Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!
Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!
Leo makamu m/kiti CCM ndg Mangula leo alisikika katika vyombo vya habari kuna watu wanaleta uasi ndani ya CCM. Akawafananisha na waasi wa Somalia. Waasi hao ni wale wanaohangaika na urais. Lowassa ni miongoni mwa wana CCm wasiojificha kutafuta nafasi hiyo.
Ndani ya CDM kuna Zitto aliyeanzisha uasi kwa kusaliti harakati ya chama. Jambo la kumshukuru Mungu ni KK kumshughulikia ZZK mpaka kakimbilia mahakamani lakini haisaidia. Tunamshughulikia vilivyo. Magamba wamejitahidi sana kumtetea ZZK lakini naona wamezidiwa na makamanda.
Kwa kuwa CCM nayo ina muasi wake, nawashauri CCM members onesheni uimara wa chama kumshughulikia muasi Lowassa ( Machar) Mkifanya hivyo tutawaamini na ninyi mpo.
Mangula naye bwana, ubunge tu alikosa sasa haya ya urais anayajua kweli??? atuachie babamkwe wetu, tuje tufanye tuliyomfanyia mkwila kule Arumeru
hakuna muasi CCM hayo yote ni upotoshaji na wala CCM huwezi kuilinganisha na hiyo SACCOS ya kasikazini. Rais mwenyewe aliwahi kusema kwamba sasa kupitapita kunaruhusiwa. Acha kulinganisha mlima na punje ya mchanga. na hata huyo Zitto mnamtia fitina na mwisho mnabaki kuaibika.
LoL!!! Kama hili ni kweli basi Ngoma inogile.
CC: Kambi ya fisadi Lowassa
Huyo ni Mangula. Kikwete anamwabudu sana Lowassa
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
HUYO NI Mangula wa nyumbani KWAKO,NA SII mzee Philip Mangula tunayemjua SISI,MWINGI wa HEKIMA,anavyo VIKAO VYA kuongelea,Hana SABABU ya kuyaongea hayo uliyomlisha,shame on you mleta MADA
Ni kweli, na nimemuomba mode aufunge!.Pasco amekasirishwa sana na hii post.
hakuna muasi CCM hayo yote ni upotoshaji na wala CCM huwezi kuilinganisha na hiyo SACCOS ya kasikazini. Rais mwenyewe aliwahi kusema kwamba sasa kupitapita kunaruhusiwa. Acha kulinganisha mlima na punje ya mchanga. na hata huyo Zitto mnamtia fitina na mwisho mnabaki kuaibika.