Manji atakiwa kuripoti Ofisi za Mamlaka ya Uhamiaji. Pasi 126 za kusafiria zakamatwa ofisini kwake

This country it heading to lawlessness......sasa how will we attract investors if they are not protected by deeds of their companies of which they have legal personality and operators, and ofcourse are quite different from the owners....(shareholders)..whom don't have direct control of day to day activities?
 
Ni Passport za nchi gani?
Tatizo Sio passport... Tatizo hawana vibali vya kufanya kazi ktk JMT
-ilisomeka kuwa Yussuf alijivua madaraka yote na kuyakabidhi..... Je anatakiwa ni mkurugenzi wa QG wa sasa au aliyepita kwenda kwenye kadhia hiyo????
 
Kuna mambo haya hitaji kukomoana, ni swala la kuelimishana na maisha yaendelee. serikali inapata kodi kutoka Quality group, kuna watu wameajiriwa kupitia Quality group....

nakumbuka kuna nchi fulani jamaa fulani alikamatwa kwa kutokulipa kodi nadhani, serikali ilichokifanya sio kumfilisi au kumkomoa ( sababu pia wanategemea kuendelea kupata mapato kutoka kwake, akifanikiwa zaidi ndivyo atalipa zaidi kodi) walimpangia muda, baada ya muda fulani uwe umelipa malimbikizi ya kodi yako.

Hapa kwetu nadhani tunataka wote tuwe masikini, na kama tukiwa wote masikini sijui serikali itakuwaje tajiri?? kodi watamdai masikini? Fikra zikigonga ukuta kwa utawaja wa chuki na kisasi basi wote tunajikuta tunaumia.
Hakika mkuu, kwa staili hii naliona anguko kubwa mbele, wakiisha kina manji sijui watatafutwa kina naniiii
 
Lakin Manji si alishajiuzulu uendeshaji wa hiyo kampuni ya familia? Au ndo anatafutwa kwa makosa milioni moja ili tu afungwe? Try him so many times until one sticks?
Kwani hizo passport fake zilikutwa nyumbani kwao au ofisini kwake?
 
UHAMIAJI WAKAMATA PASSPORT 126 QUALITY GROUP.



Upepo Mchafu Wazidi Kumuandama Manji, Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....

John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.

Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.

Mara tu atokapo, aliport ofisi hii ili tumuunganishwe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.

Utakamatwa, utawekwa ndani, utajibu mashitaka.
View attachment 470414
Yusuf Mehbub Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini Tanzaznia na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu(CCM) Jimbo la Mbagala Dar es Salaam.

Kutoka Kuuza Unga hadi issue za Passport
 
Kuna mambo haya hitaji kukomoana, ni swala la kuelimishana na maisha yaendelee. serikali inapata kodi kutoka Quality group, kuna watu wameajiriwa kupitia Quality group....

nakumbuka kuna nchi fulani jamaa fulani alikamatwa kwa kutokulipa kodi nadhani, serikali ilichokifanya sio kumfilisi au kumkomoa ( sababu pia wanategemea kuendelea kupata mapato kutoka kwake, akifanikiwa zaidi ndivyo atalipa zaidi kodi) walimpangia muda, baada ya muda fulani uwe umelipa malimbikizi ya kodi yako.

Hapa kwetu nadhani tunataka wote tuwe masikini, na kama tukiwa wote masikini sijui serikali itakuwaje tajiri?? kodi watamdai masikini? Fikra zikigonga ukuta kwa utawaja wa chuki na kisasi basi wote tunajikuta tunaumia.
Maskini wanaamini wanaweza kuwa Matajiri kwa Tajiri kuwa kama wao.....
 
alizipataje waanze na maofisa wao kwanza ndo chanzo cha uchafu wote hapa nchini
Hivi imesikiliza hiyo video vzr?si kwamba ni Passport fake pia si passport za Tanzania.Hizo ni passport za nje isipokua wanafanya kazi nchini bila vibali!!
 
Naona system hii ya sasa hawamkubali mwenyekiti wa yanga

Ova
I understand where you are coming from...

Hatujawai kuona tajiri akilala lupango tena kwenye makosa ambayo yanawahusisha maskini pia. Hii hata Makonda ameiongolea kwamba kupindi cha nyuma matajiri walikuwa wanapigiwa simu waende kituoni kuyamaliza kimya kimya!

Kwa sababu hatujazoea kuona haya ndio tunaanza kufikiria mambo mbali mbali, "ana andamwa". Lakini mpaka mwisho wa awamu ya Magufuli tutakuwa tumeshazoea kuona tajiri na maskini kwenye mikono ya sheria wana shungulikiwa sawa!
 
Kabla hujaanza kuuliza hayo masuala jiulize Kwanza unaemuuliza ni nani immigration na wewe ni nani immigration

ana elimu gani kwenye immigration na wewe una elimu gani kwenye immigration,

ana cheo gani immigration na wewe una cheo gani immigration,

kazi kaanza lini immigration na wewe kazi ulianza lini immigration.

Ukishapata majibu ya hayo maswali ndio uulize sasa maswali yako.


Kwanza Ningekuuliza Unayo Passport Na Kama Ulipata Fursa Ya Kuisoma Maelezo Yaliyomo Kwenye Passport

Ndiyo Ungeniuliza hayo Maswali Yako, Kila Nchi Ina Passport Zake Na Security Details Zake Kwenye Printing, Inks, Watermarks And Holograms

Na Verification Inafanyika Na Immigration Husika Huyu Immigration Wa Posta Anayajuaje Ya India Au Uko Passport Zilipotoka?

So Kwasababu Kasema Mtu Wa Immigration Basi Kila Anachosema Ni Kweli Usiwe Na Ujinga Wa Kiasi Hiko
 
Kwani hizo passport fake zilikutwa nyumbani kwao au ofisini kwake?
Ndugu yangu mbona maswali kama tuko shule? Nyumbani kwake anaishi peke yake? Hakuna mtu mwingine ambaye kwa sasa anaendesha kampuni hizo na anaishi na Manji?
 
This is too much jamani!
Nchi yenyewe masikini hii tajiri mwema kama Manji aliyetoa ajira kwa maelfu ya Watanzania ananyanyaswa sababu ya chuki za kisiasa.

Kwenye madawa mmekosa la kumtia hatiani mmehamia kwenye passport,soon mtafikia lile lengo lenu la kunduchi beach.
Time will tell...
Njia Moja nzuri ya kuepuka kufatwa fatwa ni kufata sheria za nchi,acheni upuuzi wa kutetea mambo yasiyo na tija,manji anatakiwa afate sheria za nchi hata wakimfata fata awapeleke mahakani
 
Lakini yote ya msing ila wangepambana na fisadi zilizotokea zikaikamua nchi sasawa kama hivi kwa madawa hata wala madawa wangepungua kwa kuwa wangekuwa na kisomo na ajira baadayake. Madawa si upatikanaji na pia sera za uchumi. Escrow, meremeta, Richmond, madini yetu etc list ni ndefu hii, hii hawajapata taarifa zake na hamna list ya wadokozi hawa kwa Dar es Salaam. Au fisadi hizi zilitoke Dodoma au Kwimba, Ni Dar es Salaam hiyo hiyo. Jameni tuwe serious na tupangilie priority ya mambo ikiwa tunataka kiki sahihi kwa wanadamu na hata kwa Muumba. Sasa watu wote watakuwa sober kisha watafanya kazi gani uchumi unavyodorora? Fedha zilizoibwa na mafisadi papa ambazo ndio wanatumia kununulia unga na kutuulia vijana wetu huku wakifilisi nchi -- hii kweli hawa intelijensia hawaoni na kujua wakibana mafisadi unga unakata na nchi inapata ajira, elimu na maendeleo? Tufikirie nje ya box pia
 
Hivi imesikiliza hiyo video vzr?si kwamba ni Passport fake pia si passport za Tanzania.Hizo ni passport za nje isipokua wanafanya kazi nchini bila vibali!!
sawa so hapa ni kwamba hawana vibali vya kuishi tz waje hata ofisini kwetu wapo kibao wanajifanya wahindi wa kariakoo kumbe wa hukoo bombay
 
Zamani walikuwa wapi? mtindo huu wa kutengeneza makosa aka kula deal pamoja na "watawala" halafu mkizenguana mnaanza kulana vichwa ukome kabisa. Kama kuna makes ya kiutendaji yanatokea huko nyuma hii inamanisha serikali ama mamlaka inajua. Tumechoka kupotezeana muda. FIX IT.
Ndo kosa la kurefusha mdomo wakati unaelewa huna maisha masafi. It was simple! Cooperate! Sasa akaanza oooh, mi yanga! Oooh jina kubwa!, Oooh mtoto mdogo, toooo much.
 
Serikali ya kitapelitapeli tu hii.

Vitu vya msingi ni kudeal na wanakwaya+wafuta gari la Manji.

Pipo from ze village now in town mtamtambuaje kama yeye kaingia town?
 
Back
Top Bottom