Manji atakiwa kuripoti Ofisi za Mamlaka ya Uhamiaji. Pasi 126 za kusafiria zakamatwa ofisini kwake

Nawapongeza sana immigration tafuteni na wageni wengine wanaoishi bila taratibu wote wachukuliwe hatua stahiki.
 
Sasa inaonekana professionalism hamna tena sasa mbona hilo kosa la kawaida hata nchi za kiarabu, uingreza na umarekani yanatokewa muajiri anapigwa faini na wafanyayakazi wanarudishwa kwao, sasa lugha kama hizo za vitisho ya nini kama mtu kaua, kuongea kuwa hatutojali pesa zake, yote ya nini, kwanini asizungumze kistaarabu pindi atapotoka hospital tutampeleka mahakamani, na kuiacha ifanye kazi yake.
Tabu sana bwana Faridi. Kuna vitu vinatia hasira nchi hii. Sasa kitu kama hichi ndio wanataka wafanye headlines tena. Wafanye kazi yao in a professional way. That's all.
 
Kamanda anasema walikuwa wanajiandaa kwenda kumkamata, kabla hawajaenda wakasikia yuko Hospitali kalazwa. Swali; Uhamiaji walikuwa wanajiandaa kwenye kumkamatia wapi ilhali alikuwa Polisi?
Ule mshtuko wa moyo ulisababishwa na mengi.
 
UHAMIAJI WAKAMATA PASSPORT 126 QUALITY GROUP.






Kuna Big Question Mark Kwenye Hii Saga.

Kwanza Passport Si Za Tanzania Iweje Immigration Officer Wa Tanzania Azisemee Passport Za Nchi Zingine Kuwa Ni Fake????

Pili Kwanini Amtaje Yusuf Manji Moja Kwa Moja Wakati Manji Ni advisor Tu Wa Quality Group Wakati Ameshajiuzuru Kuanzia Mwezi Wa 4 Mwaka Jana?

Tatu Kama Watumishi Hawana Vibali Basi Ni Kosa La Kiutawala Si La Mtu Binafsi

Nne Quality Group Ni Limited Company Iweje Umtaje Shareholder Mmoja Kuwa Ndiyo Muhusika Mkuu?

Ukifanya Kazi Kwa Hisia Au Kushurutishwa Kuna wakati Unajisahau Na Kupitiliza Mipaka

Gazeti La Citizen La Tarehe 13 April 2016 Kwenye Kurasa Nzima Ya 13 Barua Ya Yusuf Manji " Notice Of Retirement From Quality Group Of Companies"

Hii Ilikuwa Barua Ya Wazi Ya Kujiuzulu Na Kubaki Kama Mshauri Tu Pindi Atakapoitajika

Nchi Hii Inapoelekea Ni Pabaya, Na Niaanza Kukumbuka Historia Ya Robin Hood Alongside His Band Of Merry Men.

201604191443.pdf
 
Tanamuhitaji kwa lipi labda kwa mfano.Funga bakuli lako your talking non sense suala la uhamiaji linazungumzika ???
Nina maana kuwa wahusika wanaweza kuombewa kibali au wakarudishwa makwao!
Manji tunamhitaji kama mwekezaji mkubwa mzalendo! Anachangia sana kwenye pato la Taifa! Cha maana afuate sheria, na aheshimu
Mamlaka!
 
Naibu Waziri wa mambo ya ndani mwaka 2015 alisema kuanzia January ya 2016 watapita mtaa kwa mtaa kukagua wakazi ambao hawana vibali wachina wakauza bidhaa fasta fasta ili wapunguze hasara ila mwaka ukaisha bila oparesheni yoyote Leo imeibuka Na Manji
 
Tatizo Diwani wetu inasemekana pia ana uraia mwingine wa Marekani, yaani sijui atakimbilia wapi maana kule kuna Trump ataki utani uku kuna Magufuri nae vile vile hataki utani kabisa
huu uraia wa 2 2 ni wa malkia mkuu eti na mimi ninasikia.
 
Manji sio Managing Director,yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Quality Group Limited ...wangeanza na MD na sio Mwenyekiti wa bodi,wamemkosa kwenye madawa wameamua kumtafuta kwenye mengine,Mungu anawaona
 
Sasa hela zake imegeuka kuwa tusi tena??? Hawa watu walikua wapi mpaka wakaingia nchini?? Huyu uhamiaji alitakiwa akamatwe kwa kutotekeleza wajibu wake
 
Kinachonisikitisha ni hawa watu kuingiza siasa na ushabiki kwenye mambo ya msingi; inaonekana sasa kuweka watu ndani ndo sera ya serikali, anayekosea asipowekwa ndani ni kama vile wataonekana hawajafanya kazi sawasawa
Kuna mambo haya hitaji kukomoana, ni swala la kuelimishana na maisha yaendelee. serikali inapata kodi kutoka Quality group, kuna watu wameajiriwa kupitia Quality group....

nakumbuka kuna nchi fulani jamaa fulani alikamatwa kwa kutokulipa kodi nadhani, serikali ilichokifanya sio kumfilisi au kumkomoa ( sababu pia wanategemea kuendelea kupata mapato kutoka kwake, akifanikiwa zaidi ndivyo atalipa zaidi kodi) walimpangia muda, baada ya muda fulani uwe umelipa malimbikizi ya kodi yako.

Hapa kwetu nadhani tunataka wote tuwe masikini, na kama tukiwa wote masikini sijui serikali itakuwaje tajiri?? kodi watamdai masikini? Fikra zikigonga ukuta kwa utawaja wa chuki na kisasi basi wote tunajikuta tunaumia.
 
Tanamuhitaji kwa lipi labda kwa mfano.Funga bakuli lako your talking non sense suala la uhamiaji linazungumzika ???
Halafu halafu hakuna sababu ya kutumia lugha isiyo na staha! pinga hoja/mawazo/mtazamo kwa hoja/mawazo/mtazamo mbadala! Kama hujaelewa uliza!
 
Jifunze kujibu katika context!

Post yangu kabla ya hii nilliandika Manji kwa sasa ni shareholder, kwa hiyo hawezi kuhusishwa kwenye makosa ya kiutawala kupitia shares zake. Lakini kama hao watu walipewa vibali yeye akiwa kwenye utawala wa kampuni ana la kujibu.

Hapo juu nimejibu mtu anataka Manji asichukuliwe sheria kwa sababu ameajiri watu 5000. Halafu makosa yenyewe ni ya kuajiri wageni bila vibali! Crackpot reasoning!
sasa suala la wewe kupost kama yeye ni shareholder linahusiana vipi na hapa kwahiyo mimi nikae naperuzi contents unazopost wewe? stupid defense.
anyways vitu vingine haviihitaja rocket science kuviona au kuvielewa, sio kwamba nina support kosa, HAPANA. Tatizo lipo kwenye njia zinazotumika kutatua na kuwajibisha hao watenda makosa hili sakata linaendeshwa kwa chuki binafsi, statement zenyewe zinajionyesha...from coco beach to kunduchi issue, from madawa to uhamiaji.....Mdanganyika amka....usingizi uliolala ni mzito mno
 
Kuna Big Question Mark Kwenye Hii Saga.

Kwanza Passport Si Tanzania Iweje Immigration Officer Wa Tanzania Azisemee Passport Za Nchi Zingine Kuwa Ni Fake????

Pili Kwanini Amtaje Yusuf Manji Moja Kwa Moja Wakati Manji Ni advisor Tu Wa Quality Group Wakati Ameshajiuzuru Kuanzia Mwezi Wa 4 Mawaka Jana?

Tatu Kama Watumishi Hawana Vibali Basi Ni Kosa La Kiutawala Si La Mtu Binafsi

Nne Quality Group Ni Limited Company Iweje Umtaje Shareholder Mmoja Kuwa Ndiyo Muhusika Mkuu?

Ukifanya Kazi Kwa Hisia Au Kushurutishwa Kuna wakati Unajisahau Na Kupitiliza Mipaka

Nchi Hii Inapoelekea Ni Pabaya, Na Niaanza Kukumbuka Historia Ya Robin Hood Alongside His Band Of Merry Men.

201604191443.pdf
Kabla hujaanza kuuliza hayo masuala jiulize Kwanza unaemuuliza ni nani immigration na wewe ni nani immigration

ana elimu gani kwenye immigration na wewe una elimu gani kwenye immigration,

ana cheo gani immigration na wewe una cheo gani immigration,

kazi kaanza lini immigration na wewe kazi ulianza lini immigration.

Ukishapata majibu ya hayo maswali ndio uulize sasa maswali yako.
 
huu uraia wa 2 2 ni wa malkia mkuu eti na mimi ninasikia.
Alipataje huo Uraia pacha pasipo kushughulikiwa na hao uhamiaji kuhusika kwa njia moja au nyingine. Wasikomee QG tu waende kampuni zote nyingi tu. Kweli ukifuatwa na mbwa koko hakuachii kila unakokwenda anawewe.
 
Lakin Manji si alishajiuzulu uendeshaji wa hiyo kampuni ya familia? Au ndo anatafutwa kwa makosa milioni moja ili tu afungwe? Try him so many times until one sticks?
 
Gwajima kutoka smart ktk mikono ya hawa bwana nampa big up sana..issue ya kupekuliwa sio ya mchezo mchezo maana autokosekana ata chupa ya chai utaambiwa utoe risti yake...Muhind yupo ktk hali mbaya sana alijua mazoezi kumbe mechi sehem alizopita shortcut zote zitafumuliwa sasa usiombe ukutane na bwana Pepsi
Nikweli mkuu inaonekana Manji alizani hili game jepesi, hapo kila file litaguswa inabidi atafute njia mbadala ya kujikwamua.
 
Jamaa anaongea wazi akionyesha kuwa katumwa ....eti tulikuwa tumkamate jana as if hawajui alipo.....nawaambiaa akichomoa la madawa ya kulevya haya mengine mmechemsha...muache kumtumia 'mamsaidizi wa dereva wa daladala'kuwaumiza watu tumieni weredi wenu.Huyo maskini bado ni kijana mdogo after ten (10) years mzee ukishaondoka huyo kijana ataishi maisha ya akina Basil mramba wanayoishi sasa...bora wao walishajizeekea wala hawajutii kauli zao za kale

Mkuu miaka 10 mingi, huyu hatamaliza miaka 3 kwenye nafasi hiyo atang'olewa tu na huyu anaempa jeuri.
Halafu vita aliyoianzisha ni ya kisasi asipokuwa makini yaliyompata yule waziri aliyekwenda kupona India nae yanaweza kumpata, hili ndio nna shaka nalo kuliko jambo lingine lolote.
 
Back
Top Bottom