Mangula na Kinana mmejidhalilisha

Mangula na Kinana mmejidhalilisha

Wana jf

CCM chini ya Mzee wa pembe za ndovu imepanga mipango mikali sana jamaa wa ndani sana amenitonya kama ifuatavyo:
1. Wanasema kuwa lazima CHADEMA ife kabla ya zoezi la kuteu wagombea wa uraisi na ubunge kutoka vyama kwa uchaguzi 2015 halijafika wala kukaribia, kwa kuwa eti ikifikiwa wakati huo na CDM kikiwa na nguvu iliyonayo sasa hivi, eti
CCM itasambaratika yenyewe na ndio itakuwa mwisho wake.Hii wanasema ni kutokana na mgawanyiko uliopo sasa hivi,Kwa mtazamo huo jamaa kaniambia wamekuja na plan A na B. Plan A ni kuwabambika kesi viongozi wote wa CHADEMA ili wawe wanahangaika na kesi na fedha zote ziishie kwenye kesi wakose muda wa kufanya mikutano ya kushawishi wananchi,kuongea na wamiliki wa vyombo vya habari kupunguza kabisa kuandika habari ya CDM na kuanzisha vipindi kwenye redio wakati wa asubuhi na jioni vyenye lengo ya kuzunguzia amani kwa lengo la mlango wa nyuma wa kuiponda CHADEMA. Kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani kuiponda chadema hasa class mate wangu pale UDSM Mbatia. Jamaa akaniambia kama plan A itashindikana plan B watadili na Dr Slaa moja kwa moja watadili naye vipi hakunitonya. Tafakari chukua hatua.

tabia na mwenendo huu wa ccm na serikali hii unathibitisha bila shaka tetesi zako. ccm kutumia dola pinda kukatatamaa nahata kuvunja katiba eti pigeni tu tumechoka ni uthibitisho tosha uwepo wa mipango hio ya kuhujumu cdm. ccm watashindwa kwasababu wanatumia kichwa kufugia chawa badala ya kutumia kichwa kuwaondolea umaskini wa kupindukia watanzania.
 
Majinga kweli badala ya kuwasaidia wananchi ili wananchi warudishe imani kwao wanawatafuta Cdm.Ccm mbaya wake ni kutotmiza ahadi kwa wananchi na siyo Cdm
 
Yaaaaani, waasianze na Dr. Slaa wao wakitaka watuuwe wanachadema woooote popote pale tulipo hapa duniani wabaki kina Abdul Kindovu na timu yao.
 
Tayari hiyo ya amani imeshaanza kufanya kazi kwa Bidii kwelikweli...siku hizi weny eakili ndogo wakaiongelea amani lazima wachangie na aspect moja ya CDM..

Wajinga wengi sana wameshaingia ktk line..wengi watapoteza reputations ndogo walizo nazo.
 
CCM ni sikio la kufa! kamwe haliwezi kusikia dawa.....
 
Unajua kati ya hawa hakuna mzima hata mmoja tena lisu ndiyo kabisa mtagota tu.

ktk miaka 36 ya chama cha mapinduzi hakijapa bahati ya kuwa na nondo km hao, huo ndio ukweli whether you like o not CCM kinakimbiwa na wasomi wote makini na kiliobakiwa nao wote ni wababaishaji wasiojielewa ata kidogo period.
 
Problem is, the ones "UP THERE" in ZZM ni wale WALIOCHOKiA, and they confessed, they can't even think well if they feel threatened they throw a fist instead of coming up with new strategies or being bipartisan for the good of the country. Soo dumb!
 
Wana jf

CCM chini ya Mzee wa pembe za ndovu imepanga mipango mikali sana jamaa wa ndani sana amenitonya kama ifuatavyo:
1. Wanasema kuwa lazima CHADEMA ife kabla ya zoezi la kuteu wagombea wa uraisi na ubunge kutoka vyama kwa uchaguzi 2015 halijafika wala kukaribia, kwa kuwa eti ikifikiwa wakati huo na CDM kikiwa na nguvu iliyonayo sasa hivi, eti
CCM itasambaratika yenyewe na ndio itakuwa mwisho wake.Hii wanasema ni kutokana na mgawanyiko uliopo sasa hivi,Kwa mtazamo huo jamaa kaniambia wamekuja na plan A na B. Plan A ni kuwabambika kesi viongozi wote wa CHADEMA ili wawe wanahangaika na kesi na fedha zote ziishie kwenye kesi wakose muda wa kufanya mikutano ya kushawishi wananchi,kuongea na wamiliki wa vyombo vya habari kupunguza kabisa kuandika habari ya CDM na kuanzisha vipindi kwenye redio wakati wa asubuhi na jioni vyenye lengo ya kuzunguzia amani kwa lengo la mlango wa nyuma wa kuiponda CHADEMA. Kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani kuiponda chadema hasa class mate wangu pale UDSM Mbatia. Jamaa akaniambia kama plan A itashindikana plan B watadili na Dr Slaa moja kwa moja watadili naye vipi hakunitonya. Tafakari chukua hatua.

Katika RED ni kujidandanya sana kwa hawa CCM. Hivi hawa watu bado hawaamini tu kuwa CDM ni chama cha wananchi na kwa hiyo mtaji wao ni wananchi???......Aisee ukitenda wema UTAPENDWA tu na ukidharau watu,ukipenda kubeza watu,ukinyanyasa watu UTACHUKIWA TU UPENDE USIPENDE na usiombe hili likakutokea katika maisha yako......hiki ndicho kinachowatokea CCM. Kwa hili wasahau CHADEMA hawawezi kuishiwa fedha hata kama "watawabambikia" viongozi wetu wote kesi....na mbona inakuwa kama hawajui; tangu lini cha "Kumbakika" kikawa kweli??

Katika GREEN hiyo wasahau kabisa kwa sababu MUNGU HUYU tunayemjua sisi na tunayemwabudu KAMWE HAWEZI kuwaruhusu kufanya ujinga kama huu!!.... Tunajua kuwa wanamtafuta sana hata leo na lengo lao ni kumuua. Wasifikiri kwamba wao tu ndiyo wenye vichwa vyenye nywele, wasifikiri kwamba hii Tanganyika ni yao na watoto wao...Hii ni nchi yetu wote....Na ukipiga na wewe utapigwa tu,ukiheshimu na wewe utheshimiwa tu
....That's human being nature!!!.
 
Kwa hiyo kwa Mbatia kuipinga Red Brigade ina maana ameanza kutekeleza mkakati huo?

mkuu take it from me mbatia ni hatari.nawaambia cdm wawe makini na mtu huyu.tangu nccr iundwe hajaondoka.waanzilishi wote wengine wamekimbia.nadhani nimeeleweka.
 
tupo tayari kwa hayo yote.chadema kimeshavuka level hiyo.sitaendelea zaidi ya hapa

wajina hakiya mungu tena ccm ikishinda 2015 lazima tujiulize kulikon nimepita vijiji kadhaa jimbo la mtera kila nikiwauliza wazee vip mbunge wetu anafanya kazi? Wanajibu cdm itafanya kazi lusinde kashindwa,na hiyo taswira si mtera tu,ni karibu kila mahali walipo rafik zangu wananitonya kuwa kama maisha yatakuwa hv 2015 kuna mageuz makubwa kwan raia wamechoka.
 
:rip:
Hili jambo ni gumu sana yani kama mimi CDM hawanijiu lakini kila ninapokaa na watu wapya nahakikisha natoa elimu ya uraia, yaani mimi nimeapa ni mtu kwa mtu mpaka siku Uongozi unaomjali mwananchi upatikane.

nawashauri wengine wapenda haki tusisubiri M4C ya viongozi wa CDM bali kwenye mitaa yetu na vijijini kwetu ni elimu ya uraia hasa ya kupiga kura ni muhimu.

UMENENA MKUU.BIG UP SANA.TUSISUBIRI M4C.KILA UNAPOKAA TOA ELIMU YA URAIA KWA NGUVU.LENGO LAO NI KUWAKAMATA VIONGOZI MUHIMU WA CDM.WASHINDWE NA WALEGEE.TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
 
Hivi karibuni tumeona vijana wawili walioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baadaye wakafukuzwa kwa utovu wa nidhamu, wakionekana kuwa mtaji MKUUUUUUUUUUUUUUUUUBWA kabisa wa kisiasa wa Chama cha Mapinduzi.

Vijana hawa, kwa sasa hivi kwenye majukwaa ya siasa ya CCM wamechukua hata nafasi za wazee, akina Mangula na Kinana.

Wengine wanaweza kusema mie mzushi au napiga propaganda. Jamani tuwe wakweli. Changamoto gani kubwa iliyokuwa ikiikabili CCM kuliko kujaribu kurudisha jiji la Arusa mikononi mwao kwa kushinda viti ya Udiwani? Hii ndio sehemu ambayo unatumia silaha zako bora kabisa. Tena Katibu Mkuu hapo ni nyumbani kabisa, na mcheza kwao hutuzwa, lakini hakuonekana kabisa. Mzee Mangula Makamu wa Mwenyekiti, huenda alikuwa na kazi nyingi ofisini mwake, tunamsamehe.

Bila shaka nguvu ya vijana ilihitajika. Chama hiki kikongwe kuliko vyote barani Afrika kimekuwa na utamaduni wa muda mrefu wa kutayarisha vijana. Wengine hata wanapata mafunzo ya kutumia silaha kwa ajili ya kukihami chama na kwa kidhungu wanawaita Greenguards. Wazee wa chama waliangalia huku na kule hawakupata watu wa kuwaamini. Hawakuamini malezi yao. Waliona maandalizi yao yana kasoro. HAKUNA MWANA UVCCM orijino aliyefuzu kupewa majukumu!

Wazee waliposhindwa kupata mavuno mazuri toka mashamba yao, wakaambiwa kuna bidhaa ready made. Unahitaji tu kulipa. Vijana walioandaliwa na chama kidogo kinachokera sana. Vijana ambao wana gubu la kufukuzwa kutoka uongozi wa umoja wa vijana wa chama hicho kwa utovu wa nidhamu.

Wazee wakawaona kuwa hao ndio wenyewe, kwa kuwa CCM sasa inahitaji kampeni zinazoweza kufanywa na watu wasio na adabu, wasio na haya, wasio na nidhamu. Kampeni za kusema watu. Kampeni za majitaka. Wakapewa boss ambaye ana sifa zote hizo.

Hawa ndio wakaenda Arusha, kujaribu kurudisha madiwani wa CCM kwenye manispaa ya Arusha. Wakaenda wakiahidi kutumia vipaji vyao vyote, kuhakikisha CCM inashinda. Walitoa kashfa nyingi kwa maisha binafsi ya Dr. Slaa, walitoa yale waliyoyaona ni mapungufu makubwa ya uongozi wa Dr. Slaa, walikosoa muundo wa uongozi wa chama n.k.

Bahati mbaya ajali zilianza kutokea katika kikosi hiki kilichoaminiwa na chama Tawala. Mtela Mwampamba alihukumiwa kifungo cha mwezi mmoja kutokana na kuwa MUONGO, na UONGO wake ukathibitishwa pasipo kiwingu cha mashaka. Wakati bado timu ya kampeni ya CCM ikiuguza majeraha ya majeruhi Mtela, ajali nyingine ikatokea. Mheshimiwa Mbunge, na Naibu Katibu Mkuu akajikuta ameshindwa kujizuia kuonesha kipaji chake kikubwa, ufundi wa KUTUKANA MATUSI ya NGUONI. Akadhihirisha kipaji chake hadharani na kwa bahati mbaya ikawa hapa JF. Naye akahukumiwa kifungo cha mwezi mmoja.

Mpiga kampeni aliyebaki akawa Juliana Shonza. Naye siku ya Jumapili akaianza kwa majigambo akituletea uzi CCM kuibuka kidedea uchaguzi Arusha.

Aliendelea kuwepo hadi vituo vilipotangaza matokeo. Mpaka sasa hajajitokeza tena.

Maswali yangu:

Je CCM mlijua ni uwanja wa siasa au wa mipasho? Mbona basi mllituletea watu waliokubuhu kwa mipasho badala ya sera? Mbona mlituletea waongo? Mbona mlituletea watukanaji? Mlitegemea kuvuna zabibu kwenye shamba la miiba?

Poleni sana.

NAWASHAURI MUENDELEE KUWATUMIA HAO MAKADA WENU KWENYE MAJUKWAA YA SIASA!!

.
992814_508888975850421_972006896_n.jpg

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Mipango ya mfa Maji haishi kutapatapa. Kama ni kesi tayari ziko nyingi. Tunajua Mipango iliyopo Kama ya 15 june2013 Na kumtumia Tendwa. Yote itashindwa.
Tumeanza Na Mungu, tupo Na Mungu na tutamaliza na Mungu.
 
hizi plan ni failure kama zile za REPOA NA MKUKUTA NA MKURABITA INSHORT CCM INAOMBOLEZWA KIFO CHAKE DODOMA.RIP CCM.
 
Well said mkuu!na hapo ndipo wanapokosea!badala wajiimarishe wao wanatumia muda mwingi na nguvu nyingi kuishambulia Chadema

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Waache waongeee muda huu, Muda punde ujao makundi yao yakianza ndo wengine watakisapoti CDM kukua badala kukifuta. Na kama kweli Msajili atakifuta, atakuwa ametenda kosa kubwa kuliko yote yaliyowahi kutendwa nchini na huenda likaingiza nchi katika matatizo.
 
Kwa mbinu za kitoto namna hiyo hata CCK hakiwezi kufa, mi nawashauri CCM na serikali yake kwamba kama wana pesa za kutosha wafufue viwanda ili vijana wapate ajira.Vinginevyo habari za vijana wetu kunyongwa nje ya nchi kwa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya zitakuwa pambio!
 
Wana jf

CCM chini ya Mzee wa pembe za ndovu imepanga mipango mikali sana jamaa wa ndani sana amenitonya kama ifuatavyo:
1. Wanasema kuwa lazima CHADEMA ife kabla ya zoezi la kuteu wagombea wa uraisi na ubunge kutoka vyama kwa uchaguzi 2015 halijafika wala kukaribia, kwa kuwa eti ikifikiwa wakati huo na CDM kikiwa na nguvu iliyonayo sasa hivi, eti
CCM itasambaratika yenyewe na ndio itakuwa mwisho wake.Hii wanasema ni kutokana na mgawanyiko uliopo sasa hivi,Kwa mtazamo huo jamaa kaniambia wamekuja na plan A na B. Plan A ni kuwabambika kesi viongozi wote wa CHADEMA ili wawe wanahangaika na kesi na fedha zote ziishie kwenye kesi wakose muda wa kufanya mikutano ya kushawishi wananchi,kuongea na wamiliki wa vyombo vya habari kupunguza kabisa kuandika habari ya CDM na kuanzisha vipindi kwenye redio wakati wa asubuhi na jioni vyenye lengo ya kuzunguzia amani kwa lengo la mlango wa nyuma wa kuiponda CHADEMA. Kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani kuiponda chadema hasa class mate wangu pale UDSM Mbatia. Jamaa akaniambia kama plan A itashindikana plan B watadili na Dr Slaa moja kwa moja watadili naye vipi hakunitonya. Tafakari chukua hatua.
Sawa... Ila wamesahau methali moja fupi tu; Kumpiga chura teke, ni kumuongezea hatua"...
 
Back
Top Bottom