Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Wilaya ni kinondoni uende kuishi Chanika Una akili kweli weww
Mkuu umenichekesha sana. Ila mkuu haya mambo ni kama mapenzi. Wewe unaweza kuwa haumpendi fulan, lkn mungine akawa hasikii wala haambiliki kwa huyo usiompenda wewe.
 
Naona temeke imeangukia pua..kule ndio vilinge vya waganga..panya road..wala unga..singeri na malaya wachafu.

Kule uswahili mtupu na low minded people wamejazana huko.

Wajanja wapo kinondoni na wenye pesa bata zote za jiji la daslam ziko kinondoni.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ishu vipi wakuu,

Wakubwa leo kuna swali linalosumbua baadhi ya watu wanaoishi katika jiji letu kubwa la Dar es salaam. Swali lenyewe linahusu wilaya zetu tano za mkoa huu wa Dar es salaam. Yani wilaya

1) Kinondoni
2) Ilala
3) Ubungo
4) Temeke
5) Kigamboni

Swali lililopo ni watu kutaka kujua kati ya hizo wilaya tano ni wilaya gani ambayo inaongoza kuwa na sifa zifuatazo hapo chini:

a) Wajanja wengi.
b) Watu wenye vipato vya juu.
c) Mijengo ya maana.
d) Maendeleo yanayoonekana kama vile barabara nzuri, hospital na shule nzuri za serikali na private.
e) Miundo mbinu mizuri na hali ya hewa safi.
f) Upatikanaji wa maji na meme.
g) Kuchangamka kibiashara.
h) Vilevile ni sehem ipi katika wilaya hizo ambayo unaiona inafaa wewe binafsi kuishi aidha kwa kupanga au kwa kujenga nyumba yako mwenyewe?

Kwa wale ambao hawazifahamu vizuri kata za wilaya hizo naomba niziorodheshe hapo chini ili kuwarahisishia watu ambao hawafahamu kata fulan ipo katika wilaya fulan nk.

Kata za wilaya ya KINONDONI ni:
Kinondoni, Bunju, Hananasif, Kawe, Wazo, Kigogo, Kijitonyama, Kunduchi, Mabwepande, Magomeni, Makongo, Makumbusho, Mbezi juu, Mbweni, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Mzimuni, Ndugumbi, Tandale.

Kata za wilaya ya ILALA ni:
Ilala, Kariakoo, Buguruni, Gerezani, Chanika, Gongo la mboto, Jangwani, Kisutu, Kipawa, Kimanga, Kinyerezi, Kitunda, Kivukoni, Kiwalani, Majohe, Mchafukoge, Mchikichini, Msongola, Pugu, Segerea, Tabata, Ukonga, Upanga mashariki, Upanga magharibi, Vingunguti.

Kata za wilaya ya UBUNGO ni:
Ubungo, Kimara, Mbezi, Goba, Kibamba, Mabibo, Kwemba, Makuburi, Makurumla, Manzese, Mburahati, Msigani, Saranga, Sinza.

Kata za wilaya ya TEMEKE ni:
Temeke, Azimio, Buza, Chamazi, Chang'ombe, Tandika, Charambe, Keko, Kibonde maji, Kiburugwa, Kijichi, Kilakala, Kulungule, Kurasini, Makangarawe, Mbagala, Mbagala kuu, Mianzini, Miburani, Mtoni, Sandali, Toangoma, Yombo vituka.

Kata za wilaya ya KIGAMBONI ni:
Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Kimbiji, Kisarawe, Pembamnazi, Somangila, Tungi, Vijibweni.

Wakuu wenye uelewa mpana na jiji letu, pamoja na wilaya zetu karibuni tuchangie ili tupate kujua wilaya ipi inayobeba hadhi nzima ya jiji letu la Dar es salaam na nchi kwa ujumla.
Kwa taarifa yako ndani ya Dar jiji ni Ilala pekee yake,kinondoni ,ubungo,kigamboni uko ni manispaa...

Ilala ndio jiji

Ilala ndio jiji

Ilala ndio jiji

POSTA,KARIAKOO,UPANGA, ILALA BOMA Yote ile ndio Jiji lenyewe

Jengo moja tu kule posta kama yale ya pssf twin towers yanatumia umeme sawa na mkoa wa Lindi...Usipachukulie kawaida
 
Naona temeke imeangukia pua..kule ndio vilinge vya waganga..panya road..wala unga..singeri na malaya wachafu.

Kule uswahili mtupu na low minded people wamejazana huko.

Wajanja wapo kinondoni na wenye pesa bata zote za jiji la daslam ziko kinondoni.

#MaendeleoHayanaChama
Uwezekano wa Kinondoni kuibuka kidedea katika mchabango huu ni mkubwa, ikifuatiwa kwa mbali kidogo na Ilala. Temeke huenda ikawa nyuma hata ya Kigamboni ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.
 
Kwa taarifa yako ndani ya Dar jiji ni Ilala pekee yake,kinondoni ,ubungo,kigamboni uko ni manispaa...

Ilala ndio jiji

Ilala ndio jiji

Ilala ndio jiji

POSTA,KARIAKOO,UPANGA, ILALA BOMA Yote ile ndio Jiji lenyewe

Jengo moja tu kule posta kama yale ya pssf twin towers yanatumia umeme sawa na mkoa wa Lindi...Usipachukulie kawaida
Mkuu huu mtizamo wako sipingani nao, ila ngoja tutaangalia katika comments za wachangiaji wengine ili tuone wapi panakimbiza kutokana na sifa zilizoorodheshwa hapo juu.
 
Back
Top Bottom