Hivi karibuni tumeona vijana wawili walioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baadaye wakafukuzwa kwa utovu wa nidhamu, wakionekana kuwa mtaji MKUUUUUUUUUUUUUUUUUBWA kabisa wa kisiasa wa Chama cha Mapinduzi.
Vijana hawa, kwa sasa hivi kwenye majukwaa ya siasa ya CCM wamechukua hata nafasi za wazee, akina Mangula na Kinana.
Wengine wanaweza kusema mie mzushi au napiga propaganda. Jamani tuwe wakweli. Changamoto gani kubwa iliyokuwa ikiikabili CCM kuliko kujaribu kurudisha jiji la Arusa mikononi mwao kwa kushinda viti ya Udiwani? Hii ndio sehemu ambayo unatumia silaha zako bora kabisa. Tena Katibu Mkuu hapo ni nyumbani kabisa, na mcheza kwao hutuzwa, lakini hakuonekana kabisa. Mzee Mangula Makamu wa Mwenyekiti, huenda alikuwa na kazi nyingi ofisini mwake, tunamsamehe.
Bila shaka nguvu ya vijana ilihitajika. Chama hiki kikongwe kuliko vyote barani Afrika kimekuwa na utamaduni wa muda mrefu wa kutayarisha vijana. Wengine hata wanapata mafunzo ya kutumia silaha kwa ajili ya kukihami chama na kwa kidhungu wanawaita Greenguards. Wazee wa chama waliangalia huku na kule hawakupata watu wa kuwaamini. Hawakuamini malezi yao. Waliona maandalizi yao yana kasoro. HAKUNA MWANA UVCCM orijino aliyefuzu kupewa majukumu!
Wazee waliposhindwa kupata mavuno mazuri toka mashamba yao, wakaambiwa kuna bidhaa ready made. Unahitaji tu kulipa. Vijana walioandaliwa na chama kidogo kinachokera sana. Vijana ambao wana gubu la kufukuzwa kutoka uongozi wa umoja wa vijana wa chama hicho kwa utovu wa nidhamu.
Wazee wakawaona kuwa hao ndio wenyewe, kwa kuwa CCM sasa inahitaji kampeni zinazoweza kufanywa na watu wasio na adabu, wasio na haya, wasio na nidhamu. Kampeni za kusema watu. Kampeni za majitaka. Wakapewa boss ambaye ana sifa zote hizo.
Hawa ndio wakaenda Arusha, kujaribu kurudisha madiwani wa CCM kwenye manispaa ya Arusha. Wakaenda wakiahidi kutumia vipaji vyao vyote, kuhakikisha CCM inashinda. Walitoa kashfa nyingi kwa maisha binafsi ya Dr. Slaa, walitoa yale waliyoyaona ni mapungufu makubwa ya uongozi wa Dr. Slaa, walikosoa muundo wa uongozi wa chama n.k.
Bahati mbaya ajali zilianza kutokea katika kikosi hiki kilichoaminiwa na chama Tawala. Mtela Mwampamba alihukumiwa kifungo cha mwezi mmoja kutokana na kuwa MUONGO, na UONGO wake ukathibitishwa pasipo kiwingu cha mashaka. Wakati bado timu ya kampeni ya CCM ikiuguza majeraha ya majeruhi Mtela, ajali nyingine ikatokea. Mheshimiwa Mbunge, na Naibu Katibu Mkuu akajikuta ameshindwa kujizuia kuonesha kipaji chake kikubwa, ufundi wa KUTUKANA MATUSI ya NGUONI. Akadhihirisha kipaji chake hadharani na kwa bahati mbaya ikawa hapa JF. Naye akahukumiwa kifungo cha mwezi mmoja.
Mpiga kampeni aliyebaki akawa Juliana Shonza. Naye siku ya Jumapili akaianza kwa majigambo akituletea uzi
CCM kuibuka kidedea uchaguzi Arusha.
Aliendelea kuwepo hadi vituo vilipotangaza matokeo. Mpaka sasa hajajitokeza tena.
Maswali yangu:
Je CCM mlijua ni uwanja wa siasa au wa mipasho? Mbona basi mllituletea watu waliokubuhu kwa mipasho badala ya sera? Mbona mlituletea waongo? Mbona mlituletea watukanaji? Mlitegemea kuvuna zabibu kwenye shamba la miiba?
Poleni sana.
NAWASHAURI MUENDELEE KUWATUMIA HAO MAKADA WENU KWENYE MAJUKWAA YA SIASA!!
.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI