" siyo hoja ya msingi ya kubatilisha utanzania wa mtu. kwa mfano kuna watu ambao wala si wahindi wapo kwenye jamii yetu wanaodhani watoto wao hawafai kuoa au kuolewa na watu toka makabila fulani fulani au hata koo. Lakini tuwe wakweli hivi kweli unaupima utanzania wa mtu kwa kuolewa na mtu wa Rangi nyingine?
Tujadiliane hoja ya msingi ambayo tuambiane sifa za utanzania ni zipi ili tuone kama Manji anazo au hana!! Hizo nyingine ni nakshi zinazoweza kuleta tashtiti isiyo na sababu!!
Mkuu Daudi,
Huyu Allen ni Jipu. Tumemuuliza maswali ya msingi kuhusu hao magabacholi wake hataki kujibu. Anakuja na mbwembwe nyingi. Hawa watu ndio Wahujumu UCHUMI wa Taifa letu nambari moja.
Wako katika kila madili machafu, kwa mfano Issue ya Radar,Kagoda,Loliondo gate,Escrow,EPA, ukwepaji Kodi n.k.
Halafu Leo hii wanakimbilia kujiita Watanzania na kulia kwamba wanaonewa pambafu zao.
Nani racist hapa? Hebu tuambie mtz mweusi aliyemuoa muhindi?
@Elli ndiyo Tanzania ni nchi yake kwani ana uraia wa nchi nyingine? Kuna tatizo la watu kuwaza kwamba wahindi siyo watanzania. Ni bahati mbaya sana!!
Inasikisha saana watu humu hakuna kinachowasumbua ni ubaguzi tu, ni kwasababu tumeganda tu, wengi hatujawahi kutoka nje ya nchi, haya mambo sasa yamepitwa na wakati, watu hawatizami rangi, dini au jinsia ya mtu.
Wengi wetu tunazungumzia biashara wakati hatujawahi fanya biashara hata ya kuwa na kioski, tujikumbushe enzi ya Rais Nyerere tukapiga kelele kwanini sisi tunakaa nje ya mji wahindi wanakaa mjini na wanamiliki magorofa, tukasikilizwa kilio chetu zikataifishwa nyumba za wahindi na waarabu, pamoja na mashamba na biashara zao, tukapewa maflat mjini tuishi, mashamba, pamoja na baadhi ya biashara zao tuendeshe.
Baadhi ya wafanyabiashara walioamua kubaki, wakaanza biashara alifu kwa ujiti,huku wenzetu walio bahatika kupata flat walionyanganywa wahindi na waarabu, kukaa mjini wakashindwa wakaamua kuwaita wahindi wawapatie flat zao walizopewa, badala yake wao kulipwa pesa na kurudi walikotoka.
Kwa wale waliopewa kuendesha biashara wakaamua kuongeza wake na kushinda katika mabaa na kufilisi biashara walizopewa na waliopewa mashamba waka yaua yote, sasa tusione hawa wenzetu wanafanya biashara tukahisi ni kazi ndogo, akinyangaywa leo ukipewa wewe utaweza ifanya? Pesa nzuri ni ya kuipata kwa jasho lako ya kupewa bure huna uchungu nayo.
Sasa tunaanza tena kuwalalamikia wahindi.Tuache haya mambo kama hatutoacha tutabaki kulalamika tu huku tumeganda hatuendi kokote.
Hakuna nchi iliyopata maendeleo kwa kuwanyanganya wafanyabiashara mali zao au kuzitaifisha, kama unaleta maendeleo angefanya Mandela Afrika kusini kwa uchungu alio kuwa nao, na tutizame matatizo waliopata Zimbabwe na Uganda kwa kutumia hatua hizo.
Chiduo hapa hatuzungumzii ubaguzi bali tunazungumza kama Manji ni Mtanzania ama la! Mimi nataka kina Borat69 waniambie sifa za mtu kuwa Mtanzania ni zipi na waniambie Manji ni sifa gani kati ya hizo hana ili tujue wana hoja ya msingi wanaposema kwamba Manji si Mtanzania. Mandela angekuwa kama nyie leo sijui Afrika Kusini ingekuwaje?
Watu wenye sifa kama zenu ndiyo wale wamejazana Afrika Kusini kwa sasa wanaodhani waafrika wenzao toka nchi nyingine wamekwenda nchi kwao kuchuka nafasi zao za kazi. Mimi nachukia ubaguzi hata ufanywe na nani. Hakuna mahali kwenye bandiko langu nimesema kwamba wahindi hawabagui watu weusi, bali ninatetea sifa za mtu kuwa Mtanzania ambazo nadhani Manji anazo. Tatizo lenu badala ya kujadili hoja zangu mnanijadili mimi.
Nina shughuli zangu zinazoniweka mjini na kunipa uwezo wa kununua dona na kauzu wa kulisha tumbo langu!!
magufuli anamchukia sana Manji, sijui alimfanyia nini...manji amesaidia watu wengi sana mpaka club yetu ya Yanga
Ninachomaanisha ni hiki. Wangoni asili yao ni Afrika kusini, ni watanzania si watanzania? Wairaq (Kabila la Dr. Slaa?) asili yao ni Mashariki ya kati, ni watanzania si watanzania? Uasili wa mtu kabla ya kuja hapa Tanganyika si kigezo kwamba yeye si mtanzania. Tunawaita wahindi kwa kuwa wao walitokea India, lakini kutokea India hakumaanishi kwamba hawa kina Yusuph Manji wao kwao kwa sasa ni India!!Sasa mkuu hapo umemaanisha nini??
Ni kweli anaweza kuhama nchi ila tujue tu atahama na ajira za watu kibao ambao mpaka sasa serikali bado haijajipanga kuwapa ajira wala kuwawezesha kujiajiri.
Siungi mkono ufisadi ila nawakubusha tujadili haya mambo kwa kuangali pande zote ili watu waweze kujipanga.
Queen Esther unataka kuniambia kwamba viongozi wa CCM huwa wanashinda kwa kununua kura? Halafu huyo Manji kwa nini awanunue wapiga kura wa UKAWA badala ya kuwanunua CCM wanaopitisha jina la Mgombea U-meya? Mbona unataka kujenga picha kwamba wanunua kura wapo CCM ila kura zinazonunuliwa zipo UKAWA? Kwa nini Manji asinunue kura za wana CCM wenzake?